Absalom Kibanda: Namuogopa Abdurahman Kinana

Absalom Kibanda: Namuogopa Abdurahman Kinana

Nadhani wengi hamumjui Kibanda, mimi hiyo Makala niliona online nilipoanza kuisoma wala sikupoteza muda wangu kuendelea kuisoma maana ni ushuzi mtupu.

Ni kweli Kibanda anamuogopa Kinana kwa sababu Kibanda ni kibaraka wa Lowasa na uwepo wa Kinana kama katibu Mkuu wa CCM si habari njema kwa kina Kibanda & co, huyu ni mtu wa ovyo sana.

Namshangaa sana Freeman Mbowe kuendelea kumvumilia Mhariri mpumbavu wa namna na kusababi Gazeti la Tanzania Daima kushuka mvuto na kupitwa na Gazeti la Mwananchi wakati mwanzo Tanzania Daima ndio lilikuwa linaongoza. Kama kuna mtu ambaye yupo karibu na Mbowe na anapenda Tanzania Daima lifanye vizuri basi huyu Kibanda afutwe kazi mara moja na nafasi yake apewe Ansbert Ngurumo.

Sasa nimepata jibu nilikuwa najiuliza kwa muda sasa,kwa nini Tanzania daima halina mvuto
tena?nimefika mahali siku hizi sisomi magazeti kabisa kwani lilibaki Tz daima lakini nalo hivi karibuni
halivutii kusoma kumbe tatizo ni huyu jamaa,kama kanaweza kuandika ujinga wa aina hii basi ni sawa
tanzania daima kupoteza mwelekeo.
 
Nilisoma makala ya Kibanda jana usiku online.Nimejichukia binafsi kwa sababu awali mimi ni mtu niliyekuwa namheshimu sana Kibanda.Lakini kwa makala hii ya leo kwenye Tanzania Daima nimeamini njaa ni mbaya sana.Sikuamini gazeti makini kama Tanzania Daima lingeweza kutoa makala ya kishenzi hivi na kama wataendelea kutoa makala za kijinga hivi tutatangaza rasmi ikususa kununua hili gazeti.Hana hata aibu kumtaja Mbowe ambaye ni bosi wake huko ndani ya makala tena kwa kumkashifu.

Nasikitika na nashangaa Freeman Mbowe kumuacha mchumia tumbo huyo kuwa mhariri mkuu wa gazeti la Kiongozi mkuu wa upinzani nchini.Nasikitika eti Ansbert Ngurumo mzee wa Maswali Magumu kuwa ndiye naibu mhariri akiwa chini ya huyu kipofu asiyeuona ukweli.

Kibanda anadhani hii ni ile miaka ya 1990.Nimuulize huyu kibaraka wa Kinana na CCM Je,kuteuliwa Kinana tayari maisha ya watanzania yamebadilika? Je tayari mishahara ya wafanyakazi imepanda? Je tayari pembejeo za kilimo zimepatikana? Je tayari vijana nchi nzima wamepata ajira? Kwa upofu wa Kibanda anadhani kwa vile yeye ameshapewa bahasha kumsifia Kinana basi ataaminisha kila mtu kumsifia tena bila aibu akilitumia kihuni gazeti la Mwenyekiti wa chama anachokikashifu.

Wito kwa Freeman Mbowe-Muondoe huyu mchumia tumbo kwenye gazeti lako kwa heshima yako na chama chako,na Ngurumo apewe uhariri Mkuu.Hakika Tunalililia gazeti pendwa MWANAHALISI.
 
Nimekusoma nivea lakini nikuulize kitu, una uhakika kwamba kibanda amekuwa honesty katika hii makala yake ama anamtumikia kafiri apate mradi wake. Angekuwa honesty kama angekiri tu kwamba ana maslahi na mtu/watu hao.

Ukijitahidi kuunganisha dots utaona ni kwanini kibanda anaandika makala very cheap kama hii. Tafuta uhusiano ama ukaribu/umbali wa Kinana na Lowasa ndipo ujue kilichopo nyuma ya pazia.



Hakuna namna yoyote mtu unaweza kuwa honest kwa kutetea ufisadi na mafisadi. Angekuwa honest angewashambulia wote kwakuwa hakuna fisadi mdogo wala mkubwa.


Kwanini Tunawakebehi watu wazuri Jamani? sasa kipi kizuri kwenu?
"The World suffers a lot.Not because of Violence of Bad People.But because of the silence of Good People as Kinana and other good people"
 
tokea mwanahalisi lifungiwe nimeacha kunnua magazeti zaidi ya kusoma vichwa vya habari
 
Ni mengi sana yatatokea mpaka tufikie kipindi kijacho cha Uchaguzi,watanzania Wazalendo/wenye misimamo thabiti tutawaona.Watakaoweka utu wao mfukoni kwa sababu ya pesa tutawaona vilevile Watanzania wazalendo tutawaona.Watanzania wenzangu tuendelee kuweka kumbu kumbu tu ili 2015 tuwahukumu vizuri.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
nikiunganisha na kauli ya mbowe kumsifia jk kupita kiasi naanza kuhisi katumwa na mbowe kuandika makala hiyo..naomba kuwasilisha na kusubiri mitusi
 
Come to think of it nimesoma makala ya Kibanda nikabaki hoi to say the least!! lakini kwa sababu sio mwandishi ambaye amewahi kuni-impress kwa method na analytical depth ya makala zake nikaona nisubiri wadau wengine greats; watasemaje kuhusu makala yake kuhusu Kinana.

Kwa kifupi ninaweza kusema Kibanda has a crush on Kinana or he is infatuated by Kinana or he was intoxicated by Kinana's persona!! the chap is embedded pure and simple, he was too long on words but too short on substance!!

1. Yuko silent kuhusu military record ya Kinana save for only saying "anajua mbinu za medani"!!?

2. Mtu mpembuzi yakinifu anajua ushindi wa Mkapa 1995 ulitokana zaidi na ushawishi wa Mwl. Nyerere na uchanga wa demokrasia nchini kuliko uwezo wa kampeni meneja Kinana.

3. Kibanda anamlaani Ben Mkapa kwa kum-sideline Kinana baada ya kampeni 1995, je nani anamjua zaidi Kinana kati ya Mkapa wajika lake na waliokaa katika cabinet pamoja na Absalom Kibanda?!

4. Kibanda anajaribu ku-trivialize skeletons za Kinana katika hujuma nyingi nyingi bila kujipa muda wa kufanya utafiti; Kibanda no research no right to speak; this is just the begining utajuta uliandika makala hii!

5. Kibanda ungejiuliza kwa nini Kinana alizikimbia main stream politics za Arusha akahamia kwenye peripheral arena za ukampeni meneja na shughuli nyingine zisizokuwa na direct contact na public kama NEC nk. nk Kibanda ushauri wa bure; mtafute Charles Makongoro Nyerere atakutonya kuhusu hilo!

6. Kibanda kinachowaumiza CCM ni rushwa, ubadhirifu wa mali ya umma na ufisadi ambao sasa wame-uinstitutionalize, usifikiri kina Makamba ambaye vuvuzela lake lililomnusuru Kikwete asipate kura chini ya asilimia 50 za uenyekiti na sio Kinana! au Mkama a fullbright scholar; ni wajinga sana kushindwa kuinusuru CCM, la hasha!bali mfumo umewafanya redundant.

7. Mkumbuke Gorbachev wa Urusi alipoingia madarakani na sera ya Glasnost & Perestroika!! mfumo ukaikataa, akanusurika mapinduzi na mwisho wake alitupiliwa mbali leo hii he is irrellevant katika siasa za Urusi

8. Kibanda; read my lips; CCM has to die first before it can be reformed; such are the dictates of history, Je Kinana na Mangula wanaweza kwenda tofauti na matakwa ya historia?!

. Umemsikia Mangula anasema in 6 months OUT; lakini Kinana on Jenerali on monday anasema hana muujiza wa kumaliza matatizo ya CCM; Kibanda what do you read from these two statements za wateule hao wa CCM unaowaogopa!?

10. CCM inapitia kipindi kinachoitwa "OLD AGE CRISIS"; ukilichanganya na OMBWE LA UONGOZI jawabu ni KIFO.

Kibanda bora ungejipa muda tuone kuliko kutamka UNAMUOGOPA KINANA! wewe kama nani lakini? au wewe Kibanda ndio winds of change that are flowing in the hearts and souls and ringing in the minds of many Tanzanians for a better Tanzania. Kibanda you could have done better, we are disappointed.

