Absalom Kibanda (Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri) avamiwa na watu wasiojulikana na kujeruhiwa

Absalom Kibanda (Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri) avamiwa na watu wasiojulikana na kujeruhiwa

endeleeni kuruka sarakasi na taulo mbele ya wageni.hata ulimboka mlianza kurusha maneno kwa cdm.mwisho wa ubaya aibu.

Hivi CCM kila kosa CDM si wakifute sasa propagaganda nyingine bwana hata mnashangaa so siku hizi lumumba ndio wasemaji wa usalama wa taifa....mimi kuzaliwa tanzania....huu ushetani mwingine ....
 
Samahani kuuliza, huyu jamaa alikuwa kibaraka wa CCM ama CDM?
 
hapa jukwaani hata mtu akisema binadam ana miguu saba atapata wajinga wanaomuunga mkono.

Kama nimekuelewa vizuri unamaanisha wewe kuunga mkono utekaji wa kibanda kuwa ni ujinga kufanya unyama huo ila huna jinsi kwa kuwa unanufaika na ushetani huo .....sasa unaona uunge mkono ujinga huo kama ulivyesema kuwa wapo(wewe na wengine isipokuwa sisi tunaopinga) wajinga watakaounga mkono....sasa ndugu yangu gamba kwanini uunge mkono ushetani....kweli tunakosa walimu wa saikologia .....UMELAANIWA SHETANI
 
Kwa jinsi tukio lenyewe lilivyo itakuwa ngumu sana kunishawishi kuwa watekaji wa ulimboka hawajahusika, kwanza taarifa zilizopo ni kuwa jicho lake la kushoto kimeharibika sana kwa kiwango cha kutoweza pona si hapa bongo tu ila hata huko majuu.... Lets wait and see
 
Mtiririko wa matukio kabla ya kutekwa na kupigwa vibaya kwa Absalom Kibanda mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri unatia shaka sana! Kwa msiokumbuka, alianza kwa kuandika makala za kuwatahadharisha vyama vya upinzani hasa wanaounda kambi rasmi ya upinzani bungeni juu ya ujio wa Abdrahaman Kinana Katibu Mkuu wa CCM,tena akayawakilisha mawazo yake hayo kupotia gazeti lao la TanzaniaDaima!
Ikaleta maneno sana na vitisho kutoka kwa wenye chama na gazeti! Akaandika makala ya mwisho "namuogopa kinana"nayo wamiliki wa gazeti wakaja juu sana...

Akaamua kuhama gazeti na kujiunga na magazeti ya Habari Coperation,leo sio vitisho tena bali wamemng'oa jicho na majeraha kibao!

Nyie mmemfanya nini Kibanda wetu?
 
hana chama .....mwenye kujua atuwekee kadi namba na chama chake

Kwa mtanzania kutokuwa na chama si rahisi. Kama ni kibaraka wa CCM basi CDM wamfanyia, na kama ni kibaraka wa CDM basi CCM wamemfanyia.
 
Tanzania kama Ndege angani ipo kwenye anga ambalo rubani ameiweka kwenye AUTO PILOT position inajiendesha yenyewe na rubani ameenda kulala. Napata picha huu ni mwanzo tu tutashuhudia mengi kuelekea uchaguzi 2015 na hii iwe chachu kwa watanzania kutathimini huu utawala na kuacha mazoea tuliyonayo ya kuendelea kubeba huu utawala na kuhakikisha haturudii makosa tena 2015.
Ukweli ni kwamba hatuna chombo cha kuchunguza utendaji wa Jeshi la Polisi na vyombo vya usalama nahisi vimegeuka baada ya kusimamia usalama wa raia na mali zao sasa vinateka, vinatesa, vinaiba na hata kuassassin raia wanaotakiwa kuwalinda. Sasa polisi kila siku wanaua na kufanya vitendo vya kinyama.
Watanzania tuamke hatuko salama kama tunavyofiki.
God bless Tanzania, Africa.
 
Tanzania inaenda kombo. Masikini Kibanda ni nani aliyemfanyia haya? Nadhani sasa kwa kiwa FBI wapo nchini basi wapewe na kazi ya kuchunguza na kubaini ni akina nani wamefanya haya ili tuupate ukweli na ukweli mtupu.
 
Mafia wa Tanzania Daima hao, si alitoka huko kwa shari.

Sasa ndo wamfanye binadamu mwenzao hivyo. Kwani si alikuwa na hiyari yake ya kuondoka km hakuridhika na mazingira ya kazi.

Malipo ni hapa hapa. Mungu atamlipia.
 
Hivi CCM kila kosa CDM si wakifute sasa propagaganda nyingine bwana hata mnashangaa so siku hizi lumumba ndio wasemaji wa usalama wa taifa....mimi kuzaliwa tanzania....huu ushetani mwingine ....

Nadhani hapa CDM inatajwa kwa sababu ndiye mmliki wa Tanzania Daima ambako KIBANDA alikuwa akifanyia kazi na kuondoka baada ya kutoelewana na wakubwa.
Mimi stashangaa, manake kama wanaweza kutangaza namba za simu za viongozi wa kiserikali ili watukanwe hili watashindwaje
 
Sasa ndo wamfanye binadamu mwenzao hivyo. Kwani si alikuwa na hiyari yake ya kuondoka km hakuridhika na mazingira ya kazi.

Malipo ni hapa hapa. Mungu atamlipia.

Mkuu kumbe wewe hujua maana ya Mafia? hizo ndo kazi zao, kulipiza visasi, vinyongo vinyongo na upuuzi mwingine kama huo
 
Kwa mtanzania kutokuwa na chama si rahisi. Kama ni kibaraka wa CCM basi CDM wamfanyia, na kama ni kibaraka wa CDM basi CCM wamemfanyia.

Kama fulani ana kesi nae .... fulani ka.....
ukizingatia kushinda kesi siku hizi ni ngumu
 
Mkuu kumbe wewe hujua maana ya Mafia? hizo ndo kazi zao, kulipiza visasi, vinyongo vinyongo na upuuzi mwingine kama huo

God forbid kwa kweli, watatumalizia watu wenye uchungu na hii nchi.
 
Narudia. Freeman Mbowe na Godbles Lema wanajua walichomfanya Kibanda.

mtaalamu wa haya ni Rama igondu wewe na washirika wenu so mlipanga mfanye hivyo ili muanze kuihubiria mauaji CHADEMA bila kujua hizo damu hata mfanyaje mungu anatumia kiadhibu CCM.....kazi kwenu tatizo CCM hammwamini mungu
 
tuko makini sana mkuu usitake kututoa kwenye ukweli kiujanja ujanja,tanzania daima na waajiri wake wa mwanzo hamtoki katika hili.tumieni janja nyingine sio hii ya kuitpia serikali.

Mimi si mfanyakazi wa Tanzania daima na sina sababu yoyote ya kuleta ujanja ujanja wa kuitetea Tanzania daima kwa namna yoyote ile kwa kuwa sijawahi kuwa na maslahi nayo.

Lakini nimeuliza swali kwamba, Kibanda hakuwahi kuwa na mgogoro na Tanzania daima, na aliondoka kwa amani kabisa na kwa kufanyiwa sherehe ya kuagwa, lakini alikuwa na mgogoro na serikali, kiasi cha JK kusema kabisa kule Ethiopia kwamba anakerwa na magazeti yanayochochea jeshi kuasi. Na hilo suala la jeshi kuasi liliandikwa na gazeti la Tz daima wakati Kibanda akiwa mhariri, na hadi hivi sasa ana kesi ya kujibu mahakamani kwa kosa la uchochezi.

Je huoni kwamba JK, anahusika katika hili kwa kuwa alikerwa na habari iliyoandikwa na kibanda? Ni kwa vipi, Pinda alihusishwa na ule mgogoro wa Ulimboka kwa kusema liwalo na liwe, lakin JK asikihusishwe kwenye hili kwa kutamka wazi kwamba alikerwa na habari yake? I am just thinking aloud, kama una utetezi wowote wa kunishawishi nisiendelee kufikiria ninavyofikiria basi ulete.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nadhani hapa CDM inatajwa kwa sababu ndiye mmliki wa Tanzania Daima ambako KIBANDA alikuwa akifanyia kazi na kuondoka baada ya kutoelewana na wakubwa.
Mimi stashangaa, manake kama wanaweza kutangaza namba za simu za viongozi wa kiserikali ili watukanwe hili watashindwaje
Hii inawezekana tu kwa nchi inayoongozwa kwa prpaganda na si sheri na sera za kujenga nchi....iweje serikali inayoongoza vyombo vya dora ising'amue hayo na kuzuia hayo maafa japo si kweli ni ktk kujenga hoja tu, je intelijensia ya akina kova na mabawabu wenzake inang'amuaga tu kwenye maandanmano hya chadema.........hii nchi ina laana na mimi nsema kwa ujinga wa watz kama ninyi na izidi kulaaniwa....mungu saidia ilaaniwe maana hakuna sasa wa kuwa nutral na kujadili mambo kwa upana wake wamebaki kuwa watumwa wa lumumba
 
Back
Top Bottom