Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Katika hali inayoonyesha usanii mkubwa wa uongozi chini ya Mwenyekiti Mbowe, Aliyewahi kuwa mhariri wa gazeti la Tanzania Daima ndugu Absolom Kibanda, ameongea na Watanzania kupitia katika mtandao wa Clubhouse kuwa Kuna watu ndani ya sekretariat ya CHADEMA walifanya uhuni na kughushi saini ya Katibu mkuu Mnyika na kupeleka majina ya akina mama 19 katika mamlaka za serikali ili wawe wabunge.
Katika maelezo yake, Kibanda alimtetea Katibu Mkuu Mnyika kuwa hahusiki na ishu hiyo ila alizunguukwa na wahuni wachache ndani ya sekretatiat kwenye ishu hiyo.
Ifahamike kuwa miongoni mwa wanaouunda Sekreatariat ya CHADEMA ni manaibu makatibu wakuu wawili wa Bara (Benson Kigaila) na yule wa Zanzibar (Salum Mwalimu). Wote hawa wake/wapenzi wao ni miongoni mwa hao akina mama 19. Hata hivyo Kibanda hakutaja jina la yeyote kati ya hao kuwa ndiyo wanahusika.
Wiki iliyopita ndugu Lissu aliulizwa kuhusu wajumbe hao wa sekretariat kuwa na mke/wapenzi katika wale akina mama 19 walioingia bungeni kimagumashi, kwamba kwa nini wasiwekwe pembeni. Lissu akajibu kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha katiba ya chama. Akasema kuwa kwenye chama mtu haingii kama bibi na bwana, bali kila mtu anaingia yeye kama yeye. Akasema kwa mujibu wa kanuni na katiba ya chama, mtu hawezi kuadhibiwa eti kwa sababu mke/mpenzi wake amekikosea chama.
Watu wanahoji kuwa iweje chini ya uongozi wa Mbowe kunatokea uhuni mkubwa kwenye sekretariat halafu hakuna uchunguzi wala hatua zozote kuchukuliwa? Je, ni reforms zipi Mbowe atazileta kama anashindwa kusafisha sehretariat yake?. Ifahamike kuwa dhamana ya kutengeneza sekretariat iko mikononi mwa Mwenyekiti. Kwa nini hasafishi sekretariat yake?