SMU
JF-Expert Member
- Feb 14, 2008
- 9,613
- 7,889
sehemu nyingi Tanzania magari yanapishana, milimani, mabondeni, kwenye kona n.k lakini hakuna mahali panapovutia ajali zaidi kama Kibaha why?
Hiki kipande kutoka mlandizi mpaka ubungo kina magari mengi (both ways). Kwa madereva wenye haraka, inakuwa vigumu sana kupata nafasi ya ku overtake bila kukiuka sheria ya usalama barabarani.Fikiria upo nyuma ya malori kama matatu na yanakwenda polepole halafu una haraka zako.
Hivyo bado naamini sababu kubwa ni udogo wa barabara kuweza kukidhi idadi ya magari and offcourse uzembe wa sisi madereva na ukimya wa abiria hata pale wanapoona dereva anakiuka sheria na kuhatarisha maisha yao.
Nimepanda mara kadhaa mabasi yanayokwenda morogoro na hata Arusha. Ukioona madereva wanavyoendesha na kuovertake katika kipande hiki cha barabara kwa hakika hutuwezi kushangaa sana ajali zinazotokea.
Barabara ya Chalinze -Morogoro imetengenezwa vizuri sana. Wamejitahidi kuweka njia ya tatu (kwa sehemu zenye milima) ili kuruhusu madereva ambao wanakwenda taratibu kukaa pembeni.