Absalom Kibanda: Namuogopa Abdurahman Kinana

Absalom Kibanda: Namuogopa Abdurahman Kinana

Hivi nyinyi mnataka kubebwa na wahariri wa magazeti mpaka lini? chama chenu hakiwezi kujitangaza mpaka msifiwe? mlizoea kubebwa na kusifiwa na Tanzania daima sasa kibao kimewageuka mnahaha!
Viongozi wenu na magazeti yenu tayari wamewekwa mfukoni! sasa sijui mtakimbilia wapi! na huku kwetu CUF ndio kumejaa labda mkimbilie TLP au muanzishe chenu!

ndo siasa hizo baba! mikakati na mipango!

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA], Dk. Willibrod Slaa, ameichambua safu mpya ya uongozi wa Chama cha Mapinduzi [CCM] iliyoundwa hivi karibuni mjini Dodoma, akisema wana taswira ya ufisadi.

Amesema kuwa hali hiyo inatokana na baadhi yao kuhusika kwenye matukio kadhaa ya kifisadi moja kwa moja.

Akizungumza kuhusu mtazamo wake kwa safu hiyo mpya ya uongozi wa CCM iliyoundwa na Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, katika mkutano mkuu uliomalizika juzi, Dk. Slaa alisema haoni jambo jipya.

"Nadhani hakuna jambo jipya, kipya ni kwamba wameteuliwa jana, lakini wote ni wazoefu wachafu," alisema.

Katika safu hiyo, Kikwete anasaidiwa na makamu wawili, Philip Mangula wa bara na Dk. Ali Mohamed Shein wa visiwani na pia alimteua kada mkongwe, Abdullahman Kinana kuwa Katibu Mkuu mpya wa CCM. Wengine wanaounda Sekretarieti ni Zakhia Meghji, Mwigulu Nchemba, Asha-rose Migiro, Vuai Ali Vuai, Nape Nnauye na Mohamed Seif Khatib.

Akimchambua mmoja baada ya mwingine, Dk. Slaa alimtuhumu Mangula kuwa ni mmoja wa watu waliohusika na ufisadi wa fedha za Akaunti ya Malipo ya Nje(EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania.

"Makamu Mwenyekiti Mangula anahusika na EPA, vimemo vingi vya kutaka fedha za EPA vimetokea kwake…sioni leo atajisafishaje kuleta tumaini jipya kwa Watanzania," alisema.

Kuhusu Meghji, Dk. Slaa alisema huyo ndiye aliyeandika barua na kudanganya kuwa fedha hizo za EPA zimetoka kwa ajili ya Usalama wa Taifa.

"Sasa mtu kama huyo aliyedanganya, leo hii ukamweka kwenye fedha maana yake ni ku-‘recycle material' ile ile," alisema Dk. Slaa.

Akimchambua Katibu Mkuu, Kinana, alisema kigogo huyo ana mkono katika biashara chafu za makampuni ya meli na kwamba hajakanusha mpaka sasa.

Dk. Slaa alisema Kinana ambaye alikuwa meneja kampeni wa mgombea urais wa CCM mwaka 2010, katika chaguzi hizo CCM imeshutumiwa kwa kuiba kura, hivyo uteuzi wake ni kukubali kuzika demokrasia nchini.

Alisema timu hiyo imeundwa mahsusi kwa ajili ya kujiandaa kuiba kura mwaka 2015. Dk. Slaa aliongeza kuwa baada ya uchaguzi, CCM walitumia fedha nyingi kwa ajili ya kwenda kufanya utafiti wa kukijenga upya chama chao, ambao uliozaa kauli mbiu ya Kujivua Gamba', kwamba pamoja na kazi ya kitaalamu wameshindwa kuvuana magamba.

Alifafanua kuwa hatua hiyo inatokana na ukweli kwamba walioitwa magamba sasa wamo kwenye safu mpya ya uongozi wa CCM. Katika kile kinachoonekana kuwa ni kumjibu Rais Kikwete hasa kutokana na kauli yake kuwa wapinzani wanafanya kazi ya kueneza uongo na kuwataka makada wa CCM kujibu mapigo, Dk. Slaa alimtaka aache kuwadanganya Watanzania.
 
