Acha dhambi na utubu Ufalme wa Mungu umekaribia

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
557
Reaction score
858
“Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia”, Mt 3:2 SUV.

Toba maana yake ni “kugeuka”, kugeuka kutoka katika njia mbaya za uovu na kumgeukia Yesu Kristo, na kwa kupitia yeye, unamgeukia Mungu (Yn 14:1, 6; Mdo 8:22, 26:18).

Uamuzi wa kugeuka kutoka katika dhambi na kugeukia wokovu katika Kristo, unahusisha kumpokea Kristo si tu kama Mwokozi kutoka katika adhabu ya dhambi, bali pia kama Bwana wa maisha ya mtu au maisha yako.

Hivyo, toba inahusisha kubadilisha mabwana wawili, yaani kutoka katika ubwana wa Shetani (Efe 2:2) na kwenda katika ubwana wa Kristo na Neno lake (Mdo 26:18).

Toba ni uamuzi huru kwa upande wa wenye dhambi, unaofanikishwa na neema iwezeshayo ambayo watu hupewa wanaposikia na kuiamini Injili ya Yesu Kristo.

“Mkono wa Bwana ukawa pamoja nao, watu wengi wakaamini, wakamwelekea Bwana”, Mdo 11:21 SUV.

Kutoa maana ya Imani iokoayo kuwa ni kumwamini tu Kristo kama Mwokozi hakutoshelezi kabisa kutokana na madai ya Kristo kuhusiana na toba.

Kutoa maana ya Imani iokoayo katika njia ambayo siyo lazima ihusishe kuachana kabisa na dhambi ni kuharibu vibaya sana mtazamo wa Kibiblia wa ukombozi.

Imani inayohusisha toba mara zote ni sharti la wokovu;

“Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”, Mdo 2:38 SUV.

Toba ilikuwa ni ujumbe wa msingi wa manabii wa Agano la Kale (Mal 3:7; Eze 18:30; Yer 7:3), Yohana Mbatizaji (Mt 3:2), Yesu Kristo (Mt 4:17) na Wakristo wa Agano Jipya (Mdo 2:38; Lk 5:32).

Kuhubiri toba ni lazima kuende sanjari au sambasamba na ujumbe wa Injili (Lk 24:47), tofauti na hapo ujumbe wa injili bado haijakamilika.

Unaposikia unaambiwa tubu na uache dhambi zako ufalme wa Mungu umekaribia usifikiri ni jambo ambalo haliwezi kutokea, unaweza ukajifariji kuwa hizi habari nimeanza kuzisikia siku nyingi sana na sikuona lililotokea, kwanza mshukuru Mungu kukupa uhai hadi sasa na unasoma Makala hii.

Yesu anakuita utoke kwenye maisha ya dhambi uje kwake, utubu dhambi zako zote, utoke katika miliki ya Shetani na kuja kwenye miliki yake, inakuhitaji wewe kuchukua hatua. Usipochukua hatua utaelendelea kuwa mfuasi wake na siku ya mwisho utatupwa jenahamu ya milele pamoja naye.

Na wewe ambaye ulirudi nyuma, yaani ulirudi kumilikiwa na Shetani, unapaswa kutoka huko na kurudi kwa Yesu Kristo, Imani zingine zinaweza kukudanganya upo salama na huna shida Yesu alishakuokoa, hiyo Imani siyo sawa, unapaswa kumrudia Mungu wako na kuacha matendo mabaya.

Yesu yupo tayari kukupokea na kukufanya mtu mpya kabisa katika Kristo, hata ukifa leo unayo matumaini ya kufufuliwa na kuketi pamoja na Bwana Yesu. Amua sasa kumfuata Yesu, uwe salama.

Mwisho, jiunge na group la wasap la kusoma biblia kila siku kwa kufuata mtiririko mzuri, wasiliana nasi kwa wasap namba +255759808081.

Soma neno ukue kiroho

Mungu akubariki sana

Samson Ernest

+255759808081
 
Mtumishi naomba kuuliza, Je Mungu anajua kwamba wewe Samson Ernest utafikia Mbinguni au motoni?
Yeye ameshaweka utaratibu, kumwamini Kristo, yeye ndiye njia ya kweli na uzima wa milele. Huwezi kuingia kwa Baba(Mungu) pasipo yeye. Hilo ndilo linanipa uhakika wa kufika mbinguni au kuingia ufalme wa Mungu.
 
“Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”, Mdo 2:38 SUV

Mkuu we ulibatizwa kama biblia inavyosema hapa au ulibatizwa kwa jina la baba, mwana na roho mtakatifu?
 
Nimebatizwa na nimepokea kipawa cha Roho Mtakatifu
 
“Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”, Mdo 2:38 SUV

Mkuu we ulibatizwa kama biblia inavyosema hapa au ulibatizwa kwa jina la baba, mwana na roho mtakatifu?
Akijibu niambie... Hakuna mtu kwenye biblia ambaye amewahi kubatizwa kwa jina la Baba, Mwana na Roho mtakatifu hakunaaaa.. Yesu alisema hivyo lakini siku 10 baadae Peter baada ya kupokea Roho Mt anasema Tubuni mkabatizwe kwa jina la Yesu Kristo. Naipenda sana Bible vile inavyopiga chengaa.
 
