Account ya Akon yakutwa ipo mil 24 tu kwenye mchakato wa kugawana Mali na mke wake

Mali nyingine ambazo hazipo kwa jina lake mtagawaneje sasa
Mkuu,

Ndiyo maana nikauliza kesi imefunguliwa wapi kwanza tujue jurisdiction ikoje, inafuata jurisprudence gani?

Nimeona hela zimekuwa quoted kwa Euros lakini mke nafikiri ni Mmarekani na ndoa ilifungwa Marekani.

Mfano Marekani, kutegemea na jimbo, mwanamme anaweza kudaiwa kugawana mali zilizochumwa wakati wa ndoa bila kujali hizo mali zimehamishiwa kwa nani. Tena mwanamke akiweza kuonesha mwanamme kahamisha mali ili mwanamke asipate kitu hapo mahakama inakubana zaidi mwanamme.

Majimbo kama New Jersey ukimuacha mke unatakiwa kumlipa alimony aendelee kuishi maisha kama uliyomzoeza wakati wa ndoa, anaendelea kulipwa hivyo mpaka afe au aolewe na mwanamme mwingine.

Kwa hiyo narudi kwenye swali langu.

Kesi ya talaka imefunguliwa wapi?

Jibu la swali hili litatoa muongozo mkubwa kwenye mambo mengine.
 
Hili ni jambo tata kidogo, ila kwa upande wangu nafikiri sheria ipitiwe upya, kwa mwanamke anayevunja ndoa yeye mwenyewe asipate kitu, Ila mwanaume kama ndiye amemuacha mke hapo sasa anahaki ya kudai mali.
 
Wanachama wa Hakimi wamekua na furaha sana na wamekua wanachukua mafundisho kwa umuhimu ...
Ila Kuna mbulula mmoja mchezaji wa NBA alijifanya nunda mwisho wa siku mke kaondoka na bilioni zaidi ya 100 na yeye kubaki na bilioni 2 tu na huku Hana nyumba ...huyu anatakiwa kuja mbele ya kamati kuu ya hakimi's kuelezea alipotea wapi
 
Kesi imefunguliwa wapi?

Inawezekana wakapigana pasu mali nyingine pamoja na spousal support bila kujali ana kiasi gani kwenye akaunti.
Umeambiwa mali nyingine zina jina la mama yake mzazi. Hakuna pasu hapo. Sijui laki sheria za huko zinasemaje kuhusu mume kumilikisha mali kwa mtu mwengine kwa kipindi fulani wakiwa ndani ya ndoa, ikiwa na lengo la kukwepa pasu kwa pasu pindi ndoa inapovunjika
 
Hili ni jambo tata kidogo, ila kwa upande wangu nafikiri sheria ipitiwe upya, kwa mwanamke anayevunja ndoa yeye mwenyewe asipate kitu, Ila mwanaume kama ndiye amemuacha mke hapo sasa anahaki ya kudai mali.
Mwanamke anaweza kuvunja ndoa yeye kwa kupigwa, kutukanwa, kufanyiwa visa kama vyote.

Huoni kuwa hapo kwa pendekezo lako utamnyima nafasi ya kuvunja ndoa yeye na kupeea haki yake?
 
Umeambiwa mali nyingine zina jina la mama yake mzazi. Hakuna pasu hapo. Sijui laki sheria za huko zinasemaje kuhusu mume kumilikisha mali kwa mtu mwengine kwa kipindi fulani wakiwa ndani ya ndoa, ikiwa na lengo la kukwepa pasu kwa pasu pindi ndoa inapovunjika
Sasa unasemaje hakuna pasu hapo wakati hata hujui sheria za huko zinasemaje wala hujui huko ni wapi?
 
Mwanamke anaweza kuvunja ndoa yeye kwa kupigwa, kutukanwa, kufanyiwa visa kama vyote.

Huoni kuwa hapo kwa pendekezo lako utamnyima nafasi ya kuvunja ndoa yeye na kupeea haki yake?
Hayo ni mambo ambayo naamini mnaweza mkakaa mkaongea na mkayamaliza sioni ni kama sababu ya kuvunjua ndoa, sababu pekee ambayo naona inanguvu na jukumu la kuvunja ndoa ni uzinzi pekee, hayo mengine nadhani yanamalizwa tu kwa ushauri wa kuishi vema ndani ya ndoa.
 
Ushajipa mamlaka ya kuamua jambo lipi linavunja ndoa na lipi halivunji.

Mamlaka hayo si yako.

Kumbuka kisheria huna nafasi ya kumpangia mwanamke jambo gani linavunja ndoa na gani halivunji ndoa.
 
Huku si kujipa mamlaka bali ni kuileta sheria katika haki na ukweli, awali ya yote tuangalie sheria ni nini? Sheria ni jambo, jukumu au mipaka ya sehemu flani inayojiweke kwa sababu ya jambo flani, ndio maana nchi zote duniani zinasheria zinazo tofautiana kiutendaji, kwa sababu watungaji ni binadamu wenye mitazamo tofauti na kama binadamu ni lazima kutakuwako na makosa pia, hivyo ukiwa kama kiumbe mwenye akili timamu unahaja ya kupinga au kulekebisha sheria pale ambapo unaona pamekosewa.
 
Ukipanda basi ukamkanyaga mtu, halafu mtu akasema umemkanyaga, hutakiwi kumpangia kusema mbona unalia nimekukanyaga kidogo tu? Tupatane nimekukanyaga kidogo tu.

Yeye ndiye ana haki ya kusema umemkanyaga kidogo au sana.

Sasa hapa mbona unaonekana umemkanyaga mtu halafu hapo hapo unashikikia hujamkanyaga sana?
 
Back
Top Bottom