Absalom Kibanda akamatwa!

Absalom Kibanda akamatwa!

Jeshi la polisi linamshikilia mhariri wa gazeti la Tanzania Daima, A. Kibanda kwa tuhuma za uchochezi. Kibanda anashikiliwa kwenye makao makuu ya polisi jijini Dar es Salaam.

===============

UPDATES

Habari zilizonaswa sasa hivi kutoka makao makuu ya polisi Dar zinasema Mhariri wa Tz Daima Absalom Kibanda ameachiwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa na polisi kwa zaidi ya masaa matatu kwa tuhuma za uchochezi. Amedhaminiwa na Mhariri wa Mwanahalisi Saed Kubenea kwa dhamana ya Sh 5,000,000/-. Kibanda anatakiwa kuripoti polisi hqtrs Jumatatu asubuhi.

Kama nilivyoeleza hapa: JOHN MNYIKA: Mwigamba apata dhamana; tuepuke dola ya kipolisi taratibu watawala wetu wanatupeleka kuwa na dola ya kipolisi. Mwaka 2008 walivamiwa Kubenea, Ndimara na Ofisi ya Mwanahalisi nilisema kwamba lile lilikuwa na shambulio dhidi ya uhuru wa kikatiba na haki za msingi wa kutoa na kupata habari. Matukio ya kukamatwa kwa Mwigamba na sasa Kibanda kutokana na makala ni kamata kamata ya vyombo vya dola dhidi ya uhuru wa kutoa maoni na kuwasiliana.

Ni dalili mbaya wakati huu ambapo kuna sheria mbovu kama ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011 yenye kifungu chenye kutoa adhabu ya kifungo cha hadi miaka 7 au faini ya hadi milioni 15 kwa makosa ya kukusanya maoni au kutoa elimu juu ya mabadiliko ya katiba kinyume cha sheria husika.

Kama kuandika makala tu kuhusu polisi kwa masuala ambayo hayana mwelekeo wa uchochezi au uhaini kama inavyodaiwa tayari vyombo vya dola vimeanza kamata kamata hatma ya mchakato wa katiba na masuala mengine ya kitaifa iko mashakani. Awali ilikuwa ni wananchi wa kawaida, wanasiasa wakiwemo wabunge, sasa wanahabari na hali hii itaendelea kwa wengine katika jamii kama tusipoungana pamoja kuidhibiti.


JJ
 
mwenye ile makala please aniwekee hapa nijue woga wote huu kwa CCM na serikali yake unatokana na nini?

Usiwe mvivu wa kusoma mkuu. Kabla ya kureply walau pitia page mbili tatu ili ujue kinachoendelea kabla ya kupost!! Ni Ushauri tu tena wa Bure!!!

 
Jeshi la polisi linamshikilia mhariri wa gazeti la Tanzania Daima, A. Kibanda kwa tuhuma za uchochezi. Kibanda anashikiliwa kwenye makao makuu ya polisi jijini Dar es Salaam. =============== UPDATES Habari zilizonaswa sasa hivi kutoka makao makuu ya polisi Dar zinasema Mhariri wa Tz Daima Absalom Kibanda ameachiwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa na polisi kwa zaidi ya masaa matatu kwa tuhuma za uchochezi. Amedhaminiwa na Mhariri wa Mwanahalisi Saed Kubenea kwa dhamana ya Sh 5,000,000/-. Kibanda anatakiwa kuripoti polisi hqtrs Jumatatu asubuhi.
Safi Kubenea,ila ukisoma ile makala ktk Tanzania Daima ilistahili Polisi wote wa vyeo vya chini wajitokeze kumdhamini kwani makala ile iliwazindua kutoka ktk fikra mfu
 
Kama nilivyoeleza hapa: JOHN MNYIKA: Mwigamba apata dhamana; tuepuke dola ya kipolisi taratibu watawala wetu wanatupeleka kuwa na dola ya kipolisi. Mwaka 2008 walivamiwa Kubenea, Ndimara na Ofisi ya Mwanahalisi nilisema kwamba lile lilikuwa na shambulio dhidi ya uhuru wa kikatiba na haki za msingi wa kutoa na kupata habari. Matukio ya kukamatwa kwa Mwigamba na sasa Kibanda kutokana na makala ni kamata kamata ya vyombo vya dola dhidi ya uhuru wa kutoa maoni na kuwasiliana.

Ni dalili mbaya wakati huu ambapo kuna sheria mbovu kama ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011 yenye kifungu chenye kutoa adhabu ya kifungo cha hadi miaka 7 au faini ya hadi milioni 15 kwa makosa ya kukusanya maoni au kutoa elimu juu ya mabadiliko ya katiba kinyume cha sheria husika. Kama kuandika makala tu kuhusu polisi kwa masuala ambayo hayana mwelekeo wa uchochezi au uhaini kama inavyodaiwa tayari vyombo vya dola vimeanza kamata kamata hatma ya mchakato wa katiba na masuala mengine ya kitaifa iko mashakani. Awali ilikuwa ni wananchi wa kawaida, wanasiasa wakiwemo wabunge, sasa wanahabari na hali hii itaendelea kwa wengine katika jamii kama tusipoungana pamoja kuidhibiti.


JJ

Mkuu Mnyika,

Wewe ndiye uliyesign yale makubaliano kati ya Serikali na CDM. Kwa kuwa inasemekana kuwa serikali imekwenda kinyume na makubaliano yenu, je unaweza kutupa dondoo za hayo makubaliano??

Binafsi mpaka sasa sielewi kwa nini mlikubali kusign!!
 
Ni lini mhariri wa UHURU atakamatwa kwa uchochezi?
 
Mwigamba hana kesi. Makala ni nzuri na ya kuelimisha. Hakuna uchochezi hapo. Kukamatwa kwake kunaashiria kufilisika kifikra kwa serikali ya magamba.
 
Btn now na 2015 watakamatwa watu wengi sana wenye kuipinga ccm na utawala wake... ndo dalili za sikio la kufa
 
Waraka maalumu kwa askari wote
By
Samson Mwigamba
MAKALA hii ilikuwa itoke
Jumatano ya wiki iliyopita
lakini kwa sababu za kiufundi
ikashindikana. Imekuwa ni
bahati nzuri kwamba
inapotoka leo, ijibu swali la askari polisi dereva wa gari la
maji ya kuwasha. Askari huyo alimweleza
Mwalimu Mkuu wa watu jinsi
roho inavyomuuma pale
anapowamwagia Watanzania
wenzake maji hayo ya
kuwasha wakati wakidai haki yao. Askari uliyeuliza na
wenzako wote someni makala
hii kwa utulivu. Huu ni waraka
maalumu kwa askari wote wa
majeshi yote vikosi vyote
Tanzania Bara na Visiwani. Kwa lugha ya wazi zaidi
nazungumza na askari wa
Jeshi la Polisi Tanzania, Askari
wa Jeshi la Kujenga Taifa,
askari wa Kikosi Maalumu cha
Kuzuia Magendo (KMKM), askari wa Jeshi la Magereza na
wale wa Jeshi la Wananchi
(JWTZ). Kuwa mwanajeshi lolote kati
ya hayo niliyoyataja si dhambi
na si kweli kwamba kuwa
mwanajeshi kunakuondolea
uwezo wa kufikiri na badala
yake ukawa unafikiriwa na watu wengine. Wala haimaanishi kuwa askari
kuwa kama robot ndio
nidhamu bora kuliko zote
duniani. La hasha! Mimi
nilikataa utumwa huo! Mwaka 1999 nilihitimu elimu
ya cheti cha ufundi mchundo,
yaani Full Technician
Certificate (FTC) katika
uhandisi wa Elektroniki na
Mawasiliano ya Anga, yaani Electronics &
Telecommunications
Engineering kutoka Taasisi ya
Teknolojia ya Dar es Salaam
(DIT). Nikiwa bado sijapata kazi ya
maana, mwezi Aprili mwaka
2000 niliona tangazo la kazi ya
Radio Technician katika Jeshi
la Magereza. Nikatuma
maombi na kuitwa kwenye usaili uliofanyika Chuo cha
Maofisa wa Jeshi la Magereza
Ukonga, Dar es Salaam mwezi
Juni 2000. Wote tuliofaulu usaili
tulipangiwa siku ya kuripoti
Chuo cha Magereza Kiwira kule
Tukuyu, Mbeya. Kufika kule nilishuhudia
mambo ya ajabu. Ingawa wao
hufurahia na kusema eti
wanakutoa uraiani na kuwa
mwanajeshi lakini baadhi ya
matendo yanayofanyika wakati wa mafunzo ya jeshi ni
ya kuwapumbaza askari wetu
ili baadaye wakiwa kazini,
watawala wawatumie
watakavyo. Nilishindwa kuvumilia
kaulimbiu ya wakufunzi wa
jeshi pale walipoelekeza
kwamba chochote kruta
(askari mpya mafunzoni)
unachoambiwa lazima uitikie “ndiyo afande”. Nilishindwa
kuitikia kwa mfano pale
mkufunzi mmoja mwenye
cheo cha koplo alipotutamkia
mfululizo wa sentensi
zifuatazo: Mkufunzi: Nyinyi makruta
mbona wote hamkuja na
majembe? Makruta: Ndiyo afande! Mkufunzi: Hamkuambiwa
makao makuu ya jeshi
kwamba lazima mje na
majembe? Makruta: Ndiyo afande! Mkufunzi: Kwa hiyo kwa
kuwa hamkuambiwa na
nyinyi hamkuyabeba? Makruta: Ndiyo afande! Mkufunzi: Wote ni
wapumbavu pamoja na mama
zenu waliowazaa. Makruta: Ndiyo afande! Ni hayo pamoja na mambo
mengine ya kulazimishwa
kwenda kwenye kile
kinachoitwa disko, ambapo
pamoja na uchovu wa kutwa
nzima wa kazi ngumu na nyingi bado ni lazima ukae
hapo mpaka saa 4 usiku tena
ukinyooshewa kidole tu na
mwenzako lazima usimame
na kuimbisha wimbo tena
kwa tabasamu, wimbo mmoja wapo ukisema “Magereza
ninavyokupenda nitakunywa
sumu juu yako”, ndiyo
yaliyonifanya nikakataa kazi
ya jeshi baada ya wiki moja tu
ya mafunzo. Siku niliyokataa jeshi ilikuwa
ni Jumatano asubuhi ambapo
sikwenda mchakamchaka na
wakati wenzako
wanatawanyika kufanya usafi
wa nje maeneo mbalimbali, mimi nilibeba begi langu na
kuanza kuondoka chuoni
majira ya saa moja na nusu
hivi asubuhi. Nilikamatwa na mkufunzi
mmoja wa jeshi na kupelekwa
pamoja na begi langu kwa
Ofisa Mafunzo wa chuo.
Aliponiuliza sababu nilimtajia
mbili, kwanza kwamba sifurahii mambo ya jeshi na
kubwa zaidi kwamba mimi ni
Msabato na nimeambiwa na
wenzangu kwamba hapa
hakuna kwenda kusali, siku
zote za juma ni kazi. Kitu ambacho sitaweza maana
Sabato takatifu lazima
nipumzike! Bila kuuliza zaidi
aliconclude kwa kuniambia
kwamba, “Sijawahi kuona
mtu anaacha kazi kwa ajili ya mambo ya dini. ”Ni dhahiri wewe ulikuja
kutupeleleza na hivyo kazi
yako imeisha sasa unataka
kurudi. Tutakuweka rumande,
tena ile ya polisi kwa wiki
mbili wakati tunafanya upelelezi juu yako.” Askari aliyenileta alianza
kunivuta ili kunipeleka
rumande lakini nilikataa huku
nikiendelea kujieleza kwa
ofisa mafunzo ili ajue kwamba
sikuwa na mpango huo aliousema. Baada ya kuelemewa na hoja
zangu alinipeleka kwa
makamu mkuu wa chuo
ambaye yeye alitumia zaidi
Biblia kunihubiri kwamba
nakaidi amri ya mamlaka wakati hakuna mamlaka
isiyotoka kwa Mungu. Jibu langu lilikuwa fupi na
lenye msimamo mzito
kwamba ikiwa mamlaka ya
wanadamu inafika mahali
inanena tofauti na Mungu,
Mtume Petro ametuandikia kwamba katika hali ya namna
hiyo, “Imetupasa kumtii
Mungu kuliko mwanadamu”. Na yeye alinishindwa
akanipeleka kwa mkuu wa
chuo na wao wote wakiwapo.
Ushauri waliokuwa wakimpa
mkuu wa chuo ni kwamba
mimi niwekwe rumande kwanza ili wafanye upelelezi.
Lakini sikuyumba katika
msimamo wangu. Nilimweleza mkuu wa chuo
kwamba mimi ni raia na si
mpelelezi. Nilizirudia rudia
sababu zangu za kuacha jeshi
tena kwa ujasiri mkubwa na
kumhakikishia mkuu wa chuo kwamba akinipa hayo
ninayoyataka niko tayari
kubaki jeshini. Hatimaye kauli ya mwisho ya
mkuu wa chuo ilikuwa ni hii:
“Jeshi ni wito. Tunaweza
kumlazimisha huyu kijana
kuwa mwanajeshi lakini
baadaye ikatuletea madhara makubwa sana.” Akamalizia
kwa kusema, “chukueni
maelezo yake kwa maandishi
kisha arudishe vifaa vya jeshi.” Wakati naondoka nilimsikia
ofisa mafunzo akitoa
maelekezo kwa walio chini
yake kwamba mwanafunzi
mwingine wa jeshi akija
kuripoti na kwenye daftari akajaza kwamba ni Msabato,
msimsajili kwanza mpaka aje
kwangu! Sijui kama Wasabato
wameendelea kupokewa
kwenye hicho chuo cha
magereza lakini ninachotaka askari wote wa majeshi yetu
yote na vikosi vyote, ni
kwamba askari unaweza
kusimama kwa miguu yako na
kufikiri kwa akili yako
mwenyewe! Ndugu zangu askari, nchi
imefika mahali ambapo
Waingereza hupenda kupaita
‘critical point’. Ni mahali
ambapo wananchi wako
tayari kwa mabadiliko na watawala wako tayari kwa
mapambano ili kubaki
madarakani. Katika point hii askari wetu
wanakuwa na nafasi kubwa
ya aidha kuwezesha
mabadiliko hayo kutokea kwa
wakati wanaoutaka
wananchi, tena kwa amani ama kuyachelewesha (si
kuyazuia) na kusababisha
yatokee baadaye kidogo
kuliko wananchi walivyotaka,
tena baada ya kumwaga damu
nyingi ya Watanzania wasio na hatia! Napenda kurudia kwamba
hakuna jeshi lolote duniani
hata kama tungekusanya
majeshi yote ya dunia hii na
kuyaleta Tanzania
hawataweza kuizuia nguvu ya umma pale inapokuwa
imeamua kufanya mabadiliko. Napenda tena kurudia
kwamba si lazima askari
mfanye kile ambacho
wakubwa wenu wanataka na
kuwaamuru kufanya.
Tunaweza kusimama imara na kutetea haki za Watanzania
tukiwamo na sisi askari.
Niliwahi kugoma kutii amri ya
kukamatwa na kuwekwa
rumande. Lakini pia mifano ni mingi na
nisingependa kuchukua
mifano kutoka nchi za Ulaya
kama Uingereza ambako
tulishuhudia wananchi
wakiandamana mitaani na askari wao hawakuwahi hata
kumpiga kofi tu
mwandamanaji hata mmoja. Walipohojiwa na vyombo vya
habari walisema dhahiri
kwamba waandamanaji ni
raia halali wenye haki ya
kufanya kile wanachokifanya
kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi yao. Katiba ya
Tanzania na sheria za nchi hii
zinatoa haki kama zile za
Uingereza. Tofauti ni
utekelezaji wa matakwa hayo
ya kikatiba na kisheria. Watawala wa Uingereza wako
tayari hata kung’oka
madarakani ili kutekeleza
matakwa ya nguvu ya umma. Lakini wale wa Tanzania
wako tayari kung’oa uhai wa
raia wengi ili mradi kuzuia
nguvu ya umma inayodai haki
na wananya hivyo kwa
sababu ya hofu ya kung’oka madarakani, jambo ambalo
hawataki kabisa kulisikia. Na
ndugu zangu askari napenda
kuwaambia kwamba yote
yanafanywa na watawala
wetu kwa kuwategemea nyinyi. Wanaminya haki zenu nyinyi
wenyewe, haki za wazazi
wenu, dada na ndugu zenu,
marafiki zenu, jamaa zenu na
majirani zenu. Chukulia mfano
rafiki zangu Mtaki na Edwin. Tumesoma wote shule ya
msingi pale Magu. Nilichaguliwa kujiunga na
Mazengo Sekondari, shule
kubwa na ya muda mrefu
ambayo sasa imegeuzwa
kuwa chuo kikuu bila
mabadiliko ya majengo. Shule iliyokuwa na maabara
nne kwa maana ya maabara
ya baiolojia, kemia, fizikia na
jiografia. Ilikuwa ni sekondari
ya ufundi na hakuna karakana
ambayo haikuwapo. Shule iliyokuwa na walimu wa
kutosha, vyumba vya kutosha
vya madarasa na vya kulala
mabwenini. Katika bweni la Ujamaa kwa
mfano, nilikokuwa naishi
mimi, kuna vyumba kadhaa
havikuwa na watu. Darasa la
Form IVA ambalo nilikuwamo
lilikuwa na wanafunzi 21 tu darasani. Na mazingira mengine mengi
ambayo sitaweza kuyataja
hapa ambayo yanafanya
wanafunzi wa leo wa Chuo
Kikuu cha Mt. John wajiulize
kama kweli ile ilikuwa ni shule ambayo haina maktaba
wala vitabu vya kutosha, na
mengineyo mengi
mnayoyafahmu. Nikafaulu kwa kiwango cha
daraja la juu lililoniwezesha
kuendelea mpaka chuo kikuu
na kupata kazi nzuri kwenye
Umoja wa Mataiifa. Rafiki zangu nakumbuka
mlivyoamua kujiunga na Jeshi
la Polisi si kwa sababu
mlipenda kazi hiyo ama
kwamba mlikuwa na wito wa
kuwa polisi kama mnavyodanganywa kwamba
jeshi ni wito. Nakumbuka mlijiunga huku
mkilalamika kwamba
mnalazimika kujiunga huko
kwa sababu kiwango chenu
cha ufaulu hakiwapi fursa ya
kazi bora zaidi ya hiyo. Lakini mimi nawafahamu vizuri.
Najua uwezo wenu wa
darasani. Mliathiriwa na
mazingira ya hovyo ya shule
mlizosoma. Rafiki zangu nyinyi wote leo ni
wakuu wa vituo vikuu vya
polisi vya wilaya katika wilaya
za Mbozi na Igunga. Leo hii mimi nimeacha kazi ya
Umoja wa Mataifa kwa ajili ya
kushiriki vema katika
mapambano ya kutafuta
ukombozi wa taifa hili. Wadogo zenu na wadogo
zangu mnawajua wako katika
juhudi za kutafuta maisha
lakini ni magumu. Wengine
walikosa kabisa nafasi ya
kujiunga hata na hiyo Magu Day. Wakaishia Bulima na Kinango,
ambako hali ilikuwa mbaya
zaidi. Wakafeli kabisa na leo
wanahangaika hapa na pale
lakini watawala
wanawawekea mazingira magumu mno ya kuendesha
maisha. Na sasa chukulia nao
wametambua hali yao duni
inasababishwa na watawala
walafi na walaghai.
Wamejaribu kutumia njia za
kidiplomasia kudai haki zao wanakutana na watu
wanaitwa wakuu wa wilaya
na mikoa. Wanaamua kuandamana,
mnashiriki kuamrisha askari
walio chini yenu kuwapiga na
kuwaweka rumande na
hatimaye kuwafungulia kesi
za kubumba! Askari wetu igeni mfano wa
askari wa Misri! Pale wananchi
walipoamua kuandamana
kukomesha utawala wa
kidhalimu wa miaka 30 chini
ya Hosni Mubarak, askari waliwalinda badala ya
kuwapiga. Walikataa kwa sababu hata
wao walikuwa wakiumizwa
na Mubarak lakini zaidi ya
hayo, waliokuwa
wakiandamana walikuwa ni
dada zao na ndugu zao na marafiki zao. Hivi sasa nchi iko njia panda.
Ugumu wa maisha
umeongezeka mara nne na
zaidi. Watawala hawalioni hilo
wala hawajishughulishi
kurekebisha hali ya mambo hususan hali ya uchumi. Wako busy na kujiandaa kwa
uchaguzi wa 2015. Mawaziri
wako busy na kampeni za
kuteuliwa kuwa wagombea
wa urais kupitia chama tawala
hapo 2015 na rais naye yuko busy kuandaa mtu wake
ambaye anadhani akimrithisha
jumba jeupe la pale Magogoni
atasema mwacheni Ndugu
Kikwete apumzike kwa
amani. Taifa limeamua kuandika
katiba mpya, rais na serikali
yake na chama chake
wameamua kuuteka
mchakato ingawa haikuwemo
kwenye ilani yao ya uchaguzi ili tu waturudishie katiba ya
mwaka 1977 na kuipa jina juu
ya jalada KATIBA YA JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
YA MWAKA 2014. Natambua juhudi
zinazoendelea hasa
zikiongozwa na CHADEMA
kujaribu kumkumbusha rais
kwamba katiba iko juu yake
na katiba ni mali ya wananchi na yeye anaajiriwa kwa katiba
hiyo na si yeye kujiandalia
katiba ili atawale kwa ulaini. Lakini juhudi za kidiplomasia
zikishindikana hapo ndipo
itabidi haki ya watu idaiwe
kwa maandamano na hapo
askari wote tuungane na
kuwa kama Misri, kwa kuwa Katiba mpya ni kwa masilahi
yenu pia! Jaribuni kutafakari!.
i definetely agree with the article Good Job Samson.
 
Safi Kubenea,ila ukisoma ile makala ktk Tanzania Daima ilistahili Polisi wote wa vyeo vya chini wajitokeze kumdhamini kwani makala ile iliwazindua kutoka ktk fikra mfu

Hivi hamuwezi weka hapa ili tujikumbushe tu.
 
Mimi ninavyoona kinachoendelea hapo kwenye story ya Mwigamba ni kuhusu maisha yake kwa ufupi na alichojifunza kuhusu dola ya CCM na anatoa fundisho kwa wengine.

Kwa mfano alichokifanya huko chuo cha magereza hakuna tofauti na kile tulichokifanya wengi wetu tuliopiti jeshini enzi hizo (JKT). Ndiyo maana huwa nasemaga kuwa hiki kizazi cha JKT ndiyo Tatizo kubwa kwa mabadiliko Bongo!!!
 
Jeshi la polisi linamshikilia mhariri wa gazeti la Tanzania Daima, A. Kibanda kwa tuhuma za uchochezi. Kibanda anashikiliwa kwenye makao makuu ya polisi jijini Dar es Salaam.

===============

UPDATES

Habari zilizonaswa sasa hivi kutoka makao makuu ya polisi Dar zinasema Mhariri wa Tz Daima Absalom Kibanda ameachiwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa na polisi kwa zaidi ya masaa matatu kwa tuhuma za uchochezi. Amedhaminiwa na Mhariri wa Mwanahalisi Saed Kubenea kwa dhamana ya Sh 5,000,000/-. Kibanda anatakiwa kuripoti polisi hqtrs Jumatatu asubuhi.

kachochea kitu gani?
 