Biblia hajichanganyi, mtu anapobatizwa kwa maji huwa anabatizwa kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.
 
mkuu barikiwa sana kwa kutukumbusha habari hizi...hakika tupo ktk nyakati za mwisho nw mda si mrefu kanisa litanyakuliwa, tuendelee kujitakasa
 
Biblia hajichanganyi, mtu anapobatizwa kwa maji huwa anabatizwa kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.
Hakuna mtu amewahi kubatizwa hivyo kwenye biblia mkuu. Ukiweza kunionyesha mtu yeyote aliyewahi kubatizwa kawa jina la Baba Mwana na Roho mtakatifu kwenye biblia... Nakuja kubatizwa.
 
“Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia”, Mt 3:2 SUV.

Toba maana yake ni “kugeuka”, kugeuka kutoka katika njia mbaya za uovu na kumgeukia Yesu Kristo, na kwa kupitia yeye, unamgeukia Mungu (Yn 14:1, 6; Mdo 8:22, 26:18).

Uamuzi wa kugeuka kutoka katika dhambi na kugeukia wokovu katika Kristo, unahusisha kumpokea Kristo si tu kama Mwokozi kutoka katika adhabu ya dhambi, bali pia kama Bwana wa maisha ya mtu au maisha yako.

Hivyo, toba inahusisha kubadilisha mabwana wawili, yaani kutoka katika ubwana wa Shetani (Efe 2:2) na kwenda katika ubwana wa Kristo na Neno lake (Mdo 26:18).

Toba ni uamuzi huru kwa upande wa wenye dhambi, unaofanikishwa na neema iwezeshayo ambayo watu hupewa wanaposikia na kuiamini Injili ya Yesu Kristo.

“Mkono wa Bwana ukawa pamoja nao, watu wengi wakaamini, wakamwelekea Bwana”, Mdo 11:21 SUV.

Kutoa maana ya Imani iokoayo kuwa ni kumwamini tu Kristo kama Mwokozi hakutoshelezi kabisa kutokana na madai ya Kristo kuhusiana na toba.

Kutoa maana ya Imani iokoayo katika njia ambayo siyo lazima ihusishe kuachana kabisa na dhambi ni kuharibu vibaya sana mtazamo wa Kibiblia wa ukombozi.

Imani inayohusisha toba mara zote ni sharti la wokovu;

“Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”, Mdo 2:38 SUV.

Toba ilikuwa ni ujumbe wa msingi wa manabii wa Agano la Kale (Mal 3:7; Eze 18:30; Yer 7:3), Yohana Mbatizaji (Mt 3:2), Yesu Kristo (Mt 4:17) na Wakristo wa Agano Jipya (Mdo 2:38; Lk 5:32).

Kuhubiri toba ni lazima kuende sanjari au sambasamba na ujumbe wa Injili (Lk 24:47), tofauti na hapo ujumbe wa injili bado haijakamilika.

Unaposikia unaambiwa tubu na uache dhambi zako ufalme wa Mungu umekaribia usifikiri ni jambo ambalo haliwezi kutokea, unaweza ukajifariji kuwa hizi habari nimeanza kuzisikia siku nyingi sana na sikuona lililotokea, kwanza mshukuru Mungu kukupa uhai hadi sasa na unasoma Makala hii.

Yesu anakuita utoke kwenye maisha ya dhambi uje kwake, utubu dhambi zako zote, utoke katika miliki ya Shetani na kuja kwenye miliki yake, inakuhitaji wewe kuchukua hatua. Usipochukua hatua utaelendelea kuwa mfuasi wake na siku ya mwisho utatupwa jenahamu ya milele pamoja naye.

Na wewe ambaye ulirudi nyuma, yaani ulirudi kumilikiwa na Shetani, unapaswa kutoka huko na kurudi kwa Yesu Kristo, Imani zingine zinaweza kukudanganya upo salama na huna shida Yesu alishakuokoa, hiyo Imani siyo sawa, unapaswa kumrudia Mungu wako na kuacha matendo mabaya.

Yesu yupo tayari kukupokea na kukufanya mtu mpya kabisa katika Kristo, hata ukifa leo unayo matumaini ya kufufuliwa na kuketi pamoja na Bwana Yesu. Amua sasa kumfuata Yesu, uwe salama.

Mwisho, jiunge na group la wasap la kusoma biblia kila siku kwa kufuata mtiririko mzuri, wasiliana nasi kwa wasap namba +255759808081.

Soma neno ukue kiroho

Mungu akubariki sana

Samson Ernest

+255759808081
Barikiwa sana kwa somo zuri...
 
Back
Top Bottom