Absalom Kibanda: Sasa sitaogopa kitu na sina cha kupoteza, nitafichua kila kitu

Absalom Kibanda: Sasa sitaogopa kitu na sina cha kupoteza, nitafichua kila kitu

kibanda anasema kuna siku alishawahi kufuatiliwa na gari la taasisi fulani ya umma lakini pia amesema alishawahi onywa na mtu fulani kutoka serikalini kwamba awe makini. kibanda huyohuyo anasema ooh ninaiachia serikali ifanye uchunguzi wake

huyu jamaa naona kaja na style yake
 
Upelelzi gani hataki kuuharibu hivi kuna upelelezi wa kweli kuliko ukweli atakao usema yeye muathirika? Sidhani lakini kwa vile msifuji mvua imemnyeshea tusubiri na tuone kipi kitafuata au kuunda tume? Mie simo kibanda goo
 
nipo msumbiji leo na huku ndio majanga kwani magamba yanafunika hadi mawasiliano
 
Mvua inakunyeshea badala ya kujitafutia kikingio unamuachia mungu hahahaha yawezekana mgomba kuzaa mahindi muda ni jibu karibu
 
Hivi watu gani hao waliotaka kutumia nguvu kuposha ukweli wa jambo liliompata Kibanda...ambao Kibanda mwenyewe anawasema ?
 
Sijapenda hajafunguka kisawa sawa kaacha ishu pending....!!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kama Dr. Ulimboka angeweka wazi yaliyompata, tendo hili lisingerudia kwa Mh Kibanda. Kauli ya Dr. Ulimboka ya kumwachia Mungu ni UWOGA au USALITI. Basi wale wahisani waliochanga kugharamia matibabu yake nao wangelisema "wanamwachia Mungu" ingekuwaje. M/Mungu anapenda kuwa mkweli na uwazi, sio kufichaficha. Ulimboka ni Adui wa harakati na ni Msaliti kama Mbatia na Lyatonga
 
Anasema gharama za matibabu kipindi anaumwa zilibebwa na kampuni pamoja na jukwaa la wahariri,serikali haukujali

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

kwani baada ya kile kitu cha mlipuko kwenye mkutano wa chadema Arusha, reaction ya serikali ilikuwa ni nini? Kibanda aache kuuma maneno
 
Baada ya mkasa uliompata na mateso aliyoyapata,ndugu Kibanda amesema hata ogopa chochote Sasa kwasababu hana cha kupoteza ataandika mabaya yote anayoyajua.

Hamna sababu ya kutangaza. Yeye angeandika kwanza! Tanzania ni nchi ya maneno. Kila mtu anatishia
 
Tatzo hajafunguka vya kutosha bado anaogopa ogopa ingawa mwenyewe anasema tukio limempa ujasiri haogopi tena ,angetoa ambayo ni maelezo ya direct ili tujuwe kabisa kama ustadhi abdalla au Savimbi ndo wamehusika wakipewa na backup na mdebwedo wao mzee wa upepo

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
there is nothing like NAMWACHIA MUNGU
MUNGU ametupa akili ya kupigania haki zetu wenyewe
Mungu ataachiwa mangapi?
ukiona unadhulumiwa haki yako usiwe mwoga kuidai..
nawapenda wenzetu wazungu,, HAWANA HUU MSEMO NAMWACHIA MUNGU
fight for you own right...awataje hao wahusika
na leo ajiangalie anapoingia home kwake isijekuwa wanamsubiri tena getini
 
Back
Top Bottom