Achana na hizi Tabia mara moja

Achana na hizi Tabia mara moja

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Screenshot_20241121_131621_Google.jpg


Tabia ya kuwa na hasira,hii ni tabia ambayo baadhi yetu tunayo,inaweza kukuondolea kujiamini wewe binafsi,na unaweza kuwafanya watu wawe mbali na wewe

Tabia ya kuwafikiria wengine vibaya,yani huwezi kuwafikiria watu katika mlengo mzuri,wewe hufikiria mabaya tu binadamu wenzako,hayo sio maisha ebu badilika anza sasa kuwafikiria wengine kwa wema zaidi

Tabia ya kuwepo au kupatikana mara kwa mara hii itakupunguzia heshima na hadhi yako,kila ukitakiwa sehemu na wakati wowote wewe upo tu,wakati mwingine ebu adimika kidogo ili uwe wa thamani,ila kuna mambo ya kuadimika kuwa makini,usijifanye adimu kazini kwako utafukuzwa kazi hahaha!

Tabia ya uvivu,kuna watu ni wavivu balaa,yaani hata kufanya usafi chumbani kwake au nyumbani anaona uvivu,ni heri akae na mazingira machafu kuliko kufanya usafi hii ni kutokana na kuwa mvivu

Tabia ya kuwa serious kila mda,utapata presha bure,ndio maana hata majira hubadilika kuna kiangazi,kipupwe,masika na kadhalika,sasa wewe daily uko serious tu! Maisha hayakuumbwa hivyo

Asante kwa kusoma

Ni hayo tu!
 
Back
Top Bottom