PreGE2025 Achana na mihemuko, lete sababu zenye mashiko kwanini CHADEMA hawashiriki uchaguzi 2025

PreGE2025 Achana na mihemuko, lete sababu zenye mashiko kwanini CHADEMA hawashiriki uchaguzi 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Nimeeleza kwa sababu gani sijaweka hapo juu.

Uongozi wa Magufuli ulidhoofisha na kufinya upinzani bila kujali haki ya kikatiba ya shughuli za vyama vya kisiasa.

Naamini isingekua hivyo, CHADEMA ingekua zaidi kwenye majimbo na chaguzi za serikali ya mitaa 2020.
sasa hilo ndo jawabu la kwanini hali ipo hivi wakati huu.....Kwa kutazama hizo takwimu kwa misingi ya ukuaji kadri muda unavyosonga tunaweza kukadiria kwamba asilimia za urais mfano zinapanda kila baada ya miaka kumi
huwenda tukiweka mpira kati wakaachwa waibe kidogo bado CHADEMA itashinda kwa angalau asilimia 54.

tatizo kwa sasa ni wizi uliozidi na kugeuka unyanganyi ukitazamama na kutekana sioni haja ya kushiriki.
 
Mwaka 2015 chadema ilichukua Arusha yote kuanzia ngazi za chini Alafu ghafla Miaka 5 mbele wakayakosa yote Hii utaielezaje iingie akilini kama ubongo wako ni timamu?

Hata kama chama kingekuwa kimeleta asali na maziwa mlangoni mwa wananchi huwez badilisha upepo ghafla hivyo.
 
JANA NILIKUWA IGOMA, NILIWASIKILIZA SANA VIONGOZI WA CDM,,
HUWEZI AMINI WALIKUWA WANAPGA KAMPENI YA KUCHAGULIWA NA SI KAMPENI YA KUTOSHIRIKI UCHAGUZI...
imgaine heche anasema tutajenga viwanda, tutatoa pensheni kwa kila mtoa mtanzania atakayefka 60+years,tutabadli mfumo wa elimu nk.
sasa nikajiuliza hizi ndo sababu za kutoshiriki uchaguzi?
 
Tokea usajili wake mwaka 1993 na katika historia ya Tanzania, hakuna chama cha siasa ambacho kimekua kwa kasi bila kurudi nyuma kama chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) mpaka pale Magufuli alipoanza kufinya uhuru wa shughuli zake za kiasiasa ili kukidhoofisha kati ya mwaka 2019 - 2021. 

Baadhi ya matokeo ya uchaguzi toka mfumo wa vyama vingi ambayo yalisimamiwa na tume ya uchaguzi kutoka 1995 mpaka 2015.

Mwaka wa UchaguziIdadi ya Wabunge wa CHADEMAMatokeo ya uchaguzi
19954CHADEMA ilipata viti 4 kati ya 269 katika Bunge la Taifa.
20005Ilipata viti 5 na kuongoza halmashauri za wilaya za Kigoma, Karatu, na Tarime.
200511Freeman Mbowe alipata 5.88% ya kura za urais; chama kilipata viti 11 vya ubunge.
201048Dr. Willibrod Slaa alipata 27.1% ya kura za urais; CHADEMA ikawa chama kikuu cha upinzani.
201573Edward Lowassa alipata 39.97% ya kura za urais; chama kilipata viti 73 vya ubunge na kuendelea kuwa chama kikuu cha upinzani.

Pamoja na tume hii ya uchaguzi isiyo huru, CHADEMA iliendelea kukua kwenye kila chaguzi na kubeba majimbo mengi hasa yale muhimu ya mijini kwenye vinyang’a nyiro vya ubunge.

Kupitia chaguzi, CHADEMA iliwaibua na kuwaleta bungeni wanasiasa machachari na wa mfano kama Mnyika, Mdee, Waitara mwita, Heche, Wangwe, Lissu, Msigwa, Kubenea, Zitto, Slaa, Selasini, Dr. Mollel, Gekul, Bulaya, Matiko, Chacha Marwa, Silinde, Joseph Haule, Ndesamburo, Nassari, Mbilinyi na wengine wengi. 

Kutokana na trend hii ya ukuaji na mafanikio kwenye chaguzi, kwanini msimamo wa chama kwa 2025 umekua siyo kushiriki uchaguzi kwa kishindo na kurudisha uwakilishi bungeni ambapo miswada ya mabadiliko inaweza kupelekwa ili kubadili sheria za uchaguzi?

Lete majibu yenye hoja au yanayoongozwa na takwimu na siyo mihemuko. 

