Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
So wanataka kutuambia kua ule mchanga (makapi) ndio ulikua wanautegemea kwa kutafuta faida ya kila siku??
Kama ndivyo je dhahabu inayopatikana nayo wanaifanyia nini??
Wafunge tu waondoke wezi hawa, washatuibia sana
hiyo ni report yakwenu sasahivi tuna report mpya inayoonesya data mpya zaidi kwa kuambiwa kuna madini zaidi...
swali lingine hizo report unazo ziandika wewe umezifanyia uchunguzi wewe au hao acacia? na nizamwaka gani bro?
Mkuu uko sahihi kabisa, kuna comments ukisoma humu unabaki unashangaa, yaani ni aibu. Nimechukua kipande kidogo cha document ya ACACIA kinachoonyesha nchi zinazotuma makinikia zao kwenye smelter moja tu kwani ukiijenga peke yako na kutegemea migodi miwili tu itakua hasara na migodi itafungwa kabla hela yako haijarudi. Yaani mtu anasema wafukuzwe tu kama ni rahisi kiasi hicho.Kwani sisi huwa tunaeleweka basi Mkuu. Ni kushabikia tu vitu kama majuha. Tunashabikia report ya kuwananga ACACIA wakati huohuo hatusomi tafiti nyingine zilizofanywa huko nyuma zinazoonyesha kwamba hatuwezi kumudu uwekezaji wa smelter nchini. Halafu hawa watu wanayoyafanya yote yalipewa baraka zote za serikali hiyohiyo inayolialia leo. Upuuzi mtupu. Binafsi nataka kuona independent analysis ya hasara tunayoambiwa tumeingizwa na hawa ACACIA kabla sija comment zaidi.
Hatuwataki wasije tenaUzuri wakiondoka hakuna atakae kuja wekeza tena
Hii inapaswa kuwa African movement against wanyonyaji. Tuburuzane mahakamani tu ili Dunia ijue Africa inabadilika nowMay 27, 2017 | The Telegraph
Mgodi wa Bulyanhulu huenda ukafungwa kufuatia mfululizo wa hasara baada ya Serikali kusitisha usafirishwaji wa mchanga kwenda nje.
Zuio usafirishaji wa mchanga wa madini kwenda nje ya nchi, lilipelekea bei ya hisa za Kampuni ya ACACIA kutetereka kwenye Soko la Hisa la Uingereza (LSE) na Dar es Salaam (DSE).
=======
Acacia Mining is preparing to close a loss-making mine after a row over exports with the Tanzanian government escalated.
Shares in the FTSE 250 gold miner plunged nearly 40pc last week after a report by the Tanzanian government accused it of under-representing the amount of gold in the concentrate it exports, potentially depriving the country of millions in royalties.
The government said that Acacia’s gold output was 10 times greater than it claimed – a level that would “make it third-biggest gold miner in the world”, the company said.
The findings, published with great fanfare on national TV, mean an export ban on gold concentrate imposed at the start of March is likely to continue indefinitely. Acacia is still able to ship out gold bars, which make up 70pc of its output, but estimates that it is losing $1m (£780,000) in revenue every day.
The company, which is dependent on its three mines in Tanzania, has been stockpiling gold concentrate in the hope of a quick end to the dispute. But it is now preparing to close Bulyanhulu mine to stem mounting losses.
Acacia is dependent on three mines in Tanzania
Around 45pc of Bulyanhulu’s output is gold concentrate, and the losses from stockpiling production cannot be offset by sales of gold bars.
Acacia’s Buzwagi and North Mara mines will remain operational for now.
Some observers suggest that Tanzania’s president, John Magufuli, is trying to force Acacia to fund a new gold-smelting industry, but experts say the country’s output is too small for this to be economically viable.
Acacia is petitioning the government to allow a third party to assess its output.
“We need to defend ourselves,” said a person close to the situation. “The numbers are not believable. We are not guilty of a multi-billion dollar fraud.”
A second government committee is looking at gold concentrate production in Tanzania dating back 15 years - roughly the time-span that Acacia, formerly African Barrick, has been operating there. As Acacia is by far the largest miner in the country, it is thought to be the focus of the probe.
Mgodi wa Bulyanhulu, utafiti wake umefanyika kwa miaka mingi kuanzia miaka ya 1970. STAMICO walifanya wakaishiwa pesa na utaalam. Wakafuata Placedome, wakaja Sutton Resources na baadaye Barrick. Utafiti ndiyo unaowezesha mgodi kuanza kujengwa. Mgodi siyo shamba la mahindi au maharage ambalo mazao yake huweza kubadilika kufuatana na msimu au hali ya hewa. Taarifa zilizopatikana kabla ya kuujenga mgodi ni hizo hizo mpaka leo, na ndiyo zinazoongoza uchimbaji na uchenjuaji.
Taarifa hizo hupatikana baada ya kazi ya muda mrefu iliyohusisha watu wengi wenye ujuzi mbalimbali. Sisi ndiyo tuliofanya utafiti. Nilikuwepo pia miaka ya mwanzo ya uzalishaji. Baadaye niliondoka na kuendelea na kazi hizo hizo ndani na nje ya Tanzania mpaka leo. Alichoandika Mruma na wenzake hakipo katika Ulimwengu huu labda kama ni ugunduzi mpya. Na kama ni ugunduzi mpya basi ungekuwa kwa mgodi mpya siyo huu ambao taarifa zake zinafahamika sana.
At that time Magufuli alikua Mbuge na hata siku moja hakuwahi kutoa hoja kupinga issue za barrickWatu wameiba tangu wakiwa Barric Gold tunakuja kulialia wakiitwa Acacia na all days mliambiwa hawa wanaiba mkajifanya viburi,wako wapi wabunge walioshabikia?
naona malkia ni shangazi yako, hongeraI think is the time government to wake up and resolve the matter
Inawezekana kiwango cha madini hayo kwenye huu mgodi isiwe kama makisio ya findigs yanavyoonesha kutokana na utafiti wa serikali but i keep an open mind kutokana na baadhi ya maswala yaliyogundulika yanayoonesha kwamba kunaweza kuwa na mwanya wa ku temper na mchanga huo.Sielewi mengi kuhusu kemia na utafiti. Pia naweza kuwaza ya kwamba kampuni labda liko tayari kudanganya.
Lakini naona mashaka kuhusu taarifa ya maprofesa. Kama kweli asilimia ya dhahabu ni mara kumi jinsi ilivyotangazwa na kampuni - basi kweli Tanzania ingekuwa kiongozi duniani kwa uzalishaji wa dhahabu. (Sasa Tz inatoa tani 40 za dhahabu kwa mwaka, China mkubwa duniani karibu tani 400/mwaka). Hata wakiweza kuficha dhahabu hapa TZ na kuipeleka nje - soko hili si kubwa vile ya kwamba inaweza kufichwa kwenye soko la dunia. Tofauti ingeonekana - lakini hakuna taarifa ya vyanzo visivyojulikana! na ni soko linalotazamiwa sana na wenye hisa na wawekezaji wanaoshindana kati yao.
(hapa tofauti na soko la almasi ambako inajulikana kuna vyanzo visivyoweza kutajwa "blood diamonds")
Hii inanipa mashaka kuhusu taarifa ya uchunguzi wa makontena. Waongeze wengine wa nje kuthebitisha au kupinga!