INTRODUCTION:-
Mpo raia wotee hasa chama langu la KATAA NDOA??
Mmejiandaaje na 23/09 THE REVOLUTION DAY??
BODY:-
Anyway; turudi kwenye mada.
Ukitoa hizi harakati za ""KATAA NDOA"" mimi bana ni msomi, sijui nijiite hivyo??
Ila kifupi nina elimu ya Finance, Economics, and Investment niliyoipatia kwenye Degree na Masters.
Ilikuwa kidogoo niende kusoma PhD duniani huko ila nilighairi na kuamua ""Kutafuta hela kwenye biashara"".
Nakiri wazi ""Napenda hela balaaaa""
Sasa hapa naongea na wale wanaona wao kwao biashara ni risk na kuamua kukimbilia kwenye Passive income.
Ila ndugu zangu hata Active income ""You can make money while sleeping..!!!""
Hivyo msikimbie sanaa biashara.
SCENARIO.
Humu ndani raia huwa wanaongelea sanaa Mutual Fund, ila huongelea mutual fund za taasisi mbili tu
1. 98% Wanaongelea UTT chini ya Wizara ya Fedha
2. 2% Wanaongelea FAIDA FUND chini ya Wizara ya Utumishi kupitia kwa Watumishi Housing.
ila je mnajua kuwa zipo Mutual Fund za Sekta binafsi??
Hizi hapa....
1. Government.
UTT Amins Funds
Faida Fund
2. Private.
Timiza Fund
Sanlam Investment Fund
Alpha Halal Fund
Inuka Money Market Fund
CONCLUSION.
Kwanini uwekeze tu kwenye UTT hizi nyengine umezisoma ukazielewa au UNAZIJUA HATA??
Siku zotee kabla hujaamua kufanya jambo, lisome kwanza halafu lielewe, halafu ndio ufanye maamuzi SAHIHI.
Karibuni kwa maswali kuhusu MUTUAL FUND.
#YNWA
#YANGA_BINGWA
Mkuu umesahau ungetoa na tofauti zake na UTT ambao ndio umeshika hatam.. kwa research ndogo ya haraka nilioifanya kuna Mutual Funds ambazo ni private nyingi na nyingine ndio zimeanza maana yake hazina hata 5 yeas sokoni na wana ofa mfuko mmoja tu sio kama UTT ina mifuko tofauti kutokana na malengo yako
Mfano faida fund ndo wameanza hawana mfuko wa gawio wao ni unakuza mtaji hawa pia ni serikali
Wale halal hawa ndio wapya sana, nafikiri ni kampuni ya Audit wameamua kuja na package moya ya mutual fund sokoni.. Sanlam pia nao kenya wana Mutual Fund kubwa tu, hapa bongo hawajaweka nguvu sana tena sasa hivi sanlam kaamua kuingia ubia na Voda ndio wamekuja na M wekeza
Kwa kifupi uko sahihi kuna MF nyingine sio UTT peke yake.
Kimachofanya watu wakimbilie UTT. Moja ni kuwa kwa miaka Ya karibuni wamekuwa agressive kwenye kujitangaza tofauti na hizo private.. pili wana mtaji wa kuwa na miaka mingi sokoni maana yake mtu anashawishika kirahisi akiangalia history ya mfuko kwa miaka 20 iliopita..
tatu sababu ni serikali maana yake wanapata ensorsement kirahis kutoka serikalini na hata viongoz wakubwa waliopo na wastaafu wako humo mfano Sumaye yuko UTT toka inaanza huko 2004, pengine ana mabilion ya shilingi sasa hivi
Nne custodian wa mfuko nae ni bank ambayo imejipambanua kuwa na faida kubwa miaka Ya karibuni (CRDB) na wao inaonekana wako karibu na serikali sasa hivi kuliko hata NMB wenyewe
Mpaka wamehost infrastructure Bond wakaipa na jina la mheshimiwa na viongoz kibao wa serikalin wananunua
private ila bado hazijashika soko ndio wameanza na wengi hawana mifuko mmoja au miwili na hawatoi gawio la mwezi so kwa anayetaka magawio ya mwez hapata mfaa ila anaetaka kukuza mtaji patamfaa
Pia private hawajitangazi sana yaan kama hujabahatika kuingia kwenye website zao hutowaona popote
Walau hata Faida fund ambao nao ni serikali walipozindua walifanya promo