Nimeshtuka sana kusikia na kufahamu eti huyu ni mtu anayelipwa mshahara na Freeman Mbowe.Nasema tena ni aibu kubwa.Ni sawa na mtoto kumtukana matusi ya nguoni baba yake mzazi.
Makala hii ukiisoma haina tofauti na makala za Rai,Uhuru,Jambo Leo,Mzalendo na Habari Leo.
Kama huyu Kibanda ni mstaarabu ajiuzulu nafasi yake kwa heshima ya Freeman Mbowe.Vinginevyo vijana wataenda kumtoa kwa Bakora.Hawezi kumdhalilisha Mwenyekiti Mbowe hivihivi huku vijana wakichekelea.
Aibu kubwa unanyea mkono unaolia chakula.Kibanda aibu hii ni yako!...
 
Kwa mtu aneamini ktk mabadiliko hawezi kuangalia nani kasimama anapotaka kwenda then asitishe mpaka mtu huyo atakapotoka,nadhani Bw.Kibanda alitaka kutueleza namna anavyomfikiria.Mabadiliko yanapofika huwa hayana kawaida ya kutizama nani kasimama wapi ama ana nini?Yuko wapi Ghadaf je hakuwa na historia nzito ktk nchi yake,Afrika na duniani?

Nijuavyo mimi ni kwamba Kinana na wenzake wamerejeshwa ktk safu ya uongozi ili kulinda maslahi ya chama cha mapinduzi,wapo ili kuhakikisha 2015 nchi inabakia mikononi mwa chama chao lakini si kujenga taifa lenye misingi kupitia chama chao kilichopo madarakani.So kwa kibanda kuzungumza yake ni sawa kwa kuwa yeye ni mwoga wa mabadiliko na kwa kauli yake nadhani sie inatujenga zaidi kwakuwa maneno yake ni kama kuongeza petrol kwenye moto.

Sipendi kumbeza Kibanda lakini siamini kuwa uwepo wa Kinana na Mangula ktk siasa kwa muda huu ni maandalizi ya mauti ya upinzani,huku site watz hawahitaji mabadiliko kupitia CCM,what they need ni reform na to overhaul is the best solution.So bado naamini kuwa tuendako kwa upinzani ni kuzuri zaidi kwa kila watakalo jihami basi upinzani will tell the people ukweli wa mambo.

95% wa viongozi wa CCM na watendaji wake ktk serikali wako kwaajili ya kuula,si rahisi kufumua mfumo mzima si jambo la leo wala kesho,Naomba mwenye kuweza kunukuliwa kwa maneno yangu kama chama cha mapinduzi kikipata ushindi 2015 viongozi waliotajwa na Kibanda wataomba kuachia ngazi na hii ni kwa kuwa jukumu waliliopewa litakuwa limetimia.Lakini malengo ya watz na matamanio yao hayatokuwa yametimia kitu ambacho bado kinanipa nguvu kuwa mabadiliko yako jirani kufika!
 
Kama mimi ningekuwa ndio Mbowe ningeagiza Management kumfuta kazi Absalom Kibanda mara moja, wacha mbali swala la Uongozi wake Chadema lakini Kibanda anasababisha Gazeti la Tanzania Daima kukosa mvuto hivyo mauzo kushuka, na hapa Familia ya Mbowe ndio Losers. wachilia mbali Politics.

Kwa taarifa yako, mauzo ya Tanzania Daima yanaongezeka kila kukicha. Dunia inazungumzia Uhuru wa Uhariri wakati Watanzania wajinga kama wewe mnahubiri 'udikteta wa wamiliki'. Kama hatutajifunza kuheshimu maoni tusiyoyapenda tutaendelea kubakia pale pale tulipo.
 
muogope sana.juzi tuu katuhumiwa kusafirisha meno ya tembo kupitia kampuni yake yani ukicheza anaweza akakusafirisha na ww.
elephant_poaching_nyt_600-440x219.jpg
 
