Absalom Kibanda: Namuogopa Abdurahman Kinana

Absalom Kibanda: Namuogopa Abdurahman Kinana

Nilikuja Tanzania Daima nikitokea Mwananchi. Hakuna wakati Tanzania Daima limewahi kuwa juu kimauzo kwa Mwananchi ingawa mara kadhaa tumefanya vizuri sokoni kuliko wao. Kwa taarifa yako Mwananchi wanajua nini kinafanyika Tanzania Daima na kimsingi wanajua kwamba tungekuwa na investment kama yao wasingeweza kushindana na sisi. Kwa taarifa yako Mzee Mwanakijiji ni miongoni mwa waandishi wanaochangia mada Mwananchi. Tanzania Daima litaendelea kuimarika iwapo tutaoa uhuru wa mawazo kwa watu wanaofikiri kinyume cha mapenzi yenu.
Kabla ya kukwambia Alamsiki ngoja nikupe orodha ya waandishi ambao mpo in the same category, only time will tell about you.

1. Deodatus Balile
2. Jackton Manyerere
3. Charles Mulinda
4. Ramadhani Semtawa
5. Yusuf Halimoja
6. Absalom Kibamba. New Member of this Group.
 
Kuna watu kutwa wanahubiri demokrasia na uhuru wa mawazo lakini kiukweli bado wapo kwenye lindi kubwa la usingizo fofo wa "zidumu fikra sahihi za mwenyekiti"
In short ni kwamba hutakiwi kufikiri nje ya box wanalofikiria viongozi vinginevyo utaitwa majina yote mabaya duniani
 
Hahahaaahaha, miye ndiye Kibanda mwenyewe....heri lawama kuliko fedheha. Watanzania hampendi kuambiwa ukweli, mna maradhi ya kushabikia ujinga. Mnashindwa kusoma makala mkaelewa. Mwenye mawazo kinzani na haya aandike makala Tanzania Daima, tutaichapisha, nashukuru kwamba nyote mmeusoma ujumbe wangu kwa upinzani...

Hakuna anayeukataa ukweli maana daima unashinda lakini uwe ukweli kweli na si hicho chepesi ulichoandika kwenye makala yako. Unajisikiaje kuandika makala ambayo inashindwa kuonesha namna gani Kinana ataua vyama vya upinzani just kwa kuwa tu Campaign manager wa wagombea urais na waziri tu? Unapoandika makala ukaweka facts zidhani kama kuna mtu atakutilia shaka maana facts daima zinashinda.

Walau ungeonesha strategically Kinana ana uniqueness zipi ukilinganisha na makada wengine wa CCM? Je hufahamu kwamba Kinana amekuwa mjumbe wa CC na NEC ya CCM ambavyo ni vyombo vya maamuzi? Kama unajua alikuwa huko mdororo wa CCM umetokeaje wakati akiwa miongoni mwa decision makers ndani ya chama? Ina maana alikuwa kimya wakati anaona chama kinaelekea kuzimu? Lakini kichekesho kingine kwenye makala yako ni kupuuza tuhuma za Ufisadi alizonazo Kinana na kuziona zisizo na mashiko na mantiki. Kwako wewe ufisadi si lolote na ndiyo umekuwa muegemeo wako hata kwa Edward Lowassa.

Umejiuliza kidogo tu kuhusu umma na nafasi yake katika kuleta mabadiliko? Unauchukulia umma uleule wa enzi za Kinana au huu tulio nao sasa usiomfahamu hata huyo Kinana? Makala yako imekosa credibility na analysis inayozingatia muktadha na hali halisi ya kisiasa nchini. Umeongozwa na mahaba zaidi.
 
Kibanda anajitengenezea mazingira ya kukumbukwa na Kinana. Wana JF ufisadi utatuangamiza kama hawatatokea watu wa kujitoa mhanga.
 
Kuna watu kutwa wanahubiri demokrasia na uhuru wa mawazo lakini kiukweli bado wapo kwenye lindi kubwa la usingizo fofo wa "zidumu fikra sahihi za mwenyekiti"
In short ni kwamba hutakiwi kufikiri nje ya box wanalofikiria viongozi vinginevyo utaitwa majina yote mabaya duniani
Mkuu nenda kamshauri haya Mhariri mkuu wa Uhuru na Mzalendo au Habari Corporation. CCM wana vyombo kibao vya kueneza Propaganda zao, sasa watu ndio maana wanashindwa kuelewa wakiona mtu kama Kibanda naye kujiunga kucheza mdundiko wa CCM. Think Big

Makala hii ingetoka kwenye Gazeti la Rai au Uhuru au Jambo leo wala hakuna ambaye angeshangaa, labda tu kama unajitia upofu makusudi.
 
Aliyekudanganya kwamba Tanzania Daima ni gazeti la Chadema ni nani? Kumbe unajadili jambo usilolijua sawasawa? Uhuru na Mzalendo siyo saizi yangu. Naamini katika fikra huru na halisi. Mimi si bendera fuata upepo.

Acha kujishuku wewe.
Ni nani aliyekuambia Tanzania Daima ni gazeti la Chadema? Unatufanya siye wajinga?
Hivi Tanzania Daima siyo gazeti la Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Kiongozi wa upinzani bungeni? Pinga na hili sema Tanzania Daima ni la Katibu Mkuu wa CCM bosi wako Kinana.
 
Kibanda anajitengenezea mazingira ya kukumbukwa na Kinana. Wana JF ufisadi utatuangamiza kama hawatatokea watu wa kujitoa mhanga.
Sasa ndio muelewe kwamba kufungiwa kwa Mwanahalisi maana yake Wananchi tumezibwa midomo, hawa waliobaki nao wanataka washibe nao ili wavimbiwe, hii nchi kuna vita isiyotalajiwa itatokea tu lazima. watu wamekuwa Wasaliti sana.
 
Hii stor imepandkzwa hajaanda kbanda ni wanamtandao wa knana wameipost kwa jina la kibanda

ITAKUWA KWELI NACHELEA KUAMINI KIBANDA UYU NDO KAWA BWEGEH KIASI IKI, LAKINI NI BUSARA AJE AIKANUSHE MAKALA HII PASUA KICHWA, AU LABDA ELA ZA MAFISADI ZIKIWEMO ZA UYO KINANA ZA PEMBE ZA NDOVU ZLIZOKAMATWa HONGKONG ZNAFANYA KAZI YAKE BARABARA
 
Kimsingi naweza kuichukia makala ya Kibanda kwakuwa inamsifia na kumpa taswira ya kuogopwa mtu ambaye naamini ni mwepesi kama walivyo wenzake wengi kwenye chama chao.

Lakini pia makala hii inatoa tahadhari kwa upinzani kuwa kisidharau uteuzi wa Kinana na kuacha kupanga mikakati kwa kuwa tu upinzani unaamini hana jipya.Hiki ni kitu kizuri kutoka kwenye makala ya Kibanda kwasababu kuendelea kubeza kila kitu kinachofanywa na ccm kujinusuru,kunaweza kusababisha upinzani(chadema) kupumzika na kuamini wameshaizika ccm.Kwenye mapambano kila mbinu ya adui yako unatakiwa kuifanyia kazi hata kama akili yako inaamini ni mbinu ya kijinga tu.

Pia kuna watu wameenda mbali zaidi na kumhusisha mmiliki wa gazeti na kumtaka amfute kazi Kibanda.Mi nafikiri hili sio sahihi kwakuwa Tanzania daima sio mali ya chama chochote.Wala yaandikwayo nalo hayalazimiki kusifia tu chama fulani(hata kama mmiliki ana maslahi na nacho) au kupondea tu chama fulani kwakuwa mmiliki atafurahia! Sitaki magazeti ya vyama kwakuwa yamejaa propaganda ili kuhakikisha survival ya vyama hivyo. Hayana kabisa objectivity. Sitofurahi siku nikiamka na kukuta magazeti ya chadema kama yale ya uhuru na mzalendo.

Kwenye siasa hizi za sasa tunahitaji vyombo huru ili vikemee na visifie pale panapostahili.Hatuhijaji vyombo vinavyosifia tu au vinavyokosoa tu. Katika hili Mbowe ni mfano wa kuigwa kwa kutoingilia kazi ya kukagua habari ya gazeti lake kwani anaamini mmiliki hasa wa gazeti ni mwanajamii mwenyewe.
 
Nimekusoma nivea lakini nikuulize kitu, una uhakika kwamba kibanda amekuwa honesty katika hii makala yake ama anamtumikia kafiri apate mradi wake. Angekuwa honesty kama angekiri tu kwamba ana maslahi na mtu/watu hao.

Ukijitahidi kuunganisha dots utaona ni kwanini kibanda anaandika makala very cheap kama hii. Tafuta uhusiano ama ukaribu/umbali wa Kinana na Lowasa ndipo ujue kilichopo nyuma ya pazia.



Hakuna namna yoyote mtu unaweza kuwa honest kwa kutetea ufisadi na mafisadi. Angekuwa honest angewashambulia wote kwakuwa hakuna fisadi mdogo wala mkubwa.

Huyu ni tu ambaye,akiwa muda wa kazi hufanya kazi,akiwa na muda wa kutafuta hela, hutafuta hela.Huyu jamaa si wakuaminiwa hata kidogo.Nimekaa na ndugu yake aliyenipa principles za huyu jamaa.
 
Nilisoma makala ya Kibanda jana usiku online.Nimejichukia binafsi kwa sababu awali mimi ni mtu niliyekuwa namheshimu sana Kibanda.Lakini kwa makala hii ya leo kwenye Tanzania Daima nimeamini njaa ni mbaya sana.Sikuamini gazeti makini kama Tanzania Daima lingeweza kutoa makala ya kishenzi hivi na kama wataendelea kutoa makala za kijinga hivi tutatangaza rasmi ikususa kununua hili gazeti.Hana hata aibu kumtaja Mbowe ambaye ni bosi wake huko ndani ya makala tena kwa kumkashifu.

Nasikitika na nashangaa Freeman Mbowe kumuacha mchumia tumbo huyo kuwa mhariri mkuu wa gazeti la Kiongozi mkuu wa upinzani nchini.Nasikitika eti Ansbert Ngurumo mzee wa Maswali Magumu kuwa ndiye naibu mhariri akiwa chini ya huyu kipofu asiyeuona ukweli.

Kibanda anadhani hii ni ile miaka ya 1990.Nimuulize huyu kibaraka wa Kinana na CCM Je,kuteuliwa Kinana tayari maisha ya watanzania yamebadilika? Je tayari mishahara ya wafanyakazi imepanda? Je tayari pembejeo za kilimo zimepatikana? Je tayari vijana nchi nzima wamepata ajira? Kwa upofu wa Kibanda anadhani kwa vile yeye ameshapewa bahasha kumsifia Kinana basi ataaminisha kila mtu kumsifia tena bila aibu akilitumia kihuni gazeti la Mwenyekiti wa chama anachokikashifu.

Wito kwa Freeman Mbowe-Muondoe huyu mchumia tumbo kwenye gazeti lako kwa heshima yako na chama unchako,na Ngurumo apewe uhariri Mkuu.Hakika Tunalililia gazeti pendwa MWANAHALISI.
unajuaje pengine ametumwa na mbowe usiwasemee wanasiasa they can change mdawowote mpaka we ukashangaa hawana hay a hawa watu
 
Ni mtu asiyejali au mpuuzi asiyezijua vyema siasa za Tanzania anayeweza na kudharau uteuzi uliofanywa na Rais Kikwete. " Absalom Kibanda"
 
Ni mtu asiyejali au mpuuzi asiyezijua vyema siasa za Tanzania anayeweza na kudharau uteuzi uliofanywa na Rais Kikwete. " Absalom Kibanda"

"Uamsho Bye Bye" Nnape Nnauye
 
Aliyekudanganya kwamba Tanzania Daima ni gazeti la Chadema ni nani? Kumbe unajadili jambo usilolijua sawasawa? Uhuru na Mzalendo siyo saizi yangu. Naamini katika fikra huru na halisi. Mimi si bendera fuata upepo.

Mkuu Kibanda,
Ebu msome Molemo, anasema umemkandia Mbowe ambaye ni tajiri yako na mkuu wa kambi ya upinzani. Anasema ukiendelea na kazi Tanzania Daima watasusia kununua gazeti anataka ufukuzwe kazi.
 
Last edited by a moderator:
Kibanda,
Wewe ni mwandishi makini na mwenye weledi unatisha. Nimepitia makala yako kwa kweli umeandika ukweli mtupu tatizo la Watanzania hawataki kuambiwa ukweli.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Kibanda,
Ebu msome Molemo, anasema umemkandia Mbowe ambaye ni tajiri yako na mkuu wa kambi ya upinzani. Anasema ukiendelea na kazi Tanzania Daima watasusia kununua gazeti anataka ufukuzwe kazi.

Mkuu Ritz mimi nawashairi wana UAMSHO wote kuliko kupoteza Muda wenu kushughulikia Mambo ya CDM ni vyema mkajipanga kuanzisha chama chenu maana CCM haiwataki


"UAMSHO Bye Bye" Nnape Nnauye
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom