Absalom Kibanda: Namuogopa Abdurahman Kinana

Absalom Kibanda: Namuogopa Abdurahman Kinana

Ninakubaliana na Kibanda anapotoa tahadhali kwa upinzani kuwa wasimbeze Kinana.lakini sikubaliani naye anaposema Kinana atafufua CCM.inawezekana Kibanda anaamini hivyo kwa kuwa hajui hali halisi ya huku vijijini.CCM Siyo tu haikubaliki isipokuwa imefikia kiwango cha kuchukiwa.CCM imekorofisha kwa makundi yote ya jamii.huku mtwara wakulima wa korosho hawaki hata kuisikia.kule kanda ya ziwa tatizo la pamba limeizoofisha CCM kwa kiwango cha kutisha.na sasa CCM imewakosea hata wagöjwa wa ukimwi!.siamini kuwa Kinana anayo tiba ya yote hayo.
 
Kwanza nianze kwa kusema, Great Thinker hawezi kujenga hitimisho kwa kusoma makala moja ya mwandishi ambayo ukiichunguza kwa undani inajaribu tu kueleza wasifu wa mlengwa (Kinana).

Nafikili umeisoma makala kwa jicho moja huku tayari ukiwa una mawazo hasi kwa mlengwa (Kinana), matokeo yake hata mwandishi wa makala naye utamuona ni hasi.

Huu ndiyo ukweli, Kinana kwa kiasi kikubwa ameiwezesha CCM kujikusanya wakati wa kampeni zote za marais katika mfumo wa vyama vingi nchini. Hata pale ambapo kampeni za mwisho (2010) za urais zilitawaliwa na makundi aliweza pia kuyakutanisha na kuwa kitu kimoja.

Kelele za mizengwe haziwezi kufuta ukweli. linapokuja swala la oganaizesheni, Kinana ni kinara kwa hilo.

Kazi ya Ukatibu mkuu wa chama siyo kila kukicha kupiga kelele majukwaani kama wengi wanavyoaminishwa, bali ni oganaizesheni ndani ya chama.

kumuhukumu Absalom Kibanda kwa hili na kusema ni puppet wa mafisadi ni kutomtendea haki ukilinganisha na makala zake nyingi nyingine alizoandika pamoja na kwamba kila kitu Tanzania kinawezekana.


Nimekuwa na mawazo kama hayo. Siyo sahihi kubeza uteuzi wa kinana. Jaribu kutazama mwelekeo wa media katika kipindi cha takribani wiki mbili sasa, habari zote ni kuisifu CCM...huyu bwana siyo wa kubeza hata kidogo, SIASA NI MBINU NA MIKAKATI. Kinana anavyo vyote hivyo.

Ni vizuri ukajiandaa ...ukijua adui yako atakupa ushindani mkubwa hata kukushinda...kuliko kumdharau....

HATUWEZI KUSUBIRI ZAIDI YA 2015...
 
Great Thinkers,
Ni katika kipindi hicho cha kati ya mwaka 1995 na 2000 ndipo nilipokutana kwa mara ya kwanza na mara kadhaa na Kinana nyumbani kwake Masaki, jijini Dar es Salaam nikiwa nimeongozana na mhariri wangu, Muhingo Rweyemamu, ambaye sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni ambako nilipata fursa ya kumsikiliza na kuufahamu upeo mkubwa wa kuona mambo aliokuwa nao mwanasiasa huyo.

Mi jibu langu nimelipata kwenye red!
Huyu mwandishi ameweka heading kama ya kuvitahadharisha vyama vya upinzani lakini maudhui yake ni ya kuzitangaza sifa za Kinana!

My take: You may fool many but not all!
 
Tuna safari ndefu sana kufikia mabadiliko wa tz wenzangu, coz chambuzi kama za kibanda ziko nyingi sana kikweli zina kera sana
 
Nimekuwa na mawazo kama hayo. Siyo sahihi kubeza uteuzi wa kinana. Jaribu kutazama mwelekeo wa media katika kipindi cha takribani wiki mbili sasa, habari zote ni kuisifu CCM...huyu bwana siyo wa kubeza hata kidogo, SIASA NI MBINU NA MIKAKATI. Kinana anavyo vyote hivyo.

Ni vizuri ukajiandaa ...ukijua adui yako atakupa ushindani mkubwa hata kukushinda...kuliko kumdharau....

HATUWEZI KUSUBIRI ZAIDI YA 2015...
Kumbe huyu Mwenyekiti wa CCM si lolote mpaka Kinana ndio anategemewa kuja kuifufuwa CCM? this is very fun & interesting.

