The Guitarist
JF-Expert Member
- Jul 18, 2015
- 3,599
- 5,338
sasa hilo ndo jawabu la kwanini hali ipo hivi wakati huu.....Kwa kutazama hizo takwimu kwa misingi ya ukuaji kadri muda unavyosonga tunaweza kukadiria kwamba asilimia za urais mfano zinapanda kila baada ya miaka kumiNimeeleza kwa sababu gani sijaweka hapo juu.
Uongozi wa Magufuli ulidhoofisha na kufinya upinzani bila kujali haki ya kikatiba ya shughuli za vyama vya kisiasa.
Naamini isingekua hivyo, CHADEMA ingekua zaidi kwenye majimbo na chaguzi za serikali ya mitaa 2020.
😅 😅 haa haa inawezekanaUsiniulize ni nani,labda ni wewe mkuu
Kushiriki uchaguzi ambao kura za raia haziheshimiwi ni kupoteza pesa(kodi) zetu na muda bure.Matokeo hadi watu wafe au waumie ndiyo yatangazwe huwo ni ujinga wa hali ya juu.Ni heri tuwe kama China ijulikane kuliko kuwapumbaza wananchi na uchaguzi feki.Tokea usajili wake mwaka 1993 na katika historia ya Tanzania, hakuna chama cha siasa ambacho kimekua kwa kasi bila kurudi nyuma kama chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) mpaka pale Magufuli alipoanza kufinya uhuru wa shughuli zake za kiasiasa ili kukidhoofisha kati ya mwaka 2019 - 2021.
Baadhi ya matokeo ya uchaguzi toka mfumo wa vyama vingi ambayo yalisimamiwa na tume ya uchaguzi kutoka 1995 mpaka 2015.
Mwaka wa Uchaguzi Idadi ya Wabunge wa CHADEMA Matokeo ya uchaguzi 1995 4 CHADEMA ilipata viti 4 kati ya 269 katika Bunge la Taifa. 2000 5 Ilipata viti 5 na kuongoza halmashauri za wilaya za Kigoma, Karatu, na Tarime. 2005 11 Freeman Mbowe alipata 5.88% ya kura za urais; chama kilipata viti 11 vya ubunge. 2010 48 Dr. Willibrod Slaa alipata 27.1% ya kura za urais; CHADEMA ikawa chama kikuu cha upinzani. 2015 73 Edward Lowassa alipata 39.97% ya kura za urais; chama kilipata viti 73 vya ubunge na kuendelea kuwa chama kikuu cha upinzani.
Pamoja na tume hii ya uchaguzi isiyo huru, CHADEMA iliendelea kukua kwenye kila chaguzi na kubeba majimbo mengi hasa yale muhimu ya mijini kwenye vinyang’a nyiro vya ubunge.
Kupitia chaguzi, CHADEMA iliwaibua na kuwaleta bungeni wanasiasa machachari na wa mfano kama Mnyika, Mdee, Waitara mwita, Heche, Wangwe, Lissu, Msigwa, Kubenea, Zitto, Slaa, Selasini, Dr. Mollel, Gekul, Bulaya, Matiko, Chacha Marwa, Silinde, Joseph Haule, Ndesamburo, Nassari, Mbilinyi na wengine wengi.
Kutokana na trend hii ya ukuaji na mafanikio kwenye chaguzi, kwanini msimamo wa chama kwa 2025 umekua siyo kushiriki uchaguzi kwa kishindo na kurudisha uwakilishi bungeni ambapo miswada ya mabadiliko inaweza kupelekwa ili kubadili sheria za uchaguzi?
Lete majibu yenye hoja au yanayoongozwa na takwimu na siyo mihemuko.
Nawasilisha!
Mjumbe wa baraza - Mwanza!
Viti 78 mlivipataje? trend inaonyesha kila uchaguzi viti vya wabunge na madiwani vimekuwa vikiongezeka, leo mnsusiaje uchaguzi?Unaenda vipi kwenye uchaguzi ambao ccm wameshapanga washindi wao. Kwa nini ukawatoe kafara watu, SI Bora washiriki wenyewe huo UCHAFUZI.
Ni kweli wizi na uporaji upo kwenye chaguzi na mimi ni muumini wa katiba mpya ili kupunguza madaraka ya raisi kwenye utawala na kuleta muundo mpya wa tume ya uchaguzi.sasa hilo ndo jawabu la kwanini hali ipo hivi wakati huu.....Kwa kutazama hizo takwimu kwa misingi ya ukuaji kadri muda unavyosonga tunaweza kukadiria kwamba asilimia za urais mfano zinapanda kila baada ya miaka kumi
huwenda tukiweka mpira kati wakaachwa waibe kidogo bado CHADEMA itashinda kwa angalau asilimia 54.
tatizo kwa sasa ni wizi uliozidi na kugeuka unyanganyi ukitazamama na kutekana sioni haja ya kushiriki.
