Achana na UTT, unazijua "Mutual Funds" za sekta binafsi?

Boss piga hesabu zako vizuri.
Inayopanda ni bei ya kipande accumulatively na sio ""each shilling""

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Na wapi wanaweza hizo pesa ni utata pia,
Hapana sio utata.
Kabla hujawekeza unatakiwa kusoma Financial books zao.
private funds nyingi hawasemi ukweli,
Ukweli unapatikana kwenye Financial books.
Mimi pesa yangu Kwa bongo ni bond za serikali tuu, hao default ni almost zero na 25 year bond ni kama 16%, very good money kama hutaki usumbufu, tatizo ni inflation tuu
Kila fund agent ana utamu wake kwa kile ukitakacho.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Inaweza ikawa poa shida inakuja pale ukitaka kuchukua chako mchakato hausumbui ? Au haichukui muda mrefu?
Ni Open ended, kuchukua fedha hawasumbui.
Unauza vipande, unasubiri siku 3 basi unaikuta pesa yako kwenye account.
Ni hekima kuwekeza sehemu ambapo utapata pesa zako kwa urahisi pale utapozihitaji...

RE: 👇👇
Financial market ya bongo inajikongoja, ila kwenye hili takwa lako IPI VIZURI.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Atalia Mtu Muda Wowote Kuanzia Sasa
Tafuta elimu ni bure.
Punguza Upimbi.

Mimi nipo FAIDA FUND, na lengo langu ni kukuza mtaji ili ninunue aset fulani ya kutumika dukani.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Sijajua kulitokea nini ila kuna mtu alikwenda huko kimyakimya baada ya mwaka mmoja akarudi na mikono kichwani
Kakudanganya.
Mikono kichwani specifically hasa, KWENYE NINI??

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Sasa kama faida inalingana kwanini nihame UTT ambako ni salama niende kwa hao wapya?
 
Tafuta elimu ni bure.
Punguza Upimbi.

Mimi nipo FAIDA FUND, na lengo langu ni kukuza mtaji ili ninunue aset fulani ya kutumika dukani.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
Unajua we jamaa mie nakuheshimu sana, alafu mwana Liverpool mwenzangu, ila kwa hili suala sijui kwanini unanikwaza. Sio mara ya kwanza unaongelea Faida Fund, lakini unaishia kuitaja tu. Tukikuuliza ina nini cha ziada kuliko UTT sijawahi kukuona ukijibu. Huu uzi nilijua una madini,lakini umeishia kutaja tu hizo mutual funds, ikiwa ni jambo zuri kuweka awareness huoni kama ingefaa zaidi awareness creation ikifuatana na elimu ya suala husika?
 
Mkuu umesahau ungetoa na tofauti zake na UTT ambao ndio umeshika hatam.. kwa research ndogo ya haraka nilioifanya kuna Mutual Funds ambazo ni private nyingi na nyingine ndio zimeanza maana yake hazina hata 5 yeas sokoni na wana ofa mfuko mmoja tu sio kama UTT ina mifuko tofauti kutokana na malengo yako

Mfano faida fund ndo wameanza hawana mfuko wa gawio wao ni unakuza mtaji hawa pia ni serikali

Wale halal hawa ndio wapya sana, nafikiri ni kampuni ya Audit wameamua kuja na package moya ya mutual fund sokoni.. Sanlam pia nao kenya wana Mutual Fund kubwa tu, hapa bongo hawajaweka nguvu sana tena sasa hivi sanlam kaamua kuingia ubia na Voda ndio wamekuja na M wekeza
Kwa kifupi uko sahihi kuna MF nyingine sio UTT peke yake.

Kimachofanya watu wakimbilie UTT. Moja ni kuwa kwa miaka Ya karibuni wamekuwa agressive kwenye kujitangaza tofauti na hizo private.. pili wana mtaji wa kuwa na miaka mingi sokoni maana yake mtu anashawishika kirahisi akiangalia history ya mfuko kwa miaka 20 iliopita..

tatu sababu ni serikali maana yake wanapata ensorsement kirahis kutoka serikalini na hata viongoz wakubwa waliopo na wastaafu wako humo mfano Sumaye yuko UTT toka inaanza huko 2004, pengine ana mabilion ya shilingi sasa hivi

Nne custodian wa mfuko nae ni bank ambayo imejipambanua kuwa na faida kubwa miaka Ya karibuni (CRDB) na wao inaonekana wako karibu na serikali sasa hivi kuliko hata NMB wenyewe

Mpaka wamehost infrastructure Bond wakaipa na jina la mheshimiwa na viongoz kibao wa serikalin wananunua

private ila bado hazijashika soko ndio wameanza na wengi hawana mifuko mmoja au miwili na hawatoi gawio la mwezi so kwa anayetaka magawio ya mwez hapata mfaa ila anaetaka kukuza mtaji patamfaa

Pia private hawajitangazi sana yaan kama hujabahatika kuingia kwenye website zao hutowaona popote

Walau hata Faida fund ambao nao ni serikali walipozindua walifanya promo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…