Tulishawazoea hawa, sasa mtu atakuwa akivamiwa na mateja huko alkiwa amelewa na atakuja humu ataanza propaganda zake mara hoo, Wamening'oa meno, kucha kumbe matake wamemfanya kitu mbaya.
Hivi line mateja wakaitana "afande?"
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tulishawazoea hawa, sasa mtu atakuwa akivamiwa na mateja huko alkiwa amelewa na atakuja humu ataanza propaganda zake mara hoo, Wamening'oa meno, kucha kumbe matake wamemfanya kitu mbaya.
CDM inatumiwa kama kibwagizo cha wimbo lakini maudhui ya wimbo yako kwingine. Watu wanauhakika wa usalama wao wanatenda uhalifu ndani ya nchi jinsi watakavyo na hakuna anayewauliza zaidi ya kuambiwa na mamlaka husika kuwa huo sio uhalifuMazingira mkuu yanafanya CDM wahusishwe moja kwa moja.
Ukweli hauwezi kulazimishwa mkuu, punguza munkari na utoe hoja umshinde mwenzako badala ya kung'aka. Serikali haiwezi kuhusika eti kwa saababu haijawakamata wahusika, ingekuwa hivyo basi Marekani wanaosaka magaidi huku na kule basi tuwaite ni magaidi kwa vile mpaka leo hawajawakamata baadhi ya magaidi. Ujue kama hicho ni kikundi cha MAFIA kimejiandaa kutekeleza mauaji , basi hata kazi ya kuwabaini inahitaji umakini sana, Mimi naamini Serikali imejipanga vizuri na lazima washukiwa watakamatwa tu. Hizi zingine kelele za kisiasa, hata hivyo hakuna jambo la kushangaza kwa serikali kulaumiwa hasa ukizingatia kuwa majukwaa yanyotumika kufikisha ujumbe wa kupotosha dhidi ya serikali ni majukwaa aidha yanamilikiwa na vyama vya siasa au wansiasa wenyewe.
Hivi line mateja wakaitana "afande?"
![]()
Wateswe au wauawe wangapi ndipo tustuke?
Na Ndimara Tegambwage
MWANDISHI wa habari Absalom Kibanda, amevamiwa. Akapigwa. Akachokonolewa jicho. Akachomolewa kucha. Akakatwa kidole. Akang'olewa meno. Akaachwa kufa nje ya lango la nyumba yake iliyoko mtaa wa Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam.
Ni usiku wa kuamkia jana, Jumatano. Hivi sasa Kibanda, mhariri mkuu mtendaji wa New Habari Media Group – kampuni inayochapisha magazeti ya Mtanzania, Rai na The African, yuko taabani kitandani.
Aliyofanyiwa Kibanda ni yaleyale aliyofanyiwa Dk. Steven Ulimboka, kiongozi wa madaktari katika mgomo mkuu wa mwaka jana wa kushinikiza serikali kuweka mazingira bora ya kazi katika hospitali zake kwa kununua vifaa, dawa na kutoa mishahara inayostahili.
Dk. Ulimboka aliburutwa kwenye lami. Akakunjwakunjwa kama godoro na kuingizwa kwenye gari dogo. Akapigwa mara kwa mara kwa fimbo, makofi na mateke. Akang'olewa meno na kucha; akatupwa kwenye msitu wa Mabwepande, kilometa 45 nje ya jiji la Dar es Salaam. Aliponea chupuchupu.
Kwahiyo, mbinu zilizotumika kumtesa Kibanda siyo mpya. Zimewahi kutumiwa. Unaweza kusema haraka kuwa waliomtesa mwandishi, ama wamesomea chuo kimoja au ni walewale waliomtesa Dk. Ulimboka.
Je, baada ya Kibanda, nani? Lakini kabla ya Kibanda, nani? Mwaka 2008, watu watatu wakiwa na panga, chupa yenye tindikali na gongo la mti, walivamia chumba cha habari cha gazeti la MwanaHALISI tulimokuwa tumebaki wawili.
Walifanikiwa kummwagia tindikali machoni, mwandishi na mkurugenzi mtendaji wa kampuni inayochapisha gazeti hilo, Saed Kubenea. Hakupofuka kabisa lakini lazima aende India kila baada ya miezi minne kuchunguzwa macho.
