Huu mjadala safi sana. Ila kwa wengi waliojadili hapa, wanafanya makosa yaleyale ya wanasiasa. Hii kitu nitaiandika siku zote. Traffic Engineering ni somo gumu sana na linalohitaji uzoefu wa hali ya juu. Matatizo ya kuvamia hii kazi ya watu huwa ni ajali hizo zisizo na kichwa wala miguu. Kwenye ujenzi, kuna sheria zake ambazo wanasema "structure iwe nzuri, economical na iweze kuhimili mzigo (load) na kazi yake inayotakiwa kufanya".
Kwenye Traffic Engineering, inabidi Wahandisi wafuate matakwa ya watu na akili zao za kufikiri. Kwa kuangalia akili zetu hapa Tanzania, nchi ambayo viongozi na watu wenyewe hatuheshimu sheria, inabidi traffic engineer wajue hii kitu na wanapochora/kujenga barabara basi iwe akilini kuwa sisi tuna tabia hiyo.
Unaweza kupanua barabara na kuziweka kama wengi wanavyodai ila ikija semekana nyumba ya mjomba/wakwe/shangazi nk iko barabarani na inabidi ibomolewe, wewe utakuwa wa kwanza kuja hapa kulia na kuweka picha jinsi ndugu zako walivyonyanyaswa.
Njia ya pili ni KUWALAZIMISHA watumiaji barabara kupunguza mwendo mara wanapofika maeneo kama hayo na ikibidi kupunguza mwendo. Huwa kuna njia nyingi sana za kulazimisha dereva apunguze mwendo kabla hajafika sehemu hii (kwa aliyesomea highway/road design anafahamu). Labda niandike tatu:
1. Kuweka Kamera na warning kibao mapema kuwa kwenye mteremko/kilele cha mlima, kuna kamera inayorekodi kila kitu (hii kwa Tanzania haitasaidia sana).
2. Kuweka/kujenga zig zag (S shape) ya barabara kabla ya kufika eneo hilo ambapo huwafanya madereva wawe macho na kuongeza concentration zao kabla ya kufika eneo la hatari (hii nayo huhitaji eneo kubwa zaidi na inaanza kupandisha bei.
3. Kuharibu kwa makusudi kipande cha barabara mita kadhaa kabla ya kufika eneo la hatari. Hii inaweza pia kufanywa kwa kujenga kabarabara ya mawe au lami na juu kuweka kokoto (zikiwa zimeshikiliwa na lami). Hizi zitafanya dereva akifika hapo, matairi yanaanza kupiga kelele sana kutokana na kuzipitia kokoto/mawe na moja kwa moja inamshutua (inaudhi/kusumbua sana) na kumfanya aamke na kuweka concentration kwenye kuendesha na kuchunga alama za barabarani.
Labda mwisho niseme kuna njia nyingine wanatumia wenzetu, ni kuwa wanaweka vyuma vinavyong'aa nyekundu katikati mwa barabara (lanes), si ndefu sana ila kwa Tanzania inabidi viwe vingi na kila anayedhubutu kuingia upande wa mwenzake, matairi yataipata habari yake yaana hadi unayahurumia na mwenyewe atarudi upande wake. Ila zaidi ya makelele, sidhani kama yanaleta madhara kwenye gari.