Acheni kukejeli simu za watu!

Acheni kukejeli simu za watu!

Samsung ndio simu, hizo infinix and co ni vyombo vya mawasiliano. Aifoni ni showoff.

Ila baba lao ni HUAWEI PURA 70 ULTRA
While nitakubaliana na ww isipokuwa kuwa iphone ni show off nope, moja ya flagship za muda mrefu is just wengi wanao nunua hawajui watumiaje au matumizi sahihi ya iphone
 
Usirudie tena kuweka Samsung na infinix kwenye sentence moja, yaani hizi infinix zinazochemka kama birika ya kahawa ndo unaifananisha na samsung?
Hujakutana na INFINIX daraja la kwanza! Hazitofautiani na SAMSUNG!
Usirudie tena kuweka Samsung na infinix kwenye sentence moja, yaani hizi infinix zinazochemka kama birika ya kahawa ndo unaifananisha na samsung?
Hujakutana na INFINIX daraja la kwanza! Hazitofautiani na SAMSUNG.
 
Muheshimiwa mleta sledi,ni vema ukaelewa hata kwenye usafiri kuna magari na vipando.Kwa mfano,nikitaja volkswagen beetle/veewee na range rover mnyama naamini unajua hapo gari ni lipi na kipando ki-wapi!Vilevile kwenye simu.Zipo simu na visikilizio.Say amen!🙏
Aisee😃
 
Haitakaa itokee infinix iwe sawa na samsung
Wewe unataka tu kutuvunja moyo mashabiki wa NFINIX!

Mbona INFINIX yangu ni nzuri sana? Tena huwa nikienda nayo kijijini...🤣🤣🤣
 
Maisha ni magumu sana ukiji
Hivi kumbe kipimo cha kuwa una HeLa ni kumiliki simu ya samsung Leo ndo ni mejua
Maisha ni Magumu endapo utajilinganisha na mtu mwingