Dah, we acha tu mkuu!!!!Mbona tulishafika kaka genekai
Walioshuhudia tukio wanaeleza kuwa waliompiga hawajachukua kitu chochote, so tusidanganyane , huu ni mpango maalum
......
Tusiwe wepesi wa kuchora mstali na kuhitimisha kwenye jambo linalohitaji fikra pevu na uchunguzi mpana.
Cha kufanya ni kumtakia heri huku uchunguzi ukiendelea.
.......
Wakati naweka comment yangu ya awali hiyo taarifa ilikuwa haijakamilika kama ilivyo sasa. Nadhani mleta maada ameiboresha baadaye, na tayari nimeshaisoma kwenye sources nyingine na kutambua kwamba hakuna walichochukua.
Na kilichonitisha zaidi ni eti wamemvamia getini wakati anaingia nyumbani kwake. Nashangaa sana, walitaka nini? Kumuua? Au kuna document walizifuata?
Tanzania si nchi salama kabisa ya kuishi hivi sasa. Maana dola inatumika kwa ajili ya kupambana na wanaoikosoa serikali badala ya kutumika kulinda maslahi ya nchi.
Kama hawajachukua chochote, pamoja ya kwamba walimchukua yeye binafsi na kwenda kumtelekeza kusikojulikana, ni dhahiri walinuwia kumuua.
Tayari waziri wa afya ndugu Hussein Mwinyi amekwenda hospitali kumjulia hali. Na hiyo ndiyo tabia yao. Tuna wakati mgumu sana hivi sasa.
.......
Kwa hali ya kisiasa ya nchi yetu, na ukinzani uliokuwepo baina ya serikali na Wanahabari, sidhani hapa kuna sababu nyingine zaidi ya hiyo. Absalom Kibanda, amekuwa msumari mkali kwa serikali, tangu alipokuwa Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima na sasa New Habari Coorporation.
Ikumbukwe kuwa, hadi sasa ana kesi iliyoko mahakamani, kesi ya uchochezi kwa sababu ya makala iliyoandikwa na kamanda Samson Mwigamba na kuchapwa katika gazeti la Tanzania Daima wakati Bwana Kibanda akiwa bado Mhariri wa Tanzania Daima.
Ngoja tuwasikie watakavyokuja na majibu ya upelelezi wao. Ila Tanzania kwa sasa, si mahali salama sana kwa wanahabari wanaojali uzalendo na weledi wa kazi zao
Siku 2 kabla redio Imani Haijafungiwa kat ya saa 2 mpk 3 asubuh walikuwa na kipindi chao wakijadili zile tetesi za uwapo wa chuo kiislamu ktk kisiwa cha Ukerewe jjn Mwanza kinachofundisha mambo ya Ughaidi ambazo zilikuwa zimetolewa na gazeti la MTANZANIA.
ktk majidiliano yao na simu za wasilizaji walimtangaza Husein Bashe na Absolom Kibanda kama maadui wa uislamu na wanataakiwa kushughulikiwa kutokana Bashe kuruhsu habari hiyo ambayo Kibanda ndo alikuwa Mwandishi wake.
Upelelezi utabidi uanzie kwako wewe mwenyewe na huyo mwenzio,yaelekea mnamfahamu hata muhusika au yaweza kuwa ni nyinyi wenyewe.
Naamini Polisi wanatakiwa watumie utaalam wao wote pasi kufuata mis-leading info kama hii yako wewe, inaumiza sana kitu Absalom Norman Kibanda katendewa, hakika inaumiza...
kuendelea kusema Tanzania nikisiwa cha amani ni uongo mbele ya Mwenyezi Mungu na kuwahadaa raia.Ingekuwa Somalia ningesema kutokana na kutokuwa na serekali muda mrefu ila hapa si hivyo matukio ni mengi na tume ni nyizi zimeundwa hatujui matokeo yake
Zinzishia tuu kutangazwa
Poa kamanda, nshakupata. Mimi nilishasema kwenye kipachiko changu cha awali na makala yangu ndefu niliyoiweka hivi punde, "Tanzania si mahali salama kwa Wanahabari wajuao kutenda kazi kwa weledi. Tanzania si salama kwa kwa Wanaharakati"
Unajua hizi game mara nyingine huchezwa hivi:-
Kibanda kama mwandishi wa habari aliwahi kuandika makala au taarifa ambazo hazikuwapendeza watawala na serikali kwa ujumla. Akavutwa kwenye mtego na maadui zake kwa ahadi za kupewa mwezi kwenye sahani.....naye akanasa.
Sasa wale wabaya wake walipomtenda wanajua lawama (focus) haitawagusa wao waliotenda kwani wako kimzuka zaidi (ghost). Ila wao kwa upande mmoja malengo yao wameyatimiza ya aidha kulipa kisasi au kumnyamazisha. Ndio maana utakuta watu kama Pasco wa JF anaweza kuwa sehemu ya spinning machine (kwa kuusoma uzi wake katikati ya mistari); kwani, sadly, wanadamu hawana wema!
Atongwele, Atongwele, Atongwele...! I wish you could just get back into your shell and stay there, uchunguzi my foot! Kweli JF imekuwa kokoro!si vyema kukurupuka kipindi hiki wakati mwenzetu yu mahututi. cha msingi kwa sasa tumuombee ili apone na ukweli wa tukio lenyewe ufahamike. ila cha msingi jeshi uchunguzi wa kina zaidi ufanywe na wananchi tutoe ushirikiano kwa jeshi letu ili wahusika wabainishwe