Absalom Kibanda (Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri) avamiwa na watu wasiojulikana na kujeruhiwa

Absalom Kibanda (Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri) avamiwa na watu wasiojulikana na kujeruhiwa

Pona haraka kamanda uje uwe shahihi namba moja kuwatambua waliotaka kukumaliza. Naoma usitukimbie kama Ulimboka. Ila gazeti la Mwanahalisi lingekuwepo lingetupa ukweli wa jambo hili!!! We miss you mwanahalisi.
 
Jaman huyu ndiye aliyesema kuwa anamuogopa Kinana kama ukoma?
 
Polisi waanze uchunguzi na gazeti la tanzania daima na chadema. kwani hatuelewi ni kwanini alikimbia huko alipokuwa mhariri wa hilo gazeti la mwenyekiti wa chama.
Unapotezea eeh? Naategemea Waandishi wa habari mjikite zaidi katika habari za uchambuzi wa kina kuliko kuripoti matukio jambo analoweza kufanya mtu yeyote mradi anajua kuandika kiswahili... Kwa nini tunajidanganya eti Tanzania ni nchi ya amani, ni kisiwa cha amani, ni nchi salama, na hii yote ni kazi ya chama tawala!!!!

  • Tanzania tunaongoza kuua ndugu zetu wa ulemavu wa ngozi na hakuna hatua za makusudi kukomesha hili... harafu tunajidai kisima cha amani!!
  • Tunauana kwa sababu ya tofauti za imani, unamchukia mwezako kwa kula chakula usichokula!!! Tanzania nchi ya amani...
  • Mwangosi anuawa kama kibaka.... kisiwa cha amani
  • Ulimboka anapona kwa miujiza ya Mungu na madaktari... kelele nyingi toka kwa wanahabari na wanaharakati... sasa imesahaulika... nchi ya amani!!!
  • watoto wetu vyuo vikuu wanalazimika kujiuza na kuishia kupata ukimwi kisa bodi kuchelewa kuwapa hela... tanzania nchi ya amani.
  • huduma za jamii duni kupita kiasi... tanzania nchi ya amani....
Hakuna cha uchunguzi hapa... mhusika anajulikana (UDHAIFU WA SERIKALI NA VYOMBO VYAKE KUMLINDA MTANZANIA)...
anayetaka uchunguzi amemiss maigizo ya kamanda Kova...
 
Hii ni habari ya kusikitisha sana,sijui Tanzania tunaelekea wapi, ni majambazi gani wanaotoboa macho bila kupora mali yoyote?

Nadhani iliswala linahusiano na kazi yake. Hii Tanzania sasa inaelekea kua simahala salama kwa Baadhi ya watu kuishi.

Tusubirie ngonjera za jeshi la polisi kama kawaida yao.
 
Nchemba atakuwa na cd ya hili tukio likipangwa na viongozi wa chadema
 
h
Hao watu watafutwe .kwani wamechoka amani.m
Mwenye picha atuletee.Ee mungu mpe ahueni kiumbe chako
 
Hali hii si ya kufurahisha kabisa tumuombee kila la kheri mpiganaji kibanda apone haraka, lakini pia tusianze kupigia mistari majibu ambayo hatuna uhakika nayo, hayatamsaidia tutafute taarifa za uhakika ili tujulishane wadau.
 
Mara zote na wakati wote WASEMA KWELI WANA MAISHA MAGUMU AU HAWANA MAISHA KABISA HAPA DUNIANI.Mifano ni mingi sana ya watenda haki na wasema ukweli hapa duniani wanavyoteseka na kufa vifo vya ajabu.

Kibanda Mungu akuponye haraka.
 
Hatuna imani na serekal yetu hasa kwa matukio kama haya. Ya ulimboka sijui yameishia wapi.bado hili limeibuka tena,sijui kikwete unaitakia nini tanzania. Tunahitaji gazet letu mwana halisi lirudi kazini ili kufichua maovu yenu nyie vibaraka wa mabepari. Shyt
 
Natamani Jeshi letu la polisi lingekuwa na uwezo wa kuchunguza masuala kama haya. Pia natamani angekuwa mtu mkubwa serikalini kwani tungekodi FBI. Poor bro Kibanda. Wish you a quick recovery
 
du!! hii nchi huwezi kusema jambo,tunafuga majasusi na tunawalea ndio maana maovu yote yanaendelea.............tukiwa na serikali huru tunaweza kusonga mbele kama kenya.....kenya wako mbali sana kwa sababu ya democracy yao ya viombo vya habari
 
Mh? Mh? Mh? How many times have i said Mh? Three times! ".....watu wanaosadikiwa kuwa majambazi"....
..."Hakuna kilichoporwa kwenye gari lake"...Sasa ni majambazi wa kudhuru mwili tu na kuondoka? Au ndo style ya majambazi waliokuja nayo mwaka huu wa 2013?
 
Ulimboka alivyotekwa tuliambiwa CCM sasa Absalom Kibanda tutaambiwa nani.
 
Polisi waanze uchunguzi na gazeti la tanzania daima na chadema. kwani hatuelewi ni kwanini alikimbia huko alipokuwa mhariri wa hilo gazeti la mwenyekiti wa chama.

......

Good2015, Nikiita hii ni akili ya Masaburini nitakuwa sijakutendea haki. Hii itakuwa akili ya matakoni.
 
Polisi waanze uchunguzi na gazeti la tanzania daima na chadema. kwani hatuelewi ni kwanini alikimbia huko alipokuwa mhariri wa hilo gazeti la mwenyekiti wa chama.

.......

Hufai hata kuchunguza kesi ya mwanafunzi kuibiwa penseli, yule alikuwa against serikali wale (serikali)wakamsogeza kujifanya ni marafiki akajua amepata rafiki wa kweli kimaslahi kumbe urafiki wa sasa haubadilishi mabaya uliyoyafanya huko nyuma.
 
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri Mtendaji wa New Habari, Abdalom Kibanda, amekimbizwa Muhimbili baada ya kuvamiwa na kisha kujeruhiwa na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi.

Watu hao walimvamia na kumtoa katika gari kisha wakampiga kabla ya kumtupa na kumtelekeza umbali mdogo na nyumbani kwake.

Aliokotwa na majirani na kukimbizwa hospitalini Muhimbili kwa matibabu ya haraka.

Pamoja na kuumizwa hivyo, hakuna kitu hata kimoja kilichoporwa katika gari lake

attachment.php


Taarifa zaidi baadae...

.......

Unganisha na habari hizi hapa na hali hewa ilivyo sasa,yeye ni Mhariri Mkuu nafikiri unaweza kupata mwanga wa kitu kinachoendelea hapa tanzania Usalama wa Taifa,Jeshi la Polisi na hao FBI ujasusi ni kuunganisha taarifa mbalimbali kama hizi na majibu mtayapata tu.

1. Hofu ya Al Qaeda Ukerewe
2.Njia fupi kutoka Mwanza kuelekea Aljazeera Ukerewe-3

Nafikiri nitakuwa nimeeleweka.
Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom