Kandambilimbili
R I P
- Nov 11, 2008
- 782
- 40
''a scientific thread'' kwenye jukwaa la siasa!.....
nimeamini MAZOEA YANA TABU
si lazima uchangie au utoe comment kama hauna.
LOUD and CLEAR!Tatizo lako Mwanakijiji uko kama viongozi wa Tanzania mnataka kusikia yale mnayotaka, mkisikia tofauti mnajibaraguza, hiyo nayo ni comment pia.
Hii hapa, http://ajali-traumaclass.blogspot.com/Msaaada tutani mkuu hiyo tovuti mbona siioni kabisa.
Naomba link yake.
sehemu nyingi Tanzania magari yanapishana, milimani, mabondeni, kwenye kona n.k lakini hakuna mahali panapovutia ajali zaidi kama Kibaha why?
wabongo.. tuna kazi!!
na mimi nimeyakuta pale... hasa baada ya ile ajali ya jioni kwenye eneo hilohilo, thanks God hapakuwa na fatalitiesnimesikia madereva wanalalamika kuwa kuna uchawi pale......
sasa naona mchangannyiko wa sayansi ya kisayansi na sayansi y auchawi.....
nimesikia madereva wanalalamika kuwa kuna uchawi pale......
sasa naona mchangannyiko wa sayansi ya kisayansi na sayansi y auchawi.....
hiyo bolded part hiyo ndio tatizo kubwa la waswahili!NI TATIZO KWA MAANA YA TATIZO.we can write and write here kuhusu IRRESPONSIBLE BEHAVIOUR...!tuache tu maanake tutajaza server.Kuna vitu vingi sana muhimu kujadili kama kweli tunataka ufumbuzi au at leat kujua chanzo cha matatizo kwenye eneo hili; i did put one which is the craziest, lakini kwa siku hizi ambazo tunawapa akina Yahya, Mze wa ngurumo au tunaenda kwenye mikondo ya bahari kutafuta nguvu mimi naona tusiisahau, there are alot of believers out there...
Now back to senses;
reasons ni kama zifuatazo
- magari yetu ni mabovu - i am sure mengi ni used befor coming, tumeyatengenezea bodies bila standards, poor maintenance nk
- madereva wetu bado hawana elimu na uelewa wa kutosha kuhusu umuhimu wa uwepo wao barabarani
- Maendeleo yasiyona mipango miji, kusababisha human settlement sehemu na kuleta stress na anxiety kwa madereve hivyo inaongeza possibility ya mistakes
- ubou wa barabara unaoletwa na poor procurement procedures hivyo kutuletea contractors fake!
- Weak enforcement of road safety lawys
- corruption and poverty
- ubutu wa wataalam wetu wa vyuo husika kujihusisha na tatizo na solutions
- bado tuko karne ya nane kwenye infrastructure lakini tunapokea vitu vya karne ya 19
- irresponsible behaviour
Kwenye road design kuna mambo mawili yanazingatiwa.
1. Engineering Design
Inahusisha aina na uwezo wa barabara kubeba idadi/uzito fulani.
Mpaka sasa hivi, hii barabara haijaonesha udhaifu katika hili.
2. Geometric Design
Inahusiana na hali nchi na usalama wa watumiaji.
Kutokana na kutotaka kufuata haya. Watumiaji wanaweza kumlaumu mhandisi (designer). Kwenye Geometric Design ndipo tunapata mahali gani alama gani itumike kumuongoza mtumiaji.
Achilia mbali vilima na mabonde yaliyopo eneo husika, pia ukizingatia kuna alama ya mstari mnyofu kwenye barabara unaoashiria kuwa eneo hilo hauruhusiwi kupita gari la mbele yako. Lakini watumiaji wanadharau.
Swala la msingi sio kumatafuta mchawi wala mlozi. Sisi watumiaji wa vyombo vya moto hatufuati taratibu ya matumizi ya vyombo hivyo.
Utaratibu mzima wa mchakato wa utoaji leseni, uandikishaji wa magari, uthibiti wa magari nk. umekaa vibaya.
Kwa ujumla swala la usafirishaji ni swala nyeti katika kukua kwa uchumi wa nchi. Cha ajabu Tanzania hatuna Wizara ya Usafirishaji. Badala yake tuna wizara ya miundombinu. Swala la Usafirishaji na Miundombinu ni mambo yanayoenda sanjari lakini ni majukumu tofauti. Ndio maana inapotokea ajali kama hii hatujui nani wa kumlaumu.
Kwanza, mtu anaagiza gari, linakaguliwa na TRA na TBS.
Mtu akitafuta leseni, anajaribiwa na polisi anainunua TRA.
Mtu akifanya kosa, anakamatwa na Polisi. Gari likikiuka taratibu linakamatwa na SUMATRA.
Hii ni full confusion na ni swala la kuendekeza ulaji na sio utaratibu muafaka.
Maoni yangu:
Tuwe na wizara ya usafirishaji, itakayokuwa inatoa mwongozo mzima wa masuala ya usafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine ikiwa ni pamoja na kutoa mwongozo wa mchakato mzima wa kupata aina ya watu wa kuendesha vyombo hivyo (Driving License) na kuthibiti aina ya chombo na aina ya mzigo wa kubeba.
Hili linawezekana kama watu hawataweka siasa kwenye maisha ya wenzao. Tuweni wa kweli na tuachane na mambo ya kuwa eti sisi ni taifa changa au masikini. Hizi ni fikra duni zinazoturudisha nyuma kila kuchapo.
Watu wasilete siasa katika mipango ya maendeleo. Tufanye uchunguzi wa kisayansi na watumie majibu yanayopatikana kupangia bajeti na kutekeleza. waachane na ubinafsi. Kila kipindi idara/wizara inaongezewa mafungu lakini hatuoni matokeo ya hizo pesa. Swali huwa zinatumikaje? WIZI MTUPU!
Tanzania unaweza kupiga hatua ila siasa inakushika shati. AAAAGGGHH!
Can somebody articulate why it seems there is some kind of a pattern or a logical explanation of why some of the most grisly accidents have happened in or near Kibaha for many many years now? Is there any scientific reason for these occurrences that our rulers have overlooked?
Kwa sababu siamini kama ni wingi wa magari au ufinyu wa barabara tu unaweza kuelezea ajali hizi. Kuna kitu kinasababisha na nina uhakika siyo cha kishirikiana lazima kuna sababu ya kisayansi ya matukio haya.
Tembeleeni tovuti ya "Bobo" ina picha za ajali mbalimbali za vyombo vya usafiri hasa Bongo.. na mnaweza kupata picha ya jinsi gani kuna mahali kuna tatizo ambalo linaweza kuelezeka kisayansi na kutatulika kwa kiasi kikubwa kisayansi.