Nakumbuka kunyukana na vijana wawili – mmoja mwenye panga na mwingine mwenye gongo – hadi panga lililolenga katikati ya kichwa lilipokoseshwa shabaha, kutua kwenye kisogo kulia na kudondokea nyuma yangu. Nilishonwa nyuzi 15. Nani alikuwa amewatuma?
Desemba 2009, mwandishi Frederick Katulanda wa Mwanza, alivamiwa nyumbani. Wavamizi walikuwa wakipaza sauti na kudai kuwa ana nyaraka za akaunti za benki za halmashauri ya jiji la Mwanza.
Walikuwa na mapanga. Walikuwa wakichagizana kwa kusema, "Kata kichwa! Kata kichwa!" Waliondoka na mafaili. Walimwachia kilema mguuni na makovu mikononi.
Mwaka 2006, waliojiita wananchi wakazi wa jiji la Mwanza, walikusanywa na kufanya maandamano makubwa kwa walichoita "kupinga mwandishi Richard Mgamba kuandika uongo" na kudai kwamba alikuwa Mkenya na "siyo raia wa Tanzania."
Hii ilikuwa baada ya filamu iitwayo "Darwin's Nightmare" kuonyesha jinsi wananchi wakazi wa jiji wanavyokula mapanki badala ya samaki.
Mgamba alidaiwa kuwabeba watengeneza filamu na kuwaonyesha maeneo ambako kweli kunguru na binadamu walikuwa wanagombea mabaki (mifupa) ya samaki baada ya viwanda kunyofoa minofu ya kuuza Ulaya. Mgamba alilazimika kuwa "mkimbizi" jijini Dar es Salaam.
Sept 2010 wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu, katika eneo la Nyambiti, jimbo la Sumve wilayani Kwimba, mkoani Mwanza, mwandishi Frederick Katulanda alivamiwa na kupigwa na watu wapatao 15 waliojiita "Green Guard" – wa "chama cha kijani."
Katika "kumshughulikia," Katulanda anasema, walikuwa wakionyesha kuwa na ujuzi mkubwa wa judo na karate huku wakidai kuwa anawaandika "vibaya" Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mwaka 2011 mwandishi Richard Massatu alikutwa amekufa katika eneo la Igoma, jijini Mwanza. Vyombo vya habari viliripoti kuwa macho yake yalikuwa yametobolewa na kuwekwa gundi aina ya super glue; mguu wa kushoto na mbavu vilikuwa vimevunjika.
Vyombo vya habari viliripoti kuwa Massatu aliyekuwa mmiliki na mhariri mkuu wa gazeti la Kasi Mpya (sauti ya umma), alionekana mara ya mwisho usiku wa kifo chake akiwa na maofisa wa polisi na usalama katika baa iitwayo Cross Park katika eneo la Igoma.
Daudi Mwangosi, mwandishi wa kituo cha televisheni cha Channel Ten aliuawa kwa kupigwa risasi katikati na mikononi mwa polisi na hasa mbele ya mkuu wa polisi wa mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda.
Hii ilikuwa tarehe 2 Septemba mwaka jana. Kesi bado iko mahakamani. Picha zinazoonyesha Mwangosi alivyolipuliwa, zinatia simanzi kwa kila anayethamini utu.
Mwaka huu, tarehe 3 Januari, maiti ya mwandishi Issa Ngumba iliokotwa katika pori la mlima Kajuruheta, kijiji cha Mhange, wilayani Kakonko katika mkoa wa Kigoma.
Ngumba alikuwa mwandishi wa habari wa Redio Kwizela. Alikutwa amekufa baada ya kutoweka nyumbani kwa siku tatu.
Mwandishi wa habari Erick Kabendera anayeishi Dar es Salaam, anaishi kwa wasiwasi. Wazazi wake waishio Bukoba, wamehojiwa na "ofisa usalama" kwa kile kilichoitwa "uhalali wa uraia wao."
Kabendera, ambaye ncha ya kalamu yake haipindwi kwa woga wala upendeleo, amekuwa akiripoti kupigiwa simu na kutishiwa kwamba "atarudishwa kwao." Naye hajui kwao kwingine isipokuwa Tanzania.