Mkuu Mnyika,

Wewe ndiye uliyesign yale makubaliano kati ya Serikali na CDM. Kwa kuwa inasemekana kuwa serikali imekwenda kinyume na makubaliano yenu, je unaweza kutupa dondoo za hayo makubaliano??

Binafsi mpaka sasa sielewi kwa nini mlikubali kusign!!

Mr. Zero,

Nilichosaini ni "Taarifa kwa Vyombo vya Habari" ambayo ilitoa kwa umma masuala mawili ambayo tulikubaliana. Hatukukubaliana Rais asaini ile sheria, kwa kuwa suala la kusaini au kutokusaini ni kwa kadiri mamlaka yake ya katiba ibara ya 97 na ibara ya 37 inatamka bayana kwamba Rais halazimiki kufuata ushauri wa mtu yoyote.

Na sababu moja wapo ya kumueleza Rais asisaini kati ya nyingi ambazo zilielezwa kwa kina kwenye waraka kwa Rais ni hilo la kuwepo kwa kifungu cha kifungo cha hadi miaka saba au faini ya hadi milioni 15 au vyote kwa kukusanya maoni au kutoa elimu kuhusu mabadiliko ya katiba kwa kile kilichoelezwa kuwa kinyume na sheria husika.

Baadhi ya masuala ambayo umeyauliza tayari nilishayatolea majibu kwenye mkutano na wanahabari baada ya Rais kusaini sheria husika unaweza ukaingia www.chadema.tv utapata sehemu ya majibu.



JJ
 
Kwa kufuata taaluma na maadili ya uandishi katika vyombo vya habari mhariri ametoka nje ya uringo wake kwa kuruhusu makala au barua kama hii ichapishwe kwenye gazeti lake. Mhariri ana mamlaka ya kukubali au kukataa makala au habari ambayo kwa haki alizo nazo pamoja na busara yake kulinda chombo chake cha habari.

Mhariri alikuwa na haki ya kuihariri kama kuna kitu ambacho kinaonyesha kuhamasihsa kinyume cha sheria. Na kama mleta mada alikataa angeweza kuiweka kapuini, ila kwa uamuzi wake wa kuichapa alijua nini kitatokea na ndicho kilichotokea.

Kwa habari hii kama ilivyotokea kwenye gazeti lake vigumu kumtetea, kwani siku zote kutanguliza busara ni kinga kwa kazi na wajibu.
 
Kwa kufuata taaluma na maadili ya uandishi katika vyombo vya habari mhariri ametoka nje ya uringo wake kwa kuruhusu makala au barua kama hii ichapishwe kwenye gazeti lake. Mhariri ana mamlaka ya kukubali au kukataa makala au habari ambayo kwa haki alizo nazo pamoja na busara yake kulinda chombo chake cha habari.

Mhariri alikuwa na haki ya kuihariri kama kuna kitu ambacho kinaonyesha kuhamasihsa kinyume cha sheria. Na kama mleta mada alikataa angeweza kuiweka kapuini, ila kwa uamuzi wake wa kuichapa alijua nini kitatokea na ndicho kilichotokea.

Kwa habari hii kama ilivyotokea kwenye gazeti lake vigumu kumtetea, kwani siku zote kutanguliza busara ni kinga kwa kazi na wajibu.

Mkuu sijaona tatizo lolote katika makala/barua aliyoruhusu mhariri kutolewa katika gazeti. real sijaona, zaidi naona wazi uoga wa wakubwa wa polisi tu. Askari wadogo wananyimwa hata haki zao za msingi mfano mafao wanapohamishwa,lkn hawatakiwi kuhoji cause of dhana ya kutii mamlaka ya wakubwa,but kimsingi wananyanyasika
 
“your blood,yet more my blood shall irrigate victory“
 
Back
Top Bottom