PreGE2025 Achana na mihemuko, lete sababu zenye mashiko kwanini CHADEMA hawashiriki uchaguzi 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Sawa nawaachia watoto mihemko na mchakato wa mabadiliko leo ndio umeujua? Miaka 30 watu wanasema sheria mbovu mnataka mpewe karne nzima au tusubiri yesu arudi? Lini ccm waliwahi kusema muda unawatosha???

Ok kama masisiemu watafanya watakavyo ndio itakua mara ya kwanza? Walibadili hata mwaka huu, wakibadili kijinga kama tulia alivyowaelekeza na kwa kiburi chake, hawatashiriki tena, shida ipo wapi. Turudi kwenye common sense na common ground mambo yaanze. No reforms no election broda!
 
Mambo ya kushangaza sana
 
Wakati huu itachukua viti,279 Chadema.
 
Serikali ya kikomunist 😂 😂 😂 😅
 
nafkiri hili swala la mageuzi ya sheria zetu hatuaanzi kama vile hatukuwahi anza tukaishia mahali

point hapa tuanzie na rasimu ya jaji warioba
 
nafkiri hili swala la mageuzi ya sheria zetu hatuaanzi kama vile hatukuwahi anza tukaishia mahali

point hapa tuanzie na rasimu ya jaji warioba
Nakubaliana na wewe, ila hayo ni mambo mawili tofauti.

Katiba mpya - lazima tuanzie kwenye rasimu ya jaji warioba
Mabadiliko ya sheria ya uchaguzi - yanaanzia kwenye kuandika mswada wa mabadiliko. Sauti ya CHADEMA bungeni ingeleta taswira na hoja mpya kwenye mchakato.
 
Wewe ni likichwa ligumu eee,wameona mlichokifanya uchaguzi mdogo 2024 ni kama yaliyofanyika kwenye uchaguzi mdogo 2019 na uchaguzi mkubwa 2020

Wakaona kuna uhitaji wa kuwa na reforms
 
Kwamba walikuwa wanashinda na kuongeza idadi ya viti bungeni sidhani kama inahalalisha hali inayoonekana ni kikwazo tu iendelee (kuvumiliwa)
.
Mapungufu lazima ifuke wakati, yarekebishwe. Na ndiyo ambayo si ajabu yangefanyiwa kazi mapema, ushindi wao usingekuwa wa kujivuta kila msimu wa uchaguzi. Si ajabu leo CDM au wengine wangeshakuwa wameshika dola, na hawa waliopo kwenye uongozi kwa sasa, wangekuwa ama wapinzani au wangekistaafisha kama KANU ya Kenya.

kuwa na siha au kutougua kwenye mazingira yasiyofaa, hakuhalalishi kuendelea kukubali hayo mazingira Kwa hoja ya afya njema au kutougua. Unaweza kuyavumilia au kulazimika kuvumilia wa mda, ila lazima kuna siku moja, yeyote anayevumilia atachoka...hasa mwenye kujielewa.
 
After 2015 tuli witness ukiukwaji mkubwa wa sheria za uchaguzi, mamlaka ziliwapiga exile na kuwafanyia vurugu zote.

Kama hali hiyo ilijirudia uchaguzi wa serikali za mitaa, kwa nn waendelee na sheria zilizopo?
 
Nini kilitokea kuanzia 2015 mpaka kufika 2020? na kutokea hapo mpka 2024?
 
After 2015 tuli witness ukiukwaji mkubwa wa sheria za uchaguzi, mamlaka ziliwapiga exile na kuwafanyia vurugu zote.

Kama hali hiyo ilijirudia uchaguzi wa serikali za mitaa, kwa nn waendelee na sheria zilizopo?
Kwahiyo uchaguzi utasusiwa mpaka mamlala zitakapojibadili zenyewe au strategy ni nini? hasa strategy za kubadili sheria za uchaguzi?
 
Kwahiyo uchaguzi utasusiwa mpaka mamlala zitakapojibadili zenyewe au strategy ni nini? hasa strategy za kubadili sheria za uchaguzi?
Mbona wameshaweka wazi? Si walishiriki serikal za mitaa? Nini kiliwakuta?

Strategy ilishatamkwa muda sana :

- Kauli ya "no reforms, no election”, Tume Huru ya Uchaguzi Kabla ya Uchaguzi": Hii imekuwa kauli mbiu kuu ya CHADEMA, wakisisitiza kuwa uchaguzi huru na wa haki hauwezi kufanyika bila mageuzi ya kimsingi ya kikatiba na kisheria, pamoja na kuwa na Tume ya Uchaguzi inayojitegemea kikamilifu. Mkakati huu unalenga kuhamasisha umma na wadau wengine kuunga mkono madai yao ya mageuzi mapana kabla ya kushiriki chaguzi.

- Kukataa Kutambua au Kushiriki Kikamilifu katika Mchakato wa Sheria zilizopitishwa: CHADEMA imekosoa miswada ya sheria za uchaguzi iliyopitishwa hivi karibuni (hasa zile za mwaka 2024), ikisema kuwa hazijumuishi mageuzi ya kweli wanayoyadai na badala yake zinaendeleza udhibiti wa chama tawala katika mchakato wa uchaguzi. Mkakati huu unajumuisha kukataa kusaini nyaraka au kanuni zinazotokana na sheria hizo, kama ilivyotokea walipokataa kusaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi za mwaka 2025.

- Kususia Kusaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi: Kama hatua ya moja kwa moja ya kukataa sheria zilizopo na kusisitiza madai yao ya mageuzi, CHADEMA ilikataa kusaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi za mwaka 2025 zilizotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (INEC). Mkakati huu umesababisha chama hicho kutangazwa kuwa hakitashiriki chaguzi zijazo, hatua ambayo cdm inaonekana kuitumia kama njia ya kuonesha uzito wa madai yao na kuuthibitishia umma kuwa mfumo wa sasa hauna nia ya kuleta uchaguzi huru na haki.

- Kutoa Maoni na Kukosoa Hadharani Miswada ya Sheria: wamekuwa wakitoa maoni yake na kukosoa waziwazi mapungufu katika miswada na sheria za uchaguzi zilizowasilishwa au kupitishwa.

- Kuandaa maandamano: Ingawa taarifa za hivi karibuni zimejikita zaidi kwenye suala la kususia kusaini kanuni, hapo awali CHADEMA ilikuwa na mkakati wa kuandaa maandamano ya amani nchi nzima kushinikiza serikali kuzingatia maoni ya wadau na kufanya mageuzi ya kweli.

Sambamba na kutoa elimu katika mikutano yao ya hadhara kila wanapoenda( hili wanafanikiwa)
 
Nani huyo aliyekua anakubali kutekenywa?
Na mbona kwenye uongozi wake ndiyo hao viongozi wa sasa walikuzwa na kushinda majimbo?
Miaka ya hivi karibuni hali ya ushindani wa kisiasa imebadilika mno na siasa zimebadilika kwa vyama vya upinzani i .e
kushuka kwa uchaguzi huru na haki by 50%;matumizi ya deep state na vyombo vya dola kwenye vyama vya upinzani yameongezeka; ahadi ya fedha na vyeo kwa baadhi ya wapinzani; wizi wa kura, ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi kwa makusudi nk. Haya ni mambo mapya kabisa katika utamaduni wa ushindani wa siasa nchini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…