Ninakubaliana na Kibanda anapotoa tahadhali kwa upinzani kuwa wasimbeze Kinana.lakini sikubaliani naye anaposema Kinana atafufua CCM.inawezekana Kibanda anaamini hivyo kwa kuwa hajui hali halisi ya huku vijijini.CCM Siyo tu haikubaliki isipokuwa imefikia kiwango cha kuchukiwa.CCM imekorofisha kwa makundi yote ya jamii.huku mtwara wakulima wa korosho hawaki hata kuisikia.kule kanda ya ziwa tatizo la pamba limeizoofisha CCM kwa kiwango cha kutisha.na sasa CCM imewakosea hata wagöjwa wa ukimwi!.siamini kuwa Kinana anayo tiba ya yote hayo.

Tungejenga hoja za klupingana kwa namna hii, tungesaidia kujijenga kifikra. Hii ndiyo critical appraisal inayopaswa kufanywa na watu walioenda shule.
 
Hahahaaahaha, miye ndiye Kibanda mwenyewe....heri lawama kuliko fedheha. Watanzania hampendi kuambiwa ukweli, mna maradhi ya kushabikia ujinga. Mnashindwa kusoma makala mkaelewa. Mwenye mawazo kinzani na haya aandike makala Tanzania Daima, tutaichapisha, nashukuru kwamba nyote mmeusoma ujumbe wangu kwa upinzani...
Njaa mbaya sana, lakini teuzi za UDC zimejaa. Pasco angalia huyu jamaa sasa amefirisika mpaka akili, endelea kuliuwa Gazeti la Tanzania Daima ambalo mapato yake yameshuka uku ukiwa wewe ndio Mhariri mkuu.

Freemedia Management nitawashangaa kama hawatakufuta kazi wakati unaliuwa Gazeti. au hizi ndio terms ulizopewa JK ili ufutiwe ile kesi iliyopo Mahakamani? Maana Theophil Makunga yeye tayari ameshatuthibitishia kwenye kamati ya Nchimbi kuchunguza mauwaji ya Mwangosi.

Maoni yangu kwenye tume ya katiba mpya wiki hii, nitapendekeza iingizwe kwenye katiba waandishi wote waongo na mamluki wanyonge hadi kufa.
 
Last edited by a moderator:
Hahahaaahaha, miye ndiye Kibanda mwenyewe....heri lawama kuliko fedheha. Watanzania hampendi kuambiwa ukweli, mna maradhi ya kushabikia ujinga. Mnashindwa kusoma makala mkaelewa. Mwenye mawazo kinzani na haya aandike makala Tanzania Daima, tutaichapisha, nashukuru kwamba nyote mmeusoma ujumbe wangu kwa upinzani...

Kama wewe ndiye Mwenyewe umepewa shilingi ngapi kukitukana chama cha bosi wako?
Na hapa unayemwambia anashabikia ujinga ni nani? Unamwambia Freeman Mbowe bosi wako ni mjinga? Wanaomuunga mkono Mbowe ni wajinga? Mnafiki mkubwa wewe.
Unadhani ukuu wa wilaya Kinana atakubembelezea ili upewe? Leo nimeamini njaa ni mbaya.Pamoja na matusi yote kwa upinzani unaoongozwa na bosi wako bado unakuja hapa jamvini kujitapa kwamba umemkomesha Mbowe bosi wako na chama chake?
Kweli wewe ni mnafiki wa kutupwa.
 
Sitapokea fedha yoyote kudhalilisha UTU wangu.. Copy it Kibamba
 
Tungejenga hoja za klupingana kwa namna hii, tungesaidia kujijenga kifikra. Hii ndiyo critical appraisal inayopaswa kufanywa na watu walioenda shule.

Nenda kwanza uombe kazi Uhuru na Mzalendo ndiyo urudi hapa jamvini.

Hivi Mhariri wa gazeti la Yanga Imara anaweza kuchapa makala kwenye gazeti lake ya kusifu kikosi cha Simba na kubeza kikosi cha Yanga halafu bado kesho yake akajitapa kwenye mitandao eti alikuwa anaeleza ukweli?

Hakika huyo atafukuzwa kazi hata kabla gazeti halijaisha mitaani.
 
Kwa taarifa yako, mauzo ya Tanzania Daima yanaongezeka kila kukicha. Dunia inazungumzia Uhuru wa Uhariri wakati Watanzania wajinga kama wewe mnahubiri 'udikteta wa wamiliki'. Kama hatutajifunza kuheshimu maoni tusiyoyapenda tutaendelea kubakia pale pale tulipo.
Mjinga ni wewe unayeweza kuthubutu kuja kudanganya watu hapa kwamba mauzo yanapanda wakati yanashuka na ukweli ni kwamba sasa hivi Mwananchi ndio Gazeti linalonunuliwa zaidi, na hawa wakiweza ku negotiate na Mzee Mwanakijiji pamoja na Mwalimu Mkuu wa watu Mzee Mayenga basi hilo Gazeti kwishney.

Nyinyi ni waandishi uchwara ndio maana Mkapa aliwadharau na hakutaka muwe mnamuhoji kwa sababu uwezo wenu ni mdogo sana na mnaongozwa na njaa.

Kila Media House ina sera zake, haiwezekani Mhariri wa Uhuru na Mzalendo akandaa makala ndefu kuupamba uongozi wa Chadema, wewe hata umesoma hukuelimika na nyinyi ni janga kwa Taifa hili, naitafuta ile katuni ya Kenya mnayomlamba viatu JK nikuwekee hapa.
 
Mimi namuogopa Absolom Kibanda kuliko yeye anavyomuogopa Kinana na nahisi wametoka mbali. Ni nani angeweza kupewa list ya majina ya Kamati ya utendaji ya CCM usiku wa kuamkia kikao cha NEC kuwa Kinana ni katibu mkuu na list nzima na kuitoa kwenye gazeti la Tanzania Daima wakati Kikao kikiendelea na tulijua sio yenyewe au Mwenyekiti JK angebadili baada ya kuvuja lakini wapi ikatumika list ya kwenye gazeti la Absolom Kibanda ambayo hata hapa JF iliingia saa 5:00 usiku kabla ya alfajiri.
Mimi sioni mantiki ya kumtimua JEMBE kama hili wakati Chama chenyewe ni cha Demokrasia
 
Kibanda anamsifu Kikwete na Kinana ili kuomba rushwa kwa watawala hawa said:
Sina sababu ya kuomba rushwa kwa Kinana. Rushwa ya nini na ya namna gani? Hivi ninyi Watanzania hamuwezi kuamini kwamba mtu anaweza akatoa maoni yake binafsi kwa uhuru pasipo kudai chochote? Namfahamu Kinana, naufahamu upinzani. Nimeishi na wanasiasa wa takriban vyama vyote, nawajua vyema, naujua upinzani. Nilipokuwa nikiandika makala za kumshangaa na kumpinga Mrema zama nikiwa Rai baadhi ya watu waliniita mwendawazimu, nilipomponda Samuel Sitta nilishambuliwa lakini kwa wote hao wawili ukweli kuhusu wao unajifunua kila siku.

Nimempa sifa Kinana ninazozijua, nimesema wazi kwamba anaingia madarakani CCM ikiwa mahututi na wakati ikichungulia kaburi. Nimeeleza wazi kwamba sitaki kuona upinzani ukifa kwani hata mimi naamini kwamba mabadiliko yatatoka nje ya CCM. Sasa kejeli zote hizi za nini? Hivi mnadhani kununuliwa ni kitu rahisi ninyi siyo!
 
Kwa taarifa yako, mauzo ya Tanzania Daima yanaongezeka kila kukicha. Dunia inazungumzia Uhuru wa Uhariri wakati Watanzania wajinga kama wewe mnahubiri 'udikteta wa wamiliki'. Kama hatutajifunza kuheshimu maoni tusiyoyapenda tutaendelea kubakia pale pale tulipo.

Naamini Kesho Tanzania Daima litapambwa na ziara ya Kinana Mtwara.Pole sana ndugu yangu.Kinana amefanya kazi kubwa kupiga Pentagon.Yaani anamweka mfukoni Mhariri wa gazeti la Mkiti wa chama kikuu cha upinzani.
 
