Absalom Kibanda: Sasa sitaogopa kitu na sina cha kupoteza, nitafichua kila kitu

Absalom Kibanda: Sasa sitaogopa kitu na sina cha kupoteza, nitafichua kila kitu

Kibanda kafunguka na ukweli umefichuka...magaidi wabaki uchi!

  1. Amesema yako matukio mengi yalitangulia ya kuwadhuru waandishi wa habari kabla yake yeye.
  2. Amesema wiki mbili kabla ya kutekwa aliwahi kuliona gari la taasisi moja limepaki na kuanza kumfuatilia.
  3. Aliwahi kutahadharishwa na mtu toka taasisi nyeti ya taifa hili kuhusu msimamo wake katika maswala ya taifa.
  4. Amesema viongozi wengi wa serikali wamefanya jitihada kubwa katika kukwepesha ukweli wa yaliyomkuta.
  5. Amesema vyombo vya dola vimetumika katika kupotosha ukweli wa matukio ya aina hiyo.
  6. Amesema amepata faraja kuwa wapo viongozi wa ulinzi wa usalama wastaafu wanafuatilia.
  7. Amedai kama alivyowahi kulialia Pinda kuwa nchini kuna watu wahalifu wenye nguvu zaidi ya dola, hawakamatiki!
Asante sana Absalom Kibanda, kama kawaida ya binadamu wapo wanaosubiri chakula wawekewe mezani na hata baada ya hivyo, walishwe. Wapo pia ambao baada ya kulishwa wanashindwa kutafuna na kumeza, hao kwa kweli na bila kutafuna maneno ni wagonjwa mahututi, miili na akili imepooza!
 
Kwa nchi maskini kama Tanzania kauli za "Tunamuachia Mungu" zimekuwa za kawaida, si kwa watu wa kawaida tu bali hata kwa viongozi wa kisiasa,.. na hata katika matamushi ya kiserikali. Hata raisi anapenda hiyo kauli. hii ni dalili ya kukata tama na "kufikia ukomo wa kufikiri". Hii ni dalili tosha kabisa kuwa kukuwa kwa DEMOKRASIA kutachukua muda mrefu sana! Na hicho ndicho kikwazo kikubwa kwa maendeleo katika nchi yetu!

Ni jukumu la raia wote kuiwajibisha serikali na chama tawala na siyo kuwaachia baadhi ya watu ama taasisi na asasi zisizo za kiserikali. Otherwise..tutaendelea kumwachia Mungu sana!
 
kwani baada ya kile kitu cha mlipuko kwenye mkutano wa chadema Arusha, reaction ya serikali ilikuwa ni nini? Kibanda aache kuuma maneno

Ndiyo maana mh. Mbowe hakuuma maneno. Ukianza kusema 'nitasema', basi umekwisha. Taja, tamka wazi ili wahusika wabaki kuhangaika kuijinasua, na hapo watakuogopa. Kwa sasa Kibanda anawezamalizwa na ikaishia hapo basi. Anatakiwa aonyeshe hasira!
 
Anasema alipolazwa hospitalini nchini Afrika Kusini serikali ilimtuma mtu mmoja kwenda kuona maendeleo yake. Uongozi wa hospitali uliamua kumficha ili kunusuru maisha yake.
 
jamani maumivu ya kung'olewa kucha na meno na kutobolewa jicho bila ganzi si mchezo. Anasema sasa ana ujasiri upi? Anajua fika kuwa wahusika wako juu ya sheria wakimtaka wanampata. Hii nchi jamani!!
 
Baada ya mkasa uliompata na mateso aliyoyapata,ndugu Kibanda amesema hata ogopa chochote Sasa kwasababu hana cha kupoteza ataandika mabaya yote anayoyajua.

kumbe alikuwa anaficha?????hili ndilo tatizo la wanahabari wa tanzania.wanaficha habari muhimu.BADILIKENI SASA.
 
kibanda mungu akupe afya njema uweze kuwa shushua hawa magamba na lameck wao.
 
Waharifu walitumia utaalam katika kujeruhi ili kumuangamiza kibanda.
Anasema matukio mengi yalitangulia ya kuwadhuru waandishi wa habari kabla yake yeye.

Kibanda anasema alipata kutahadharishwa na mtu toka taasisi nyeti ya taifa hili. Aliambiwa jambo ajiangalie wapi na mtu huyo. Aliambiwa awe makini na getini na mahali anapokunywa.

Wiki 2 kabla aliona gari limepaki la taasisi moja na gari lilimfuata

Kibanda anasema viongozi wengi wa serikali wamekuwa na jitihada za kukwepesha ukweli. Amewaomba wanahabari wasonge mbele ushindi utapatikana. Vyombo vya dola vilihusika kupotesha ukweli.

Amekubali hali iliyompata kama chachu ya kusimamia anayoyaamini. Hata alipokuwa anasita sasa hatakuwa mwoga. Mambo mengi alikuwa anayafikiria sana. Lakini kwa sasa amejijua namna alivyo jasiri tofauti na awali. Hali ya afya yake madaktari walimuona ni jasiri.
Anasema lugha za kishabiki ziliandikwa wengine wakiwahusisha wanasiasa.


