Abiria wa Tanzania akamatwa Hong Kong na heroin ikiwa ndani ya mashine

Abiria wa Tanzania akamatwa Hong Kong na heroin ikiwa ndani ya mashine

Aiseee nadhani mh mwakyembe ana hitaji msaada kwenye hii vita?

atajijuwa mwenyewe, hata akihitaji sitamsaidia, maana same people who created the same problem are the ones pretending to solve the same problem.

shauri yake!
 
akamatwe ridhiwani kikwete ndo tutaona mnajua kufanya kazi, sio kukomaa na vidagaa tu...
 
Hii machine mbona Kama imechakaa ghafla baada ya kukata hicho Chuma au ilifungwa hapo kwanza kisha kikahamishiwa katika machine nyingine! Tazama kwa umakini hizo picha.

Ni kweli Yahaya hizo mashine ni tofauti ila haiondoi ukweli wa tukio,cha kuangalia sasa ni uhalali wa wamiliki wa passport zetu maana kuna watu wa mataifa fulani reputation yao ni mbaya abroad na ujanja wanaotumia ni kujificha kwenye uraia wa nchi zinazoaminika na kufanya maovu!
 
Yale yale watu wanaofanya ujambazi huko misitu ya Biharamulo ni Wanyarwanda, wanaofanya uhalifu Arusha ni Wakenya, nk. Wabongo tuna mtazamo mmoja finyu sana wa kujiaminisha kuwa Mtanzania ni malaika, hayo mazagazaga ni watu wengine! Sisi huwa hatufanyi uhalifu! Je wale mabinti wasanii akina Masozange waliokamatwa SA ni Wanyarwanda au Wakenya, Wasomalia?

Sikatai kuwa watz wapo wamnaofanya hii biashara isipokuwa idadi yao inaweza kuwa exaggerated na wasio watz walionunua hizo passport,unaposafiri hizo int airports sio tukio la ajabu kukuta mtu kabeba passport ya Tz ila msalimie usikie kama atawezajibu chochote!
 
Hili Bomu litatumaliza haswa, Picha mbaya sana kwa dunia.
Viongozi wa Nchi Mpo wapi ??

Kwa mara nyingine, maafisa wa Hong Kong katika kiwanja cha ndege wamefanikiwa kukamata dawa za kulevya zilizokuwa zinasafirishwa kutokea Tanzania safari hii zikiwa zimefichwa katikati ya chuma cha mashine.

Dawa hizo aina ya heroin zilikamatwa katika nyakati mbili tofauti kwa jumla zikiwa na kilo 1.5 na thamani ya dola milioni 1.3 za Marekani.

Maafisa hao wanasema kwa kuwa wamekuwa wakifuatilia kwa karibu nyendo za wauza dawa na mbinu za kuficha dawa hizo, walilazimika kukikata chuma cha mashine hiyo ili kuziona.

Adhabu ya kupatikana na dawa za kulevya huko Hong Kong ni faini ya dola milioni 5 za Kimarekani.

Taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya Serikali ya nchi hiyo na picha zinazoambatana na taarifa hiyo vimepachikwa hapo chini.

6366947_orig.jpg

8940017_orig.jpg

8668822_orig.jpg
 
Ni kweli Yahaya hizo mashine ni tofauti ila haiondoi ukweli wa tukio,cha kuangalia sasa ni uhalali wa wamiliki wa passport zetu maana kuna watu wa mataifa fulani reputation yao ni mbaya abroad na ujanja wanaotumia ni kujificha kwenye uraia wa nchi zinazoaminika na kufanya maovu!

Sawa walitokea uwanja upi wa ndege??!!
 
Toka lini kifaa kinunuliwe Tanzania kitumwe China mbona vice-versa

Tanzania hawana mitambo ya kuona madawa yaliyofichwa namna hiyo.

Hakika Wewe ni Great Thinker! Good observation Mkuu! Yani mashine imenunuliwa Tanzania inapelekwa China! Au ni biashara ya chuma chakavu?????
 
Kwa mara nyingine, maafisa wa Hong Kong katika kiwanja cha ndege wamefanikiwa kukamata dawa za kulevya zilizokuwa zinasafirishwa kutokea Tanzania safari hii zikiwa zimefichwa katikati ya chuma cha mashine.

Dawa hizo aina ya heroin zilikamatwa katika nyakati mbili tofauti kwa jumla zikiwa na kilo 1.5 na thamani ya dola milioni 1.3 za Marekani.

Maafisa hao wanasema kwa kuwa wamekuwa wakifuatilia kwa karibu nyendo za wauza dawa na mbinu za kuficha dawa hizo, walilazimika kukikata chuma cha mashine hiyo ili kuziona.

Adhabu ya kupatikana na dawa za kulevya huko Hong Kong ni faini ya dola milioni 5 za Kimarekani.

Taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya Serikali ya nchi hiyo na picha zinazoambatana na taarifa hiyo vimepachikwa hapo chini.

6366947_orig.jpg

8940017_orig.jpg

8668822_orig.jpg

Ndugu ebu tuweke wazi mbona hizo mashine ni tofauti? hiyo nzima hailingani na hiyo iliyokatwa inawezekana kuna udanganyifu wa picha ingawa taarifa inaweza kuwa ya kweli.
 
Mwakyembe si anakesha hapo kiwanjani..sasa huyu kapitia wapi tena?

Jamani Wachina wa Hong Kong wameshangaa ni aje chuma itoke Tz kwenda kwao badala ya kutoka kwao kwenda Tz!

Hii inaonyesha kuwa wauza unga wanaanza kuishiwa mbinu!

Mr dhaifu huwezi kuwa dhaifu kwa kila kitu daaah mpaka kwenye hili still unaendekeza udhaifu wako tu
 
Ndugu ebu tuweke wazi mbona hizo mashine ni tofauti? hiyo nzima hailingani na hiyo iliyokatwa inawezekana kuna udanganyifu wa picha ingawa taarifa inaweza kuwa ya kweli.

Mkuu nitajaribu kukueleza kwa kadiri nilivyoelewa:

1. Picha ya kwanza na ya pili ni picha mbili tofauti zioneshazo matukio mawili tofauti ya ukataji chuma.

2. Chuma kinachoandaliwa kukatwa katika picha ya kwanza ni tofauti na kile kilichokwishakatwa katika picha ya pili.(kulikuwa na vyuma viwili tofauti vilivyoshindiliwa dawa).
Jaribu kuvichunguza kwa makini utagundua havifanani.

3. Ukisoma kwa makini yale maelezo yaliyopo katika picha yenye maelezo utaona wamebainisha wazi kabisa utofauti wa tarehe baina ya tukio la kwanza na lile la pili. Ufanano wa matukio hayo mawili upp sehemu moja tu, njia iliyotumika kuyaficha madawa hayo inafanana.

4. Hivyo basi kutokana na maelezo namba 1, 2 na 3, ni wazi utagundua kuwa hakuna udanganyifu wowote kwani hayo ni matukio mawili tofauti. Kwa mantiki hiyo hata mashine za ukataji kuna uwezekano zikawa zaidi ya moja.
 
Hapo jamaa wakabonyezana kwa kumwona Mtz analeta utani kwa kusafirisha mashine kutoka Africa kupeleka nchi za watu ambako ndiko zinakotokea, ni sawa kama mtu anapakia ndizi kwenye behewa anatoa Dar anapeleka Bukoba lazima wakuangalie mara mbilimbili
 
Back
Top Bottom