Mjinga ni wewe unayeweza kuthubutu kuja kudanganya watu hapa kwamba mauzo yanapanda wakati yanashuka na ukweli ni kwamba sasa hivi Mwananchi ndio Gazeti linalonunuliwa zaidi, na hawa wakiweza ku negotiate na Mzee Mwanakijiji pamoja na Mwalimu Mkuu wa watu Mzee Mayenga basi hilo Gazeti kwishney.

Nyinyi ni waandishi uchwara ndio maana Mkapa aliwadharau na hakutaka muwe mnamuhoji kwa sababu uwezo wenu ni mdogo sana na mnaongozwa na njaa.

Kila Media House ina sera zake, haiwezekani Mhariri wa Uhuru na Mzalendo akandaa makala ndefu kuupamba uongozi wa Chadema, wewe hata umesoma hukuelimika na nyinyi ni janga kwa Taifa hili, naitafuta ile katuni ya Kenya mnayomlamba viatu JK nikuwekee hapa.

Nilikuja Tanzania Daima nikitokea Mwananchi. Hakuna wakati Tanzania Daima limewahi kuwa juu kimauzo kwa Mwananchi ingawa mara kadhaa tumefanya vizuri sokoni kuliko wao. Kwa taarifa yako Mwananchi wanajua nini kinafanyika Tanzania Daima na kimsingi wanajua kwamba tungekuwa na investment kama yao wasingeweza kushindana na sisi. Kwa taarifa yako Mzee Mwanakijiji ni miongoni mwa waandishi wanaochangia mada Mwananchi. Tanzania Daima litaendelea kuimarika iwapo tutaoa uhuru wa mawazo kwa watu wanaofikiri kinyume cha mapenzi yenu.
 
Nenda kwanza uombe kazi Uhuru na Mzalendo ndiyo urudi hapa jamvini.

Hivi Mhariri wa gazeti la Yanga Imara anaweza kuchapa makala kwenye gazeti lake ya kusifu kikosi cha Simba na kubeza kikosi cha Yanga halafu bado kesho yake akajitapa kwenye mitandao eti alikuwa anaeleza ukweli?

Hakika huyo atafukuzwa kazi hata kabla gazeti halijaisha mitaani.

Aliyekudanganya kwamba Tanzania Daima ni gazeti la Chadema ni nani? Kumbe unajadili jambo usilolijua sawasawa? Uhuru na Mzalendo siyo saizi yangu. Naamini katika fikra huru na halisi. Mimi si bendera fuata upepo.
 
Kibanda,

..sasa kwanini humpingi Kinana kutokana na ufisadi wake kuanzia Loliondo, mpaka sasa ambapo ni wakala wa kusafirisha pembe za ndovu??

..rekodi ya Kinana kama FISADI ni ya kutukuka, lakini badala ya kuwatahadharisha vijana kuhusu hilo, unaleta stori za kumtukuza.
 
Last edited by a moderator:
Aliyekudanganya kwamba Tanzania Daima ni gazeti la Chadema ni nani? Kumbe unajadili jambo usilolijua sawasawa? Uhuru na Mzalendo siyo saizi yangu. Naamini katika fikra huru na halisi. Mimi si bendera fuata upepo.

Labda nikuulize wewe
Mbona sijawahi sikia Jenerali Ulimwengu na magazeti yake wakituhumiwa kuwekwa mfukoni na kumpigia debe mtu au watu?
huoni hii ni ishara wewe au ninyi kuna kitu mnakosea?
 
Mimi napendekeza wote tuliochukizwa na babaishaji wa Kibanda tupeleke masikitiko yetu Freemedia na mwenye mawasiliano ya Freeman Mbowe ayaweke hapa ili tumueleze ukweli kwamba Gazeti lake linatumika kuhujumu Mabadiliko na amfute kazi mara moja Absalom Kibanda.

Free Media Limited
mtaa wa Mkwepu na Makunganya, SLP 15261, Dar es salaam, Tanzania
simu +255-22-2120604 • faksi +255-22-212623

tzdaima@freemedia.co.tz

Namba ya Freeman Mbowe hii 0784 779944
 
Back
Top Bottom