Accidents at Kibaha: A Scientific Reason?

Accidents at Kibaha: A Scientific Reason?

Pamoja na ufinyu wa barabara, kuna mapepo ya ajali hapo. Ushirikina haukwekepi katika jambo hili. Madreva huamua kuchua maamuzi ambayo kama amepona ukimuuliza kwanini alikuwa anaovateki kwenye kona au mlima anaweza kukupa jibu la ajabu sana.

Mawazo kama haya ndiyo yanafanya tusitoe maamuzi ya kuboresha barabara. Madereva kukimbilia kusema mambo ya ajabu ni njia ya kujilinda na adhabu baada ya kuboronga. Huo ushirikina upo kwa wingi kwenye corrupt countries tu?.

Nakumbuka kuna jamaa alikabidhiwa duka kuuza, ikawa kila siku anaondoka na robo kilo ya sukari, nusu kilo ya mchele. Kufika wakati wa stock taking ikaonekana loss kubwa kweli akakimbilia kusema WANANIIBIA KICHAWI, HASA WAKATI WA KURUDISHA CHENJI TUTAFUTE SANGOMA ATENGENEZA DUKA, AKASHINDA KESI KWA MWENYE DUKA.
 
Kibamba pana bonde lenye daraja na pia barabara imewekwa matuta makubwa pande zote mbili za daraja. Sasa, kwa kujua au kutojua, madereva( ambao ni wazembe) wanaoendesha kwa mwendo kasi (wenye uzoefu wa kuendesha magari wanajua) wanapofika kwenye matuta magari yanaruka na kupoteza mwelekeo.
Sababu nyingine ni ubovu wa magari, madereva wageni kutoijua njia vizuri na tanzania sehemu kubwa ya njia zetu hazina alama za barabarani.
Madereva wengi wanapotoka jijini kuelekea mikoani au nje ya nchi, wakishapita mbezi wanaongeza mwendo ili kufidia muda walioupoteza kwenye foleni na ndipo linaanzia kibamba.
Suluhisho: 1. Mfumo wa utoaji leseni uangaliwe upya 2. Ili kuipunguzia idadi ya magari barabara ya morogoro, barabara ya bagamoyo iboreshwe iweze kupitisha magari yanayoelekea kaskazini, barabara ya nyerere kwenda kisarawe ikaunganishwe na barabara ya morogoro ili iweze kupitisha malori
 
gari halikuwa na "breki" haiwezekani kuwa ni kweli; kwa sababu kama lilikuwa halina breki ndio wakagundua hivyo ilipofika Kibamba? Kwanini isiwe huko ilikoanzia? Yaani huko kote haikusimama? Na breki huwa hazinyofoki tu hivi hivi!
 
suppose lile li-death trap (mfereji) lingekuwa na cover what would have happened?.......nina hakika wahandisi wanaweza kutueleza hali ambavyo ingekuwa............yaani i'm really confused.............hizi geometrics ni ngumu sana au?
 
Can somebody articulate why it seems there is some kind of a pattern or a logical explanation of why some of the most grisly accidents have happened in or near Kibaha for many many years now? Is there any scientific reason for these occurrences that our rulers have overlooked?

Kwa sababu siamini kama ni wingi wa magari au ufinyu wa barabara tu unaweza kuelezea ajali hizi. Kuna kitu kinasababisha na nina uhakika siyo cha kishirikiana lazima kuna sababu ya kisayansi ya matukio haya.

Tembeleeni tovuti ya "Bobo" ina picha za ajali mbalimbali za vyombo vya usafiri hasa Bongo.. na mnaweza kupata picha ya jinsi gani kuna mahali kuna tatizo ambalo linaweza kuelezeka kisayansi na kutatulika kwa kiasi kikubwa kisayansi.
Siku moja niliwahi kumuliza Mama yangu ambaye ni Pastor ni mchungaji na akasema kuwa kuna mashetani ay mapepo saa haya mambo sijui kama ni kweli
 
Je.. tuanzishe kampeni ya kusajili upya madereva wote baadaya kutimiza defensive driving course? Yaani, tuanza moja tena na madereva wetu katika kampeni mpya ya kitaifa kwa sababu ukiondoa hizo ajali za sehemu kama Kibaha kuna hizi ajali ambazo zinatokana na "aggressiveness" ya watu kama kuchomekeana n.k hasa katikati ya jiji na miji.

hili ni wazo zuri.lakini kama kawaida kuna watu watapata ulaji hapo wa kutoa certificate za defensive driving course kwa back door,unakumbuka waliweka sheria leseni hadi certificate ya driving school?iliishia wapi?
 
Wabongo hawachelewi kukuambia kwamba eneo hilo kuna jini..teh teh teh....Nadhani Waziri Kawambwa na wahusika wengine wafanye uchunguzi wa kina ili kugundua tatizo.
 
Mkuu pamoja na kukaa na wazee, naamini bado kuwa barabara hii ni FINYU sana na bajeti ingetengwa ili barabara hii ipanuliwe kuanzia Chalinze! Hapo tutapunguza vifo vingi sana.

Nairobi wameweza kwa kiwango kikubwa kupanua barabara zinazoingia katikati ya Jiji, na mpaka sasa wanaendelea na upanuzi huo, sisi tunashindwa nini? Ni nini priorities za serikali yetu?

Kinachosikitisha, wanaendelea na ujenzi wa vibarabara finyu, na hivi vinatuingiza gharama pia tena kwa kubamizwa bei za kifisadi na makampuni yanayojenga vibarabara hivi uchwara!

Mkuu hilo la wizi liko wazi na litaendelea hadi siko tutakapokuwaserous. Lakini ukisema kutenga fedha zaidi it will be the same old story, fedha ziliztotengwa kwa ajili ya upanuzi zwa baraara zimeibiwa na zinatumika kwenye kampeni. Hiyo ni easy sana kuiba. Lakini naona kulikuwa na haja ya ku-go high tech kudhibiti movement ya magari kwenye maeneo korofi, nadhani it is high time tukianza kutumia benefits za optic fibre kurekebisha mambo.
 
Ni kwa sababu ya combination za milima, mabonde na kona kali ..... madereva wengi hawako makini; wanataka kupita magari mengine sehemu zisizo stahili na vilevile madereva wengi TZ hawa-practice "defensive driving" ... simply put, unapoendesha gari TZ assume kwamba madereva wote waliopo barabarani hawajui kuendesha kwa usalama, isipokuwa wewe tu ... ukifikiri hivyo chances za wewe kupata ajali ni ndogo sana.
 
si lazima uchangie au utoe comment kama hauna.

Mzee Mwanakijiji embu acha upuuzi wako...he has a point.....mimi niliweka swali kuhusu elimu ya John Mnyika kauliza kuhusu Div yake ikahamishiwa kwenye sehemu ya Jukwaa la "Elimu (Education Forum)" sasa kuna ubaya gani Geoff kuuliza?...
Geoff haina haja ya kuomba msamaha hii JF itakufa kwasababu ya mambo na maneno na ubaguzi wa kipuuzii.

SOMETIMES theare some BULLSH*T hapa JF
 
Wakuu, eneo la kuanzia Luguruni mpaka kibaha yenyewe, lina miteremko na milima kama nane hivi, barabara imetengenezwa bila kufuata safety issues, kuna kona kwenye miteremko kama minne hivi, Hata ni mambo ambayo yangeweza kuepukika. kwani waliotengeneza, waliofanya sijui umbembuzi yakinifu hawakuweza hata kutumia chembe ya busara, achilia mbali taaluma walizonazo.

Sawa kuna kona kwenye miteremko, lakini hiyo siyo sababu ya kuwa na ajali, kwa kuwa ukiachilia mbali design ya barabara pia watumia barabara wana wajibu wa kuzuia ajali. kuna maeneo yana barabara nyembamba na kona nyingi kuliko eneo hilo lakini ajali ni kidogo sana au hakuna kabisa. Inawezekana kabisa tatizo ni kotekote, waliodesign na watumiaji,

Hapa kwenye hii thread naona kuna Wanasiasa wapenda sayansi na wanasayansi wafanya siasa!
 
Can somebody articulate why it seems there is some kind of a pattern or a logical explanation of why some of the most grisly accidents have happened in or near Kibaha for many many years now? Is there any scientific reason for these occurrences that our rulers have overlooked?

Kwa sababu siamini kama ni wingi wa magari au ufinyu wa barabara tu unaweza kuelezea ajali hizi. Kuna kitu kinasababisha na nina uhakika siyo cha kishirikiana lazima kuna sababu ya kisayansi ya matukio haya.

Tembeleeni tovuti ya "Bobo" ina picha za ajali mbalimbali za vyombo vya usafiri hasa Bongo.. na mnaweza kupata picha ya jinsi gani kuna mahali kuna tatizo ambalo linaweza kuelezeka kisayansi na kutatulika kwa kiasi kikubwa kisayansi.

Kwanza napenda kuuliza hivi wale Majembe Auctions walipopewa ile Tender sijui ni ya kukagua magari inahusu magari yaliyopo mkoa wa Dar es Salaam tu au nchi nzima?

Je, Majembe Auctions wana utaalamu wa Highway Code? Je, Wizara inayoshughulikia ujenzi wa barabara inafuata sheria zinazohusu barabara? i.e. kuweka alama za barabarani na kuonyesha speed katika sehemu mbali mbali kwa madereva. Kwa mfano kwenye mteremko mkali kuna kuwa na speed ambayo imewekwa dereva aifuate au kwenye kona kali ni speed kiasi gani dereva atumie nk. Je alama za barabarani zinampa guide hata dereva yoyote kwenda kwa mwendo gani (ambaye hajapita hiyo njia nk.) je, serikali ina mpango gani wa kujenga barabara ambazo ni Highway? Wasiseme hakuna fweza mbona wanakomba kila siku? Je, barabara zinazojengwa hivi sasa ni za kiwango gani? (Life span yake kutokana na design etc.?) Je, is that value for money?

Bila kuzingatia hayo hapo juu na mengineyo kila uchwao tutaendelea kulia na ajali, bila kusahau kuwa na kipimo cha kuwathibiti madereva, yaani kama dereva anapata ajali kiasi flani au anaendesha huku amekunywa togwa asipewe leseni milele nk. Lazima kuwe na discipline.
 
Mwisho wa siku mwanakijiji utueleze kwa nini umekuwa mwepesi kuikosesha njia sahihi hii thread? Huoni ungekuwa dereva wa lile lori au kipanya ungesababisha ajali kwa uzembe mdogo tu.

Au kwa kuwa tumefika salama tutulie tu? Kuna abiria wachache wamelamika.


 
Nakubaliana na wewe MKJJ kwa hii scientific approach to solving a nagging problem.
Suala la barabara kati ya DSM na Mlandizi linaanza kuwa na utata kutikana na sababu za kisayansi.

Naleta sababu kama tatu kuu
  1. Barabara ni FINYU SANA na kila maboresho ya barabara hii yana kumbwa na kelele kubwa za fidia toka kwa wananchi, kitu ambacho kinanyima fursa ya hata kuwa na 4 lane 2way highway.Tukumbuke kuwa hiki kipande ndio mlango mkubwa kuliko yote nchini kuingia jijini DSM
  2. TOPOGRAPHY-cheki miinuko na mabonde toka Kimara hadi Mlandizi. Maboresho yote yamekwepa kukata vilima na kujaza mabonde katika juhudi za kukwepa gharama.Sasa hivi kuna vikona vya ajabu na vimiinuko/vimteremko vya kuudhi hasa kwa magari makubwa, bila kuongeza upana wa barabara kama ilivyo Chalinze -Morogoro(3lane,2 way)
  3. Kutokana na kuboreka kwa teknolojia ya magari, mengi yanabeba mizigo mikubwa zaidi na hata madogo yanakwenda spidi kubwa zaidi , hivyo kuongeza uwezekano zaidi wa kuwa na ajali, tena mbaya zaidi.(severity of accidents increase with better roads)
MKJJ ukiondoa masuala ya uzembe wa madereva, gari kupata hitilafu za ghafla kama breki kufeli, ukweli unabakia pale pale kuwa barabara hii kipande cha DSM- Mlandizi sasa hivi kimepitwa na wakati na ni vyema tukaanza kuipanua au kama ambavyo serikali imeanza, kujenga barabara mbadala kama ya Bagamoyo-Msata.
Naomba kutoa hoja!!!!

Mkuu Lole.........good points.......however, nachelea kusema hata kama barabara zetu ni finyu...topography ndio hivyo tena........ninaamini hizi bara bara zinakuwa design kwa standards fulani..............na kwenye design yeyote kitu cha msingi sana ni Safety.................hata kama barabara ni finyu........je hiyo ndio iwe sababu ya kukubali matokeo ya ajali ile.........?
 
naomba kuchangia kidogo,
Kila gari la mizigo au la abiria, lazima lisajiliwe na dereva wake, sio kila dereva anaendesha, kila inapotokea ajali na gari husika iliyosababisha ajali pamoja na dereva bima yake lazima ipande hata kama maradufu,
Kipimo kwa dereva, madereva wengi wa magari ya abiria na mizigo, wanatumia vileo, kuwe na ukaguzi wa umakini wa dereva kwa random, ukitumia kilevi mfano bangi na mirungi hubakia kwenye damu kwa muda wa wiki zaidi ya tatu, na medical test itaonesha kama ulitumia,
Moja ya nchi inayopiga hatua katika kudhibiti rushwa ni China, ukipokea rushwa kama utasalimika ni kifungo cha maisha au kifo, askari wa barabarani wapate adhabu kali wanapothibitika kupokea rushwa,hata kama kufungwa maisha, kwani wao pia huchangia sana kwenye ajali
Utowaji wa leseni za magari ya mizigo, uzingatie uwezo wa barabara, sio strength peke bali upana wa barabara,
Naomba kuwasilisha hayo machache,
 
Kama kumbukumbu zangu zitakua sahihi ajali nyingi miaka ya nyuma zilikua zinatokea morogoro eneo la kuelekea mikese lakini jitahada na marekebisho kaika eneo hilo ilichukuliwa na kupunguza ajali kwa kiasi kikubwa ni pamoja na kuomgeza njia nyingine kwenye miinuko mikali ili kuruhusu magari makubwa yaendayo taratibu.
Pamoja na kutozingatia sheria za matumizi ya barabara , uzembe na makosa ya kibinadamu imekua ndio chanzo kikubwa cha ajali za barabarani lakini pia ukosefu wa alama za barabarani, viwango vya mwendo kasi, na ufinyu wa barabara. Barabara moja tu inayojengwa sasa toka Arusha hadi Namanga ndio itakua imekidhi matakwa ya kimataifa cha upana wa mita saba hivyo basi ipo haja ya lazima ya kuangalia namna ya kuiboresha kama si yote kwa wakati mmoja tuanze na eneo hili la Dar, Kibaha Chalinze na kuangalia upya mfumo wetu wa kutoa liseni za kuendeshea magari vinginevyo ajali za barabarani itabakia kuwa janga la taifa.
 
Asilimia kubwa ya ajali zinasababishwa na ovateki mahali pasipostahili, madereva wengi wanaovateki mahali popote iwe kwenye mlima, kona kali nk...Ajali ya jana ilisababishwa na lori lilikuwa linaovateki likakutana na ile hiace.

Nilikoswa koswa sana na tanker nikiwa natoka Dodoma kuja Dar kwa gari ndogo; niko ninapanda kilima fulani maeneo yale, mara ghafla nikakutana tanker linachomoka directly mbele yangu wakati ninamalizia kilima kile. Namshukuru Mungu, nilipeleka gari mtaloni bila kubiringika hivyo sikupata madhara yoyote na wala gari langu halikupata msukosuko sana. Kilichonishanganza ni kuwa lile tanker lililokuwa linaovateki roli la mizigo na kunisababishia dhahama ile halikusimama wala kuangalia masahibu yaliyonikuta.

Dawa kubwa ni kutenganisha njia za kwenda bara na zile za kuja Dar.


Kuhusu swali lako Mwanakijiji, nadhani hakuna sababu yoyote ya kisayansi kuelezea ajali hizo, ni carelessness na incompetence ya madereva wetu tu. Kungekuwa na sababu ya kisayansi basi magari yote yangekuwa yanapata ajali hizo. Kila ajali inapotokea utakuta kuwa sababu kubwa huwa ni dereva tu.
 
Ajari nyingi zinazotokea Tanzania ni za kisayansi. Kuna vitu vingi sana ambavyo ni vya msingi vinakiukwa na watumiaji wa barabara. Mfano: Ukiendesha gari mida ya alfajiri sana (kama saa 9 - 10 hivi) ukitokuelekea Ubungo kwenda Morogoro utakutana na Magari mengi yamewasha full light na kwa uzoefu wangu nimekuwa sioni kabisa mbele ninapopishana na magari ya jinsi hiyo na mengi huwa ni daladala (hiace) na gari ndogo (taxi kwa jina lililozoeleka). Watumiaji hawa hata kama utawaomba wapunguze taa huwa hawa hitikii maombi yako.

Wataalamu wa masuala ya ujenzi wa barabara, wanajua kuwa wakati wanafanya usanifu na ujenzi kuna vitu wanavyotegemea mtumiaji wa barabara awe anavijua na kuvifuata. Watanzania wengi hatutaki kufuata taratibu hizo. Watu wengi na hasa wanasiasa wetu wanapiga kelele kwa matatizo mengine madogo madogo yasiyo na msingi kama kona mbaya, uchawi, tunaiomba serikali ifanye bur buraa!, serikali mbovu n.k
Elimu ya watumia barabara inatakiwaa sana lakini inatolewa kwa usahihi kabisa na wadau mbalimbali kwani ni elimu ya msingi kabisa katika matumizi ya barabara (basic education) ambayo unaweza kuzaliwa nayo pia (yaani kutumia akili na utashi wako kujua.. mfano siyo lazima ufundishwe kuwa kulipita gari (overtake) kwenye kona usiyoona unaweza kusababisha ajari). Ninaamini kuwa tukiwajibika kwa pamoja na kujari taratibu, kanuni na sheria za matumizi ya barabara ajari hizi zitapungua sana.

Mfano: Ajari ya Hiace na Lori hivi majuzi.... mie naamini kabisa dereva wa Hiace alikuwa ameweka full light ili aone abiria n.k hivyo alijisahau kuhusu usalama wake na abiria wake. Dereva wa lori hakuona njia vizuri na hivyo kumgonga.... siamini kuwa dereva wa lori alikuwa amepitiwa na usingizi kwani alikuwa ni asubuhi sana wakati huo.

Matatizo mengine ni ya teknolojia. Teknolojia inabadilika kwa haraka sana. Sasa hivi kuna magari yanaweza kukimbia spidi ya 250 km/saa n.k wakati miundo mbinu yetu in design speed ya 80 km/h. Mfano kuna eneo linaitwa Machinjioni ukiwa unaelekea Rwanda kabla ya kufika Rusumo. Binafsi niliwahi kueleza chanzo cha ajari katika eneo hilo kwa mkuu wa wilaya ya Ngara, Tanroads mkoa wa Kagera na Naibu waziri (wakati huo Dr. Makongoro ) lakini hakuna aliyenielewa hata mmoja na wakaamua kuweka matuta. Nilishitushwa na uamuzi wao lakini kwa taarifa sahihi ni kuwa vifo vimeongezeka zaidi baada ya kuweka hayo matuta kama nilivyo shauri kitaalam. The problem there is simple and clear.... horizontal curve imeunganishwa na vertical curve bila kuwa na transition curve. Ukiona jinsi magari yanavyoanguka eneo hilo utajua kabisa from basics of physics kuwa ni centrifugal forces ndo inayatoa barabarani.

Teknolojia iliyojenga ile barabara ilikuwa ni ya mwaka 1975 na hivi leo tuko 2010. Wataalamu wetu tulionao wanajua kufanya routine maintenance, periodic maintenance na spot improvement tu lakini hawawezi kuangalia mabadiliko haya ya kiteknolojia na philosophia mpya za ujenzi wa miundo mbinu.
 
Je yawezekana mwendo katika barabara zetu kubwa (highway) ni mdogo sana kwa usalama wa magari na abiria? Mwendo wa 80KM/H ni sawa na na karibu 50MpH. Mwendo huu ni wa pole pole sana. Bila ya shaka unachangiwa vile vile na wembawemba wa barabara. Kijijini ninapoishi mimi mwendo ni 70M/H sawa na 112KM/H kwenye freeways (highways) na maeneo mengi ya miji (nje ya bara bara kuu) ni 45MpH ambayo ni sawa na 70 Km/H.
 
Ajari nyingi zinazotokea Tanzania ni za kisayansi. Kuna vitu vingi sana ambavyo ni vya msingi vinakiukwa na watumiaji wa barabara. Mfano: Ukiendesha gari mida ya alfajiri sana (kama saa 9 - 10 hivi) ukitokuelekea Ubungo kwenda Morogoro utakutana na Magari mengi yamewasha full light na kwa uzoefu wangu nimekuwa sioni kabisa mbele ninapopishana na magari ya jinsi hiyo na mengi huwa ni daladala (hiace) na gari ndogo (taxi kwa jina lililozoeleka). Watumiaji hawa hata kama utawaomba wapunguze taa huwa hawa hitikii maombi yako.

Sasa tunazungumzia Sayansi.. thanks..

Wataalamu wa masuala ya ujenzi wa barabara, wanajua kuwa wakati wanafanya usanifu na ujenzi kuna vitu wanavyotegemea mtumiaji wa barabara awe anavijua na kuvifuata. Watanzania wengi hatutaki kufuata taratibu hizo. Watu wengi na hasa wanasiasa wetu wanapiga kelele kwa matatizo mengine madogo madogo yasiyo na msingi kama kona mbaya, uchawi, tunaiomba serikali ifanye bur buraa!, serikali mbovu n.k

vizuri..

Elimu ya watumia barabara inatakiwaa sana lakini inatolewa kwa usahihi kabisa na wadau mbalimbali kwani ni elimu ya msingi kabisa katika matumizi ya barabara (basic education) ambayo unaweza kuzaliwa nayo pia (yaani kutumia akili na utashi wako kujua.. mfano siyo lazima ufundishwe kuwa kulipita gari (overtake) kwenye kona usiyoona unaweza kusababisha ajari). Ninaamini kuwa tukiwajibika kwa pamoja na kujari taratibu, kanuni na sheria za matumizi ya barabara ajari hizi zitapungua sana.

Nimependa mfano huo. Inawezekana wanaombea kuwa mbele hakuna gari!



Matatizo mengine ni ya teknolojia. Teknolojia inabadilika kwa haraka sana. Sasa hivi kuna magari yanaweza kukimbia spidi ya 250 km/saa n.k wakati miundo mbinu yetu in design speed ya 80 km/h.

Sawasawa nimeligusia hilo hapo juu.. kwa sababu watakapotengeneza hizo flyovers magari yataanza "kuflyover the road!"..
The problem there is simple and clear.... horizontal curve imeunganishwa na vertical curve bila kuwa na transition curve. Ukiona jinsi magari yanavyoanguka eneo hilo utajua kabisa from basics of physics kuwa ni centrifugal forces ndo inayatoa barabarani.

Now this is scientific and rational.. lakini wanaotengeneza vitu hivyo wanafuata siasa au wanafuata sayansi? Kanuni za Mwendo za Newton ni lazima ziheshimiwe.

Teknolojia iliyojenga ile barabara ilikuwa ni ya mwaka 1975 na hivi leo tuko 2010. Wataalamu wetu tulionao wanajua kufanya routine maintenance, periodic maintenance na spot improvement tu lakini hawawezi kuangalia mabadiliko haya ya kiteknolojia na philosophia mpya za ujenzi wa miundo mbinu.

Magafu..ningekuwa na uwezo ningekuomba upitie pale kibaha kuangalia kwa macho ya kisayansi na hata ikibidi vipimo vya kawaida tu. Kwa sababu binafsi naamini siyo shetani, mizimu wala majini yanasababisha ajali. Hypothesis yangu ni kuwa kuna sababu ya kisayansi inayotokana na miundombinu, mazingira na uendeshaji wa magari unasababisha ajali hizo. I just need to prove this or disprove it..
 
Back
Top Bottom