Yaani watu na akili zenu kabisa mnadhani tatizo ni CCM? CCM haina tatizo bali tatizo ni Serikali ya CCM, mwenye uwezo angalau kidogo kuiwezesha CCM angalau iungwe mkono uchaguzi ujao ni Jakaya Kikwete peke yake na Serikali yake na si Kinana na Sekretariet yake.

Tanzania ndio nchi pekee ninayoona watu wanatalajia mabadiliko ya kimaisha kutoka kwa viongozi wa chama tawala na si Serikali, huu ni zaidi ya Ujinga, ila Absalom Kibanda ndio mjinga wa kwanza maana wa mwisho ana nafuu.
 
Waambie waliokutuma kwamba wenyewe wamekataa kufungua mlango.
Kwanza muulize anadhani wote tunawekewa bundle za bure ili tuwe na huo muda wa kijinga wa kumaliza bundle zetu huko Youtube? Nonsense.
 
Kama hawa ndo wahariri wa taifa hili basi nchi itazidi kupoteza mwelekeo, nimesikitishwa sana na hoja ya kupaka mafuta ufisadi eti "sio hoja tena" pasipo kujua kwamba ufisadi ndo umetufikisha hapa. Kwa mtu yeyote makini ukisoma makala ya huyu anaejiita mhariri utagundua kuwa anamaslai binafsi na kinana na nimarafiki ya muda mrefu, kwani kaeleza kuwa toka miaka ya 90 alikuwa anaenda kwa kinana pamoja na mhariri wake ambae kwa sasa ni mkuu wa wilaya. Baada ya mhariri aliyekuwa akienda nae kwa kinana kupewa ukuu wa wilaya na yeye ameamua kujipendekeza ili kujaribu bahati yake. Penye maslai binafsi UKWELI hutupwa pembeni,thus y wasafirishaji wa nyara za taifa ndio wasifiwao na wahariri wetu.
 
Kama Kanali Mstaafu Kinana ni mwadilifu ki vile ilikuwaje ushindi wa Kikwete ukawa wa kuchakachua? Inawezekanaje akawa hakuhusika? Kibanda anasema alipata mafunzo ya kimkakati, mkakati gani wa uwizi wa kura? Kibanda anataka kutoa ujumbe gani kwa wapinzani- kuwatisha, kuwakatisha tamaa, kuwanyong'onyeza? Way forward ya Kibanda ni ipi? Tufute vyama vya upinzani sababu ya uteuzi wa Kibanda? Busara ya Kikwete ni ipi? Mwenye kuanzisha makundi ndani ya CCM ni yeye, mwenye kutoa uteuzi kwa MISINGI YA urafiki, udugu, mizengwe ni yeye. Historia imemrudi, ikamwonyesha enzi za Mangula chama kiliendeshwaje, amejaribu kulinganisha uongozi wake akaona matokeo. Kikwete ni kama mtoto aliyetaka kushika moto akaungua na kuurudisha haraka. Kurudisha mkono sio busara ni makali ya moto. Matukio yana busara sio Kikwete.
Kibanda anamsifu Kikwete na Kinana ili kuomba rushwa kwa watawala hawa, anajua Kikwete ni mlevi wa sifa, anampa rushwa ya sifa akisubiri marejesho ya ukuu wa wilaya. Asubiri atapata, lakini asijaribu kufikiri kwa niaba ya Dr. Slaa, Mbowe Prof. Lipumba wala Zito, afikiri kwa niaba yake mwenyewe
 
Huyu nae sijui kakurupushwa kutoka wapi. Hizi gongo mnazonyweshwa mchana wa jua kali zinawaharibia akili zenu. Aliyeandika makala inayodaiwa kuichonganisha serikali na wanajeshi ni Kamanda Samsoni Mwigamba.


Mwita Maranya pole kwa kuchanganyikiwa na kimbunga kinachoisomba chadema kwa sasa. Nina uhakika na nilichoandika sema wewe ndo umelewa gongo na mnazi hadi unasahau kesi inayomkabili kamanda wa zamani wa CDM Absalom Kibanda. Uliza chadomo wenzio watakueleza juu ya kesi inayomkabili Kibanda. Acha kuweweseka dogo Kinana ndo kwaaaanza ameanza mashambulizi kusini.
 
Kibanda ni mpuuzi tu au ana agenda nyingine na huyu Kinana? CCM imefika hapo ilipo Kinana akiwemo katika kila chombo kizito cha maamuzi cha chama hicho. Hivi huo ukatibu mkuu utamwongezea nini Kinana ambacho kitamsaidia kuibadili CCM? Nawashangaa sana watu na akili zao timamu wanaodhani hizi dawa za kurefusha maisha ya CCM zitaifanya ipone gonjwa ambalo halina tiba! Tatizo la CCM ni zaidi ya UONGOZI wa juu peke yake. CCM imeoza tangu mashinani. Kinana au Mangula watafanyaje?

Huku juu kuanzia NEC yao viko vyama kadhaa wala sio kambi au makundi kama wengi tunavyofikiri. Msajili wetu tu hajaliona hili akifute chama hiki. Kibanda anataka ukatibu myeka wa Katibu Mkuu wa CCM.

Hapo kwenye Red; hilo ni moja ya tu ya mambo ambayo Kibanda alipaswa kujiuliza kabla hajafikia hitimisho lake. Anamchukulia Kinana kama mtu ambaye hakuwa mjumbe wa NEC wala CC ya CCM, anamuona kama mtu aliyetoka mwezini na kudondoshwa kuja kuiokoa CCM. Ni kama vile Kinana hajui myumbo uliopo wa CCM na hata kwenye vikao vya CC na zaidi majukwaa ya siasa huwa hashiriki.

Maandiko mengi ya Kibanda yamekuwa ya kimahaba kupindukia, akileweshwa kwa fedha basi anasahau hata kufikiri na kujenga hoja walau kwa uhalisia wake. Kitu kimoja kikubwa alichoniuza ni kupuuza tuhuma za ufisadi na kuziona si lolote. Na hiyo ndiyo imekuwa kazi yake kupuuza tuhuma na kusafisha kwa nguvu zote wanaotuhumiwa. Amekuwa akifanya hivyo kwa Lowassa kwa maslahi anayojua.
 
Mwita Maranya pole kwa kuchanganyikiwa na kimbunga kinachoisomba chadema kwa sasa. Nina uhakika na nilichoandika sema wewe ndo umelewa gongo na mnazi hadi unasahau kesi inayomkabili kamanda wa zamani wa CDM Absalom Kibanda. Uliza chadomo wenzio watakueleza juu ya kesi inayomkabili Kibanda. Acha kuweweseka dogo Kinana ndo kwaaaanza ameanza mashambulizi kusini.
Si vyema ukionekana ni taahira hapa jamvini, wewe ni mwehu na mjinga wa kwanza, Mwandishi wa Makala ni ukurasa wa kalamu ya Mwigamba, ambayo mwandishi Samson Mwigamba.

Absalom Kibanda anaunganishwa tu kwenye kesi hiyo kwa sababu yeye ndio Mhariri mkuu, na Theophile Makunga ameunganishwa humo kwa sababu kampuni yao ya Mwananchi ndio iliyochapisha hilo toleo, ni sawa na kesi ya kupinga Ubunge ni lazima na mwanasheria mkuu aunganishwe kwenye kushatikiwa. Kilaza Mbulula wewe.
 
Kamanda Mbowe atahusishwa na hili la Kibanda atake asitake, ahusike asihusike!

Inaonekana mtego wa kumbomoa Mbowe umekamilika, je atanasa au atausambaratisha?
 
Kwanza muulize anadhani wote tunawekewa bundle za bure ili tuwe na huo muda wa kijinga wa kumaliza bundle zetu huko Youtube? Nonsense.

Hivi nyinyi mnataka kubebwa na wahariri wa magazeti mpaka lini? chama chenu hakiwezi kujitangaza mpaka msifiwe? mlizoea kubebwa na kusifiwa na Tanzania daima sasa kibao kimewageuka mnahaha!
Viongozi wenu na magazeti yenu tayari wamewekwa mfukoni! sasa sijui mtakimbilia wapi! na huku kwetu CUF ndio kumejaa labda mkimbilie TLP au muanzishe chenu!

ndo siasa hizo baba! mikakati na mipango!
 
Kamanda Mbowe atahusishwa na hili la Kibanda atake asitake, ahusike asihusike!

Inaonekana mtego wa kumbomoa Mbowe umekamilika, je atanasa au atausambaratisha?
Kama mimi ningekuwa ndio Mbowe ningeagiza Management kumfuta kazi Absalom Kibanda mara moja, wacha mbali swala la Uongozi wake Chadema lakini Kibanda anasababisha Gazeti la Tanzania Daima kukosa mvuto hivyo mauzo kushuka, na hapa Familia ya Mbowe ndio Losers. wachilia mbali Politics.
 
Hahahaaahaha, miye ndiye Kibanda mwenyewe....heri lawama kuliko fedheha. Watanzania hampendi kuambiwa ukweli, mna maradhi ya kushabikia ujinga. Mnashindwa kusoma makala mkaelewa. Mwenye mawazo kinzani na haya aandike makala Tanzania Daima, tutaichapisha, nashukuru kwamba nyote mmeusoma ujumbe wangu kwa upinzani...
 
Back
Top Bottom