Ulimwengu anamuuliza kuhusu upelelezi ulipofikia:
Amepata mawasiliano ya viongozi wa vyombo vya dola kuwa wanalifuatilia hata viongozi wa ulinzi wa usalama wastaafu wanafuatilia. Kitu hiki kinampa faraja. Wameliangalia kama maisha binafsi ya kibanda. Kuna afisa wa jamii alitumwa kumhoji afrika kusini.
Alisema wazi kuwa tukio hilo ni la uhalifu na aliamini kuwa aliumizwa kwa sababu ya msimamo wake kwa masuala mbalimbali kitaifa. Lakini pia alitoa ruhusa kwa vyombo vya dola kufuatia maeneo mengine.

Kibanda akiri kuwa kuna watu wananguvu ambao wanashughulika na jambo hili ili ukweli usibainike ndio maana hata leo hakuna hata mmoja amekamatwa.

Hapa naanza kupata kapicha kidogo
1. Mahusiano ya Mwigulu na Rudovick,
2. Mwigulu kusema anaomkanda unaoonyesha Viongozi wa CDM wakipanga mauaji,
3. Siku Kibanda anatekwa naye Rudovick kusingizia katekwa pia.
4. Mwigulu kumtumia Rudovick kumrecord Lwakatare
5. Kukamatwa kwa Lwakatare kuhusishwa na kesi ya kutaka kuteka na kumzuru Denis

Nahitimisha kwa kusema wahusika wameishaanza kuanikwa - Rudovick, Mwigulu, Usalama wa Taifa na vyombo vingine vya usalama Lengo ni kuihusisha CHADEMA na matukio yote haya lakini kwa maneno haya ya Kibanda ukweli unaanza kujulikana na ndo maana CDM wamekaa mbali sana na Rudovick.
 
Haya ... hata akisema mhusika ni Mr ABCD mtafanya nini? Kwa sababu watanzania ni mafundi sana wa maneno lakini utendaji unakuwa sifuri. Wale waliotaka kumuua Dr Ulimboka mbona wanajulikana? Wananchi walifanya nini? Kazi kuangalia kama sinema tu!

Asiwe mwongo!
 
Pengine Kibanda hajui hili hapa: Kwamba vyombo vya dola katika nchi zote duniani hutumia sana uncertainty, suspense, obscurity, gray facts kuchelewesha taarifa; na hilo hufanywa si kwa faida ya Subjects, bali kwa faida ya upande wa Serikali. Angalizo hapo ni haya maneno: uncertainty, Suspense, obscurity, gray facts. Nina mashaka Kibanda kaweka katika mazingira hayo akidhani litamsaidia.

Anaweza akatokea mtu kutoka ofisi fulani akakuambaia subiri kidogo hili jambo linafanyiwa kazi. Lengo ni kupitisha muda yatokee mengine hilo liwe historia. Na Historia mambo yakipitwa sana na wakati, au niseme muda, wakati una desturi ya kupunguza hasira au hata relevance ya jambo.

Uncertainty, Suspense, obscurity, gray facts: Mtu amshauri Kibanda awe mwangalifu na watu
wanaomsubirisha kusema kilicho moyoni. Kwa sababu kama wapo hawana nia njema. They are pushing the problem to him. He should consider pushing the problem to them. Aseme tu anachokijua.

Yaani true !!halafu yeye haogopi kama watu wanamteka akili,na amekili ni watu wakubwa ambao wanaweza hata ingilia upelelezi,my take ni kwamba huu ndo wasaa wa kibanda kumtaja vinginevyo watamuua kwa sababu hawezi na hana uwezo wa kuwatishia(kuwa threat) kwa mtandao kama huo,kwa hilo namshauri aendelee kutembea na ganzi

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Aseme aliye mteka kabla hawajammalizia
 
Washauri wa kisheria hawashauri kumuhudumia victim unless inataka kuonyesha unawajibika. Hata ukimgonga mtu na gari sio wajibu wako kumpatia matibabu. Serikali haiwajibiki kuwatibu waliotekwa unless makosa yalikuwa ya askari wake.
Inasikitisha' serikali hawakugharimikia matibabu,, kazi waliyoifanya ni uchunguzi...je, angepoteza maisha kwa kukosa huduma ya matibabu uchunguzi ungesaidia nini??
 
Kwa nchi maskini kama Tanzania kauli za "Tunamuachia Mungu" zimekuwa za kawaida, si kwa watu wa kawaida tu bali hata kwa viongozi wa kisiasa,.. na hata katika matamushi ya kiserikali. Hata raisi anapenda hiyo kauli. hii ni dalili ya kukata tama na "kufikia ukomo wa kufikiri". Hii ni dalili tosha kabisa kuwa kukuwa kwa DEMOKRASIA kutachukua muda mrefu sana! Na hicho ndicho kikwazo kikubwa kwa maendeleo katika nchi yetu!

Ni jukumu la raia wote kuiwajibisha serikali na chama tawala na siyo kuwaachia baadhi ya watu ama taasisi na asasi zisizo za kiserikali. Otherwise..tutaendelea kumwachia Mungu sana!

Mungu mwenyewe anakuambia jisaidie nami nitakusaidia, sasa wanamwachiaje angali hawajajisaidia kwa njia yoyote?
 
Back
Top Bottom