Juzi, Jumanne, mwandishi Charles Misango wa TanzaniaDaima, alishindwa kurudi nyumbani kwake, Kimara nje kidogo ya Dar es Salaam.
Kwa siku nzima familia yake ilishinda ikiripoti watu tofauti waliokuwa wakifika nyumbani kwake wakimuulizia na wengine kuzengea nyumba tu.
"Nilipomwambia mhariri wangu juu ya hali hiyo, aliniambia ‘usiwe mjinga; nenda ukalale hotelini.' Nilikwenda kwa rafiki yangu mwenye ua mkubwa, nikaegesha gari na kulala katika gari langu kwa kuwa alikuwa na wageni wengi," anasimulia Misango.
Misango ni mmoja wa wahariri wanaokabiliwa na tuhuma za "kuandika uongo." Kesi yao iko mahakamani jijini Dar es Salaam.
Kuna orodha ndefu ya waandishi wa habari waliotishwa na wanaoendelea kutishwa; waliopigwa na polisi na askari magereza (Ukonga, Dar es Salaama) kwa tuhuma mbalimbali; waliotishiwa maisha kwa simu na hata kwa kufuatiliwa na watu wasiowafahamu.
Miezi mitatu iliyopita, ilivumishwa kuwa Ansbert Ngurumo, mhariri mtendaji wa sasa wa TanzaniaDaima amefariki. Taarifa hii ilipelekwa pia kwenye mtandao mpana na unaoheshimika wa Jamii Forum (JF).
Hakuna ajuaye kama hakukuwa na nia ya kuua au kudhuru Ngurumo. Livumalo lipo na Ngurumo alipewa ushauri wa "kuwa makini" kwani kila uvumi una shina lake.
Ngurumo amekuwa muwazi siku zote kuelezea jinsi baadhi ya walioko madarakani walivyoshindwa kumshawishi kuwapenda, kuwanyenyekea na hata kufanyakazi nao.
Tatizo lililopo ni kwamba kila janga lilipotokea, baadhi ya waandishi walijitenga na kusema, "Shauri yao, nao wamezidi." Nani amezidi wapi? Kumekuwa na tabia ya kujitenga na kubaguana.
Huko tuendako, baada ya kujikata kutoka shina kuu la wanataaluma, tunakuwa kama vifaranga vya kuku visivyo na ulinzi wa mbawa wala kelele za mama. Tunajianika mmojammoja kwa mwewe kututafuna mmoja baada ya mwingine. Tutaisha!
Nani atalinda maisha ya waandishi wa habari Tanzania? Tayari mmoja yuko kariku kufa kwa woga. Aliwaambia wenzake jana kwenye viwanja vya hospitali ya Muhimbili (MOI), "Labda tutafute makazi nje hadi mwisho wa utawala wa awamu hii nne…"
Huu ni woga, labda ni upumbavu pia. Kwamba kumekuwa na taarifa za madai ya kuua waandishi wawili maarufu wa habari na wanasiasa wawili mashuhuri; siyo sababu ya kukimbia nchi.
Kuwa na umoja katika taaluma, kuandika zaidi na hasa kuandika ukweli; kuchunguza, chambua na kufafanua zaidi – kuweka jamii wazi juu ya kinachoendelea – hivi vinaweza kuwa ngao kuu kwetu sasa na huko tuendako.
Bali tujenge mashaka juu ya mfanano wa mbinu za kutesa na kuua. Watesaji na wauaji waweza kuwa watu walewale. Wako wapi? Tuwasake na kuwaanika. Tunaweza katika umoja wetu.
Mwisho
Na Igunda wa Ikulu je aliyemtesa Ulimboka ameshakamatwa? Wanaozuga ni akina Kova eti wamemkamata Mkenya aliyemtesa Ulimboka wakati huo huo hawataki kumpeleka Mkenya huyo mbele ya Ulimboka amtambueKumbe wewe huji movie zinavyoandaliwa? pole sana. Kwani wale wanao act POLISI, MADAKTARI n. k kwenye movie huwa ni POLISI kweli. Inawezekana kabisa hao waliotekeleza tukio hilo walijipanga kujiita maafande utajuaje? hata mleta mada mwenyewe amewasilisha mada yake ki-movie movie eti KIBANDA alisema aliskia huyu mleta mada yeye walikutana na wapi na KIBANDA na kumwambia hivyo? Tuoneshwe basi hata media iliyomhoji baada ya tukio akayatamka yaho maneno. Acheni kutuzuga humu JF. hatuko humu kupiga umbea
Peleka taarifa kwa Said Mwema na Kova wafanye mpango wa haraka wa kuwakamata.
Mwambie aje huyo Kiranga wako halafu njoo na wewe na wanao wanaosoma St. Mary's na yule demu wako anayefagia ofisi za British Council.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri Mtendaji wa New Habari, Abdalom Kibanda, amekimbizwa Muhimbili baada ya kuvamiwa na kisha kujeruhiwa na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi.
Watu hao walimvamia na kumtoa katika gari kisha wakampiga kabla ya kumtupa na kumtelekeza umbali mdogo na nyumbani kwake.
Aliokotwa na majirani na kukimbizwa hospitalini Muhimbili kwa matibabu ya haraka.
Pamoja na kuumizwa hivyo, hakuna kitu hata kimoja kilichoporwa katika gari lake
![]()
Taarifa zaidi baadae...![]()
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri Mtendaji wa New Habari, Abdalom Kibanda, amekimbizwa Muhimbili baada ya kuvamiwa na kisha kujeruhiwa na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi.
Watu hao walimvamia na kumtoa katika gari kisha wakampiga kabla ya kumtupa na kumtelekeza umbali mdogo na nyumbani kwake.
Aliokotwa na majirani na kukimbizwa hospitalini Muhimbili kwa matibabu ya haraka.
Pamoja na kuumizwa hivyo, hakuna kitu hata kimoja kilichoporwa katika gari lake
![]()
Taarifa zaidi baadae...![]()
Mkuu Jicho la 3 nahisi hii utakuwa umeandika ukiwalenga watu fulani wakusifie! ila elewa kwamba hujafa hujaumbika.Huyu mwandishi si naye alimwagiwa Tindikali na wabaya wake, wala hawezi kuandika lolote zaidi ya kua na hisia kama hizo. Mimi nadhani tufike mahala tujitathmini huko tunakoishi, mahali pa kazi na hata katika maeneo ya mahusiano ya kijamii kuona kama tunao maadui wanaotunguka na kuchukua tahadhari badala ya kuendelea kupotoshana kuwa watu fulalani au serikali ndiyo inayohusika bila kuwa ushahidi wa kutosha. Kuihusisha serikali yetu na matukio kwa kigezo kuwa haijawakamata washkiwa ni udhaifu wa kufikiri na upeo mdogo wa kuchambua mambo.
Ulitaka asemeje afe haraka? watu wengine bwana.
KUna misemo mingi tuu hapa wengine huku wanasema ni mtandao wa Membe,Kinana na Kikwete wanasema wanataka kuwazimisha sauti wale wanaoibua maovu yao kwa hiyo mazingira ni mengi tu na ukiangalia CCM na viongozi wake walivyopandikiza watu kwenye jamvi hili kutengeneza stori unaweza ukasema mazingira hayo hao watu watajwa wanaweza kuhusika moja kwa moja Mungu mpe ujasiri KIbanda apiganie uhai wake ,na kama yasemwayo mjini kwamba watawala ndio wameplot basi Mungu awalaaniKumbe wewe huji movie zinavyoandaliwa? pole sana. Kwani wale wanao act POLISI, MADAKTARI n. k kwenye movie huwa ni POLISI kweli. Inawezekana kabisa hao waliotekeleza tukio hilo walijipanga kujiita maafande utajuaje? hata mleta mada mwenyewe amewasilisha mada yake ki-movie movie eti KIBANDA alisema aliskia huyu mleta mada yeye walikutana na wapi na KIBANDA na kumwambia hivyo? Tuoneshwe basi hata media iliyomhoji baada ya tukio akayatamka yaho maneno. Acheni kutuzuga humu JF. hatuko humu kupiga umbea
Tulishawazoea hawa, sasa mtu atakuwa akivamiwa na mateja huko alkiwa amelewa na atakuja humu ataanza propaganda zake mara hoo, Wamening'oa meno, kucha kumbe matake wamemfanya kitu mbaya.
Mmmmmmh. Pole yake twamuombea apone.