Wizi ulikuwepo sana, ila pia tusisahau migogoro ya ndani kwa ndani, kuhama kwa wabunge wenye ushawishi wa CHADEMA kwenda CCM baada ya kupewa rushwa, kupoteza ushawishi kwa wabunge wa CHADEMA kama Lema na kushindwa chaguzi za ndani etc.Mwaka 2015 chadema ilichukua Arusha yote kuanzia ngazi za chini Alafu ghafla Miaka 5 mbele wakayakosa yote Hii utaielezaje iingie akilini kama ubongo wako ni timamu?
Hata kama chama kingekuwa kimeleta asali na maziwa mlangoni mwa wananchi huwez badilisha upepo ghafla hivyo.
hata hio 2015 CCM waliiba sema walikuw ana aibu kwenye wizi .... ambao kuanzia 2019 hawakuwa na aibu tenaNi kweli wizi na uporaji upo kwenye chaguzi na mimi ni muumini wa katiba mpya ili kupunguza madaraka ya raisi kwenye utawala na kuleta muundo mpya wa tume ya uchaguzi.
Si kweli kwamba tuna hizo namba za kushinda, tulikua close na Lowassa kwa sababu ya nguvu ya moto wa wanasiasa wa CHADEMA kwa wakati huo, pamoja na mamluki aliokuja nao kutoka CCM.
Bado hatujajikita kwenye majimbo ya vijijini na miji midogo ambapokuna wapiga kura wengi. Kutumia ushawishi wa Lissu, huu ulikua mwaka wa kuendeleza ukuaji wa chama kwenye wilaya na majimbo ya pembezoni ambako ndiyo kuna udhaifu maana huku mijini CHADEMA tayari ina ushawishi .
Kama wewe ni mpenzi wa data, nenda kaangalie matokea ya ubunge na udiwani 2015 uone tofauti za matokeo majimboni.
Sijatoa jibu, nimetoa maelezo ya kwanini sijaweka matokeo ya 2020.Mbona jibu umetoa mwenyewe tayari ukirejea 2020, 2024. Unataka majibu kutoka kwa mwenyekiti?
Hayo ndio majibu yenyewe sasa.Siajtoa jibu, nimetoa maelezo ya kwanini sijaweka matokeo ya 2020.
Nasubiri jibu lako mkuu!
Nafkiri kuna mtu alisema kutumia njia ile ile na kila siku unakwama ama kwa hakika utakuwa kichaa...ukuaji kupitia chaguzi wapinzani wameshaona kufikia 2030 nchi itawaponyoka hivyo wamebinya uwanja wa kukua kupitia chaguziNi kweli wizi na uporaji upo kwenye chaguzi na mimi ni muumini wa katiba mpya ili kupunguza madaraka ya raisi kwenye utawala na kuleta muundo mpya wa tume ya uchaguzi.
Si kweli kwamba tuna hizo namba za kushinda, tulikua close na Lowassa kwa sababu ya nguvu ya moto wa wanasiasa wa CHADEMA kwa wakati huo, pamoja na mamluki aliokuja nao kutoka CCM.
Bado hatujajikita kwenye majimbo ya vijijini na miji midogo ambapokuna wapiga kura wengi. Kutumia ushawishi wa Lissu, huu ulikua mwaka wa kuendeleza ukuaji wa chama kwenye wilaya na majimbo ya pembezoni ambako ndiyo kuna udhaifu maana huku mijini CHADEMA tayari ina ushawishi .
Kama wewe ni mpenzi wa data, nenda kaangalie matokea ya ubunge na udiwani 2015 uone tofauti za matokeo majimboni.
Asante kwa kushare hii experience, ni kweli msukumo wa wananchi kwa sasa uko chini sana.Binafsi 2015 niliona watu wakiweka mawe katika foleni ya kupiga kura....watu walitoka majumbani saa kumi na moja alfajiri...kubeba kichinjio ilikuwa fahari furaha na tabasamu kuwahi kituoni.
Mkutano wa Kimandolu nilisimama juu ya tindiga tunazama katika matope taratibu lakini bado tulisimama kusikiliza viongozi wa ukawa wakisema mabadiliko.
Hatukulazimishwa tulitaka mabadiliko sikua naamini tume lakini niliamini safari hii tupo wengi hata ukiiba hutamaliza....matokeo kutangazwa ilikuwa kama msiba watu kimya na viapo kwamba tusingepiga tena kura.
2020 nlienda kupiga kura na katika familia namaanisha boma zima ni mimi pekee niliyefanya hivyo.......Lakini 2025 hata mimi nasema sitapiga .
je! ni nani atakayeenda? hapa nmeongea uhalisia wa yale nimeyaona kwa miaka 10 wala sio takwimu za kupika...
Hoja mbele, mihemuko waachie watoto wa sekondari, mtu mzima wewe!Muondoeni mwenyekiti wa sisiemu kuteua makamishna watashiriki tu, una common sense mkubwa? Kama walishiriki miaka ya nyuma haina maana hawakuona makosa
Wameamua sasa hawataki rekebisheni, muache kuja na maswali ya kitoto hapa, wazee na misharubu yenu!