Kwenye road design kuna mambo mawili yanazingatiwa.
1. Engineering Design
Inahusisha aina na uwezo wa barabara kubeba idadi/uzito fulani.
Mpaka sasa hivi, hii barabara haijaonesha udhaifu katika hili.
2. Geometric Design
Inahusiana na hali nchi na usalama wa watumiaji.
Kutokana na kutotaka kufuata haya. Watumiaji wanaweza kumlaumu mhandisi (designer). Kwenye Geometric Design ndipo tunapata mahali gani alama gani itumike kumuongoza mtumiaji.
Achilia mbali vilima na mabonde yaliyopo eneo husika, pia ukizingatia kuna alama ya mstari mnyofu kwenye barabara unaoashiria kuwa eneo hilo hauruhusiwi kupita gari la mbele yako. Lakini watumiaji wanadharau.
Swala la msingi sio kumatafuta mchawi wala mlozi. Sisi watumiaji wa vyombo vya moto hatufuati taratibu ya matumizi ya vyombo hivyo.
Utaratibu mzima wa mchakato wa utoaji leseni, uandikishaji wa magari, uthibiti wa magari nk. umekaa vibaya.
Kwa ujumla swala la usafirishaji ni swala nyeti katika kukua kwa uchumi wa nchi. Cha ajabu Tanzania hatuna Wizara ya Usafirishaji. Badala yake tuna wizara ya miundombinu. Swala la Usafirishaji na Miundombinu ni mambo yanayoenda sanjari lakini ni majukumu tofauti. Ndio maana inapotokea ajali kama hii hatujui nani wa kumlaumu.
Kwanza, mtu anaagiza gari, linakaguliwa na TRA na TBS.
Mtu akitafuta leseni, anajaribiwa na polisi anainunua TRA.
Mtu akifanya kosa, anakamatwa na Polisi. Gari likikiuka taratibu linakamatwa na SUMATRA.
Hii ni full confusion na ni swala la kuendekeza ulaji na sio utaratibu muafaka.
Maoni yangu:
Tuwe na wizara ya usafirishaji, itakayokuwa inatoa mwongozo mzima wa masuala ya usafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine ikiwa ni pamoja na kutoa mwongozo wa mchakato mzima wa kupata aina ya watu wa kuendesha vyombo hivyo (Driving License) na kuthibiti aina ya chombo na aina ya mzigo wa kubeba.
Hili linawezekana kama watu hawataweka siasa kwenye maisha ya wenzao. Tuweni wa kweli na tuachane na mambo ya kuwa eti sisi ni taifa changa au masikini. Hizi ni fikra duni zinazoturudisha nyuma kila kuchapo.
Watu wasilete siasa katika mipango ya maendeleo. Tufanye uchunguzi wa kisayansi na watumie majibu yanayopatikana kupangia bajeti na kutekeleza. waachane na ubinafsi. Kila kipindi idara/wizara inaongezewa mafungu lakini hatuoni matokeo ya hizo pesa. Swali huwa zinatumikaje? WIZI MTUPU!
Tanzania unaweza kupiga hatua ila siasa inakushika shati. AAAAGGGHH!