Pamoja na ufinyu wa barabara, kuna mapepo ya ajali hapo. Ushirikina haukwekepi katika jambo hili. Madreva huamua kuchua maamuzi ambayo kama amepona ukimuuliza kwanini alikuwa anaovateki kwenye kona au mlima anaweza kukupa jibu la ajabu sana.
Mawazo kama haya ndiyo yanafanya tusitoe maamuzi ya kuboresha barabara. Madereva kukimbilia kusema mambo ya ajabu ni njia ya kujilinda na adhabu baada ya kuboronga. Huo ushirikina upo kwa wingi kwenye corrupt countries tu?.
Nakumbuka kuna jamaa alikabidhiwa duka kuuza, ikawa kila siku anaondoka na robo kilo ya sukari, nusu kilo ya mchele. Kufika wakati wa stock taking ikaonekana loss kubwa kweli akakimbilia kusema WANANIIBIA KICHAWI, HASA WAKATI WA KURUDISHA CHENJI TUTAFUTE SANGOMA ATENGENEZA DUKA, AKASHINDA KESI KWA MWENYE DUKA.