Kibanda makala yako ina viashiria vyote kwamba you are embedded! lakini tumekuelewa kwa sababu tunajua kwamba "He who pays the piper calls the tune" jaribu tena Kibanda; lakini nina hakika njia yako itakuwa ngumu, we have come a long way kuweza kudanganywa kirahisi.
 
Last edited by a moderator:
Kwanini Tunawakebehi watu wazuri Jamani? sasa kipi kizuri kwenu?
"The World suffers a lot.Not because of Violence of Bad People.But because of the silence of Good People as Kinana and other good people"

Aneisifia mvua lazima itakuwa imemnyeshea,Kinana amekuwapo ccm wakati wote huo pia ccm imekuwapo wakati wote huo(miaka50 ya uhuru bandia)ni yapi yamebadilika au lipi la kujivunia kama Watanzania kuwa kweli tupo na Serikali inayowajali wananchi?.Uongozi wa Nyerere ulijitahidi sana lakini yoote mazuri aliyoyafanya Mwalimu Jullius yapo wapi?(viwanda vyetu vipo wapi/shirika la reli lipo wapi?).
 
Hii stor imepandkzwa hajaanda kbanda ni wanamtandao wa knana wameipost kwa jina la kibanda
 
Nimekusoma nivea lakini nikuulize kitu, una uhakika kwamba kibanda amekuwa honesty katika hii makala yake ama anamtumikia kafiri apate mradi wake. Angekuwa honesty kama angekiri tu kwamba ana maslahi na mtu/watu hao.

Ukijitahidi kuunganisha dots utaona ni kwanini kibanda anaandika makala very cheap kama hii. Tafuta uhusiano ama ukaribu/umbali wa Kinana na Lowasa ndipo ujue kilichopo nyuma ya pazia.



Hakuna namna yoyote mtu unaweza kuwa honest kwa kutetea ufisadi na mafisadi. Angekuwa honest angewashambulia wote kwakuwa hakuna fisadi mdogo wala mkubwa.
nilimaanisha hivi kuwa honest huwezi kukutarajia kwa watu kama kibanda kamwe lazima ni kafiri upate mradi wako lol.hujambo lakini????
 
From this minute Kibanda ukiniona usiniite wala kunisalimia mie siwezi kuwa na urafiki na mtumishi na mwajiriwa wa ufisadi na mafisadi .This was too low hakika mawazo ya Nape na FM wa Idodomya ya kukaa US miaka 20 karudi na kasi akitaka kumpiku Mbowe ambaye amekuwa akimtupia madongo na kujipendekeza kwake .
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Wachawi wa Nchi hii ni wengi, kila tukipunga mapepo ya upande fulani yanatokea kwengine hata sujui tufanyeje, Waandishi kama Kibanda wapo wengi na kwa kiasi fulani wanakatisha watu tamaa na article zao, kuna mwingine naye alikuja juzi na kutuletea habari zake juu ya Waziri Membe, kinachonisikitisha ni kuwa waandishi wa habari wanamchango mkubwa na ustawi wa TAIFA bora la TANZANIA lakini kwa staili ya uandishi huu wa makundi napata shida nini kitafuata, tunavifuatilia vyombo vya habari ili tupate yaliyo mema na kujua ukweli wa mambo lakini ni tofauti na wanayotuletea waandishi wetu.

Binafsi huo umahiri wa Kinana Kibanda anaojitapa nao na kuuogopa sijauona, na sio kwamba nina wivu wa kike kama walivyozoea kutuambia la hasha! Kinana sio mgeni katika Siasa za Tanzania, alikuwepo katika nyazifa mbalimbali ndani ya ccm kwa muda mrefu tu, sasa sioni vp mambo aliyoshindwa kuyasimamia miaka yote huko nyuma leo ndio aweze kiasi cha kuogopwa na mwandishi kama KIBANDA.
 
Kwanini Tunawakebehi watu wazuri Jamani? sasa kipi kizuri kwenu?
"The World suffers a lot.Not because of Violence of Bad People.But because of the silence of Good People as Kinana and other good people"

We nae sijui umetokea wapi na haya mawazo yako mfu. Kinana nae ni mtu mzuri miongoni mwa watanzania?
Kinana huyu huyu aliyekwiba mashine za kufulia nguo za hospitali ya mount meru na kufungua kampuni ya udobi ya Falcon dry cleaners?
Kinana huyu huyu aliyeshiriki kikamilifu kuiuza loliondo kwa waarabu, ambao wamesababisha kila aina ya madhila kwa ndugu zetu wamasai.
Kinana huyu huyu anayesafirisha nyara za serikali kwenda nchi za nje?
Kinana huyu huyu anayetuhumiwa kuwaingiza wasomali wenzake nchini kinyume na taratibu za uhamiaji?
 
Nadhani wengi hamumjui Kibanda, mimi hiyo Makala niliona online nilipoanza kuisoma wala sikupoteza muda wangu kuendelea kuisoma maana ni ushuzi mtupu.

Ni kweli Kibanda anamuogopa Kinana kwa sababu Kibanda ni kibaraka wa Lowasa na uwepo wa Kinana kama katibu Mkuu wa CCM si habari njema kwa kina Kibanda & co, huyu ni mtu wa ovyo sana.

Namshangaa sana Freeman Mbowe kuendelea kumvumilia Mhariri mpumbavu wa namna na kusababi Gazeti la Tanzania Daima kushuka mvuto na kupitwa na Gazeti la Mwananchi wakati mwanzo Tanzania Daima ndio lilikuwa linaongoza. Kama kuna mtu ambaye yupo karibu na Mbowe na anapenda Tanzania Daima lifanye vizuri basi huyu Kibanda afutwe kazi mara moja na nafasi yake apewe Ansbert Ngurumo.

Mkuu Matola, Editors Forum yote iko chini ya Lowassa na kwa kukuhakikishia zaidi kuna jarida lilikuwa linasimamiwa na Kibanda liitwalo UMOJA siku hizi silioni tena sokoni ni Lowassa alikuwa analifadhili, kulitolea fedha na hata kuwalipa wahariri wake akiwemo Kibanda. Kibanda amekuwa ni mvunaji mkubwa wa fedha za Lowassa na naweza kusema hayuko kwa maslahi ya Taifa bali watu fulanifulani ambao anapata mshiko kutoka kwao.

Hata katika uchaguzi wa mwaka 2010 jarida hilo la UMOJA lilimpa Dkt. Slaa nafasi ndogo sana ya kushinda huku likipambwa na makala kubwa ya Kinana iliyokuwa na headline ya WAPINZANI HAWAWEZI KUINGIA IKULU KWA KUWATUPIA KASHFA MAKADA WA CCM.
 
Last edited by a moderator:
nilimaanisha hivi kuwa honest huwezi kukutarajia kwa watu kama kibanda kamwe lazima ni kafiri upate mradi wako lol.hujambo lakini????

Ok nivea sasa nimekuelewa, mwanzoni nilidhani kwamba unamaanisha kwamba kibanda ni honesty, kumbe sivyo!?
Btw mimi sijambo sana, nimeshangaa tangu usubuhi hatujaonana kabisa hadi jioni hii.
 
Last edited by a moderator:
Kibanda ni mpuuzi tu au ana agenda nyingine na huyu Kinana? CCM imefika hapo ilipo Kinana akiwemo katika kila chombo kizito cha maamuzi cha chama hicho. Hivi huo ukatibu mkuu utamwongezea nini Kinana ambacho kitamsaidia kuibadili CCM? Nawashangaa sana watu na akili zao timamu wanaodhani hizi dawa za kurefusha maisha ya CCM zitaifanya ipone gonjwa ambalo halina tiba! Tatizo la CCM ni zaidi ya UONGOZI wa juu peke yake. CCM imeoza tangu mashinani. Kinana au Mangula watafanyaje?

Huku juu kuanzia NEC yao viko vyama kadhaa wala sio kambi au makundi kama wengi tunavyofikiri. Msajili wetu tu hajaliona hili akifute chama hiki. Kibanda anataka ukatibu myeka wa Katibu Mkuu wa CCM.
 
Huyu jamaa ama anataka afutiwe kesi au anatafuta cheo. Si muda mrefu atafukuzwa kwenye hilo gazeti na atahamia gazeti la uhuru. Subiri tuone!
 
Back
Top Bottom