Nawasilisha!
Mjumbe wa baraza - Mwanza!
Kushiriki uchaguzi ambao kura za raia haziheshimiwi ni kupoteza pesa(kodi) zetu na muda bure.Matokeo hadi watu wafe au waumie ndiyo yatangazwe huwo ni ujinga wa hali ya juu.Ni heri tuwe kama China ijulikane kuliko kuwapumbaza wananchi na uchaguzi feki.
 
Binafsi 2015 niliona watu wakiweka mawe katika foleni ya kupiga kura....watu walitoka majumbani saa kumi na moja alfajiri...kubeba kichinjio ilikuwa fahari furaha na tabasamu kuwahi kituoni.
Mkutano wa Kimandolu nilisimama juu ya tindiga tunazama katika matope taratibu lakini bado tulisimama kusikiliza viongozi wa ukawa wakisema mabadiliko.
Hatukulazimishwa tulitaka mabadiliko sikua naamini tume lakini niliamini safari hii tupo wengi hata ukiiba hutamaliza....matokeo kutangazwa ilikuwa kama msiba watu kimya na viapo kwamba tusingepiga tena kura.

2020 nlienda kupiga kura na katika familia namaanisha boma zima ni mimi pekee niliyefanya hivyo.......Lakini 2025 hata mimi nasema sitapiga .

je! ni nani atakayeenda? hapa nmeongea uhalisia wa yale nimeyaona kwa miaka 10 wala sio takwimu za kupika...
 
Vi
Unaenda vipi kwenye uchaguzi ambao ccm wameshapanga washindi wao. Kwa nini ukawatoe kafara watu, SI Bora washiriki wenyewe huo UCHAFUZI.
Viti 78 mlivipataje? trend inaonyesha kila uchaguzi viti vya wabunge na madiwani vimekuwa vikiongezeka, leo mnsusiaje uchaguzi?
 
sasa hilo ndo jawabu la kwanini hali ipo hivi wakati huu.....Kwa kutazama hizo takwimu kwa misingi ya ukuaji kadri muda unavyosonga tunaweza kukadiria kwamba asilimia za urais mfano zinapanda kila baada ya miaka kumi
huwenda tukiweka mpira kati wakaachwa waibe kidogo bado CHADEMA itashinda kwa angalau asilimia 54.

tatizo kwa sasa ni wizi uliozidi na kugeuka unyanganyi ukitazamama na kutekana sioni haja ya kushiriki.
Ni kweli wizi na uporaji upo kwenye chaguzi na mimi ni muumini wa katiba mpya ili kupunguza madaraka ya raisi kwenye utawala na kuleta muundo mpya wa tume ya uchaguzi.

Si kweli kwamba tuna hizo namba za kushinda, tulikua close na Lowassa kwa sababu ya nguvu ya moto wa wanasiasa wa CHADEMA kwa wakati huo, pamoja na mamluki aliokuja nao kutoka CCM.

Bado hatujajikita kwenye majimbo ya vijijini na miji midogo ambako kuna wapiga kura wengi. Kutumia ushawishi wa Lissu, huu ulikua mwaka wa kuendeleza ukuaji wa chama kwenye wilaya na majimbo ya pembezoni ambako ndiyo kuna udhaifu maana huku mijini CHADEMA tayari ina ushawishi.

Kama wewe ni mpenzi wa data, nenda kaangalie matokea ya ubunge na udiwani 2015 uone tofauti za matokeo majimboni.
 
Mwaka 2015 chadema ilichukua Arusha yote kuanzia ngazi za chini Alafu ghafla Miaka 5 mbele wakayakosa yote Hii utaielezaje iingie akilini kama ubongo wako ni timamu?

Hata kama chama kingekuwa kimeleta asali na maziwa mlangoni mwa wananchi huwez badilisha upepo ghafla hivyo.
Wizi ulikuwepo sana, ila pia tusisahau migogoro ya ndani kwa ndani, kuhama kwa wabunge wenye ushawishi wa CHADEMA kwenda CCM baada ya kupewa rushwa, kupoteza ushawishi kwa wabunge wa CHADEMA kama Lema na kushindwa chaguzi za ndani etc.
 
Ni kweli wizi na uporaji upo kwenye chaguzi na mimi ni muumini wa katiba mpya ili kupunguza madaraka ya raisi kwenye utawala na kuleta muundo mpya wa tume ya uchaguzi.

Si kweli kwamba tuna hizo namba za kushinda, tulikua close na Lowassa kwa sababu ya nguvu ya moto wa wanasiasa wa CHADEMA kwa wakati huo, pamoja na mamluki aliokuja nao kutoka CCM.

Bado hatujajikita kwenye majimbo ya vijijini na miji midogo ambapokuna wapiga kura wengi. Kutumia ushawishi wa Lissu, huu ulikua mwaka wa kuendeleza ukuaji wa chama kwenye wilaya na majimbo ya pembezoni ambako ndiyo kuna udhaifu maana huku mijini CHADEMA tayari ina ushawishi .

Kama wewe ni mpenzi wa data, nenda kaangalie matokea ya ubunge na udiwani 2015 uone tofauti za matokeo majimboni.
hata hio 2015 CCM waliiba sema walikuw ana aibu kwenye wizi .... ambao kuanzia 2019 hawakuwa na aibu tena

ni kama watu wasiojulikana mara ya kwanza walikuwa anajificha ila kwa sasa wameamua kujiweka wazi na kufisha sura zao tu
 
Mbona jibu umetoa mwenyewe tayari ukirejea 2020, 2024. Unataka majibu kutoka kwa mwenyekiti?
 
Mbona jibu umetoa mwenyewe tayari ukirejea 2020, 2024. Unataka majibu kutoka kwa mwenyekiti?
Sijatoa jibu, nimetoa maelezo ya kwanini sijaweka matokeo ya 2020.
Nasubiri jibu lako mkuu!
 
Ni kweli wizi na uporaji upo kwenye chaguzi na mimi ni muumini wa katiba mpya ili kupunguza madaraka ya raisi kwenye utawala na kuleta muundo mpya wa tume ya uchaguzi.

Si kweli kwamba tuna hizo namba za kushinda, tulikua close na Lowassa kwa sababu ya nguvu ya moto wa wanasiasa wa CHADEMA kwa wakati huo, pamoja na mamluki aliokuja nao kutoka CCM.

Bado hatujajikita kwenye majimbo ya vijijini na miji midogo ambapokuna wapiga kura wengi. Kutumia ushawishi wa Lissu, huu ulikua mwaka wa kuendeleza ukuaji wa chama kwenye wilaya na majimbo ya pembezoni ambako ndiyo kuna udhaifu maana huku mijini CHADEMA tayari ina ushawishi .

Kama wewe ni mpenzi wa data, nenda kaangalie matokea ya ubunge na udiwani 2015 uone tofauti za matokeo majimboni.
Nafkiri kuna mtu alisema kutumia njia ile ile na kila siku unakwama ama kwa hakika utakuwa kichaa...ukuaji kupitia chaguzi wapinzani wameshaona kufikia 2030 nchi itawaponyoka hivyo wamebinya uwanja wa kukua kupitia chaguzi

hiii njia ya sasa ni nzuri kwani inalenga kutoa elimu ya uraia badala ya mabadiliko kupitia bungeni ambako hamna matu ataachia uende...

umma umekubali kuhudhuria darasa la CHADEMA na wanchofanya chadema ni kuwaambia wananchi kwann mmesusa kupiga kura hivyo basi chama kinazungumza lugha moja na wananchi mm sioni tabu hapo
 
Binafsi 2015 niliona watu wakiweka mawe katika foleni ya kupiga kura....watu walitoka majumbani saa kumi na moja alfajiri...kubeba kichinjio ilikuwa fahari furaha na tabasamu kuwahi kituoni.
Mkutano wa Kimandolu nilisimama juu ya tindiga tunazama katika matope taratibu lakini bado tulisimama kusikiliza viongozi wa ukawa wakisema mabadiliko.
Hatukulazimishwa tulitaka mabadiliko sikua naamini tume lakini niliamini safari hii tupo wengi hata ukiiba hutamaliza....matokeo kutangazwa ilikuwa kama msiba watu kimya na viapo kwamba tusingepiga tena kura.

2020 nlienda kupiga kura na katika familia namaanisha boma zima ni mimi pekee niliyefanya hivyo.......Lakini 2025 hata mimi nasema sitapiga .

je! ni nani atakayeenda? hapa nmeongea uhalisia wa yale nimeyaona kwa miaka 10 wala sio takwimu za kupika...
Asante kwa kushare hii experience, ni kweli msukumo wa wananchi kwa sasa uko chini sana.
 
Muondoeni mwenyekiti wa sisiemu kuteua makamishna watashiriki tu, una common sense mkubwa? Kama walishiriki miaka ya nyuma haina maana hawakuona makosa

Wameamua sasa hawataki rekebisheni, muache kuja na maswali ya kitoto hapa, wazee na misharubu yenu!
 
Hoja mbele, mihemuko waachie watoto wa sekondari, mtu mzima wewe!
Mchakato wa mabadiliko ya sheria unaujua, unaanzia wapi?

Mnawaachia masisiemu kufanya machakato wa mabadiliko ya sheria za uchaguzi (ambao kama hufahamu unafanyika bungeni) bila sauti wala kuwa challenged na upinzani (CHADEMA). Watabadili wanavyotaka wao, and then?
 
Back
Top Bottom