Mtunza siri zako
JF-Expert Member
- Apr 11, 2025
- 586
- 975
Tokea usajili wake mwaka 1993 na katika historia ya Tanzania, hakuna chama cha siasa ambacho kimekua kwa kasi bila kurudi nyuma kama chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) mpaka pale Magufuli alipoanza kufinya uhuru wa shughuli zake za kiasiasa ili kukidhoofisha kati ya mwaka 2019 - 2021.
Baadhi ya matokeo ya uchaguzi toka mfumo wa vyama vingi ambayo yalisimamiwa na tume ya uchaguzi kutoka 1995 mpaka 2015.
Pamoja na tume hii ya uchaguzi isiyo huru, CHADEMA iliendelea kukua kwenye kila chaguzi na kubeba majimbo mengi hasa yale muhimu ya mijini kwenye vinyang’anyiro vya ubunge.
Kupitia chaguzi, CHADEMA iliwaibua na kuwaleta bungeni wanasiasa machachari na wa mfano kama Mnyika, Mdee, Waitara mwita, Heche, Wangwe, Lissu, Msigwa, Kubenea, Zitto, Slaa, Selasini, Dr. Mollel, Gekul, Bulaya, Matiko, Chacha Marwa, Silinde, Joseph Haule, Ndesamburo, Nassari, Mbilinyi na wengine wengi.
Kutokana na trend hii ya ukuaji na mafanikio kwenye chaguzi, kwanini msimamo wa chama kwa 2025 umekua siyo kushiriki uchaguzi kwa kishindo na kurudisha uwakilishi bungeni ambapo miswada ya mabadiliko inaweza kupelekwa ili kubadili sheria za uchaguzi?
Lete majibu yenye hoja au yanayoongozwa na takwimu na siyo mihemuko.
Nawasilisha!
Mjumbe wa baraza - Mwanza!

| Mwaka wa Uchaguzi | Idadi ya Wabunge wa CHADEMA | Matokeo ya uchaguzi |
| 1995 | 4 | CHADEMA ilipata viti 4 kati ya 269 katika Bunge la Taifa. |
| 2000 | 5 | Ilipata viti 5 na kuongoza halmashauri za wilaya za Kigoma, Karatu, na Tarime. |
| 2005 | 11 | Freeman Mbowe alipata 5.88% ya kura za urais; chama kilipata viti 11 vya ubunge. |
| 2010 | 48 | Dr. Willibrod Slaa alipata 27.1% ya kura za urais; CHADEMA ikawa chama kikuu cha upinzani. |
| 2015 | 73 | Edward Lowassa alipata 39.97% ya kura za urais; chama kilipata viti 73 vya ubunge na kuendelea kuwa chama kikuu cha upinzani. |