ACACIA Mining PLC set to close loss-making mine as Tanzania export row deepens

Uzuri wakiondoka hakuna atakae kuja wekeza tena
 
Ndiyo! Inamaana bila huo mchanga kusafirishwa hakuna mgodi?
 
Unajua watu wangapi watakosa ajira na wanafamilia au unashabikia tu? Unadhani ni Arsenal na Man U
Hivi nawewe unafahamu ni pesa kiasi gani zinapotea kila mwaka kwenye huo mchanga? Au mzee unalalamatu.
 
surely another Zimbabwe in the making..
 
Mgodi upo dhahabu zinazopatikana palepale mgodini, pamoja na mchanga ambao ndani kuna madini ni mali ya mwekezaji. Kilichomo kwenye mchanga wanaenda kukitoa huko mbele Europe. Hiyo ni sehemu ya mkataba otherwise waisingechukua mchanga.
 
Tusi tishiane nyau hapa. Kama ilikuwa mchanga tu usio na thamani kubwa kwa nini waondoke. Nina uhakika kama wao walikuwa na haki kwenye hili wange hangaika kwenda mahakamani.
Ukiona wanaondoka hivyo ujue wameshikwa pabaya.
Rais tunaomba wasiondoke mpaka wanetulipa hela zetu.
Eti kuna mtu anasema serekali itapata wapi hela ya kufukia mashimo. Lini na wapi hawa jamaa walisha fukia mashimo baada ya kuchukua madini.
Na wish kumsikia Rais akitoa agizo la kushikiliwa passports zao mpaka vitu vikae sawa.
 
Kati ya makontena ya mchanga na gold inayopatikana pale Acacia (ambapo kuna % ndogo inalipwa ya mapato) ni upande gani hasa Taifa linapoteza ela nyingi?
 
Mgodi upo dhahabu zinazopatikana palepale mgodini, pamoja na mchanga ambao ndani kuna madini ni mali ya mwekezaji. Kilichomo kwenye mchanga wanaenda kukitoa huko mbele Europe. Hiyo ni sehemu ya mkataba otherwise waisingechukua mchanga.
Ni sawa mkataba unaruhusu kubeba mchanga lakini sidhani kama unaruhusu kureport data za uongo!
 
Unaonaje kama ile uchunguzi mwingine huru (unbiased) ukifanywa, wadau wa pande zote mbili (govt na mwekezaji) washiriki kujiridhisha findings, maana Acacia walikataa report ya Tume ya Prezda kwa madai kuna exageration?
 
Your absolute correct and it doesn't need someone to be Rocket enginner to understand simple mathematics.
Simple Matrix
 
Ushaambiwa watu walitumwa wakaishia hoteli wakarudi. Sasa jiulize hapo kilichowagandisha hoteli wasiendelee na safari yao ya kutafuta smelter ya serikali ni nini??
 
Na taarifa isiyoshtua! Bali inafurahisha hadi moyoni. Wasepe
 
So wanataka kutuambia kua ule mchanga (makapi) ndio ulikua wanautegemea kwa kutafuta faida ya kila siku??
Kama ndivyo je dhahabu inayopatikana nayo wanaifanyia nini??
Wafunge tu waondoke wezi hawa, washatuibia sana
Waliowaibia sio wao. Ni wale waliopitisha sheria kwa hati ya dharura na kwenda kusaini mkataba wa uchimbaji hotelini majuu huku wanakunywa wiski.

Mwekezaji anafanya watakacho watawala.
 
Mchanga ungekuwa hauna ziada hawa jamaa wasingelia lia hivi. Pia ungekuta nchi zao ama makampuni yao yameshatoa mkopo Tz ijenge smelter ili waondoke na mzigo safi
 
Waende, wanataka tuwaonee huruma?
Hata watoe chozi la damu, walipe kwanza trillion 286 walizoiba! Halafu inawezekana vipi hayo mabaki ya mchanga ambayo wanasema hayana dhahabu ya kutosha ndio iwatie hasara?

Halafu wanasema mashudu au pumba yana punje kidogo sana (economically not viable), chakushangaza mchozi unawatoka baada ya kuzuia pumba zisitoke kwenda nje ya nchi.
 
Wafungashe na waondoke. Hatutaki wawekezaji wezi na wanyonyaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…