Absalom Kibanda: Sasa sitaogopa kitu na sina cha kupoteza, nitafichua kila kitu

Absalom Kibanda: Sasa sitaogopa kitu na sina cha kupoteza, nitafichua kila kitu

Anaogopa kutaja jina la hiyo "taasisi nyeti..." anaogopa kutaja huyo aliyeambiwa ajitahadharishe nae, anaogopa kutaja chochote halafu anatuambia kuanzia sasa atakuwa jasiri, ataandika kila kitu. Ridiculous.

Kwamfano akishataja wewe utafanya nini, ama utamsaidia nini? Labda kuna mahala ambapo yeye anaona akitaja patakuwa na impact. Yani wewe unataka ataje tu, then....
 
Kwamfano akishataja wewe utafanya nini, ama utamsaidia nini? Labda kuna mahala ambapo yeye anaona akitaja patakuwa na impact. Yani wewe unataka ataje tu, then....
Okay, sawa, kama hawezi kutaja kwa sababu "patakuwa na impact," whatever the heck that means, basi asitudanganye kwamba kuanzia leo ataanza kusema vitu bila kuogopa.

Watanzania masikini ya Mungu tuko very gullible, hatuna uwezo wa kupima kitu anachosema mtu, tunabugia tu.

Mtu anakwambia kuanzia leo nitaanza kufichua vitu bila kuogopa. Halafu hapo hapo katika taarifa hiyo hiyo ya kutueleza kwamba ataanza kuwa jasiri anaogopa kutaja taasisi ambayo anadai ilimdhuru. Ain't that some nonsense?
 
Sijamuelewa Kibanda ............ anadai haogopi kitu tena wakati interview nzima inaonyesha uoga wa hali ya juu!!
 
Sijamuelewa Kibanda ............ anadai haogopi kitu tena wakati interview nzima inaonyesha uoga wa hali ya juu!!
Alishindwa hata kusema ni gari ya taasisi gani kubwa ilikuwa imesimama hapo nje ya ukuta wa nyumba yao,sielewi ana hesabu gani anayoipiga.
 
Kibanda mnafiki, kama walivyosema wengine anashindwa nini kutuambia kwamba informer wake toka ofisi ya juu ni nani japo hiyo ofisi tunajua kuwa ni ya DCI Manumba. Anashindwa nini kutambia hiyo gari ya polisi iliyokua imembeba Ludovick ina namba gani mbona Bashe aliitaja? sasa kama kweli mwenyekiti wa Editors forums anaweza kufanyiwa haya na akawa bado muoga hivi hiyo forums yao itaheshimiwa na nani?
 
Chukua LiKE mkuu,watanzania ni waoga sana katika kutanabaisha ukweli ili kupunguza maovu hapa nchini kwetu.Wataendelea kung'olewa kucha/meno mpaka wakome.Uoga sio jambo jema ktk maisha ya kila siku ya mwanadamu.
 
Lakini nimuombe tu aseme kila kitu wakati ni huu kwa maana akificha ni kutengeneza bomu kwa wengine ngoja tuone mpaka mwisho wa kipindi kama atafunguka kwa maana ya kufunguka kwani nafasi ni hii gooooooooo absalom kibanda
Huyu bado mwoga...anasema amefunguka wakati story yake haieleweki. Anamaanisha nini akisema kuna watu wanatumia nguvu sana hili swala la upelelezi lisifanyike? Ni watu gani?
Kibanda, nakupa pole lakini usiwe msiri. Funguka na weka kila kitu hewani. Kama sivyo, unyamaze na ugua pole.
Huwezi ukasema utaweka kila kitu hewani na bado ukawa msiri. Sasa ujasiri upo wapi?
 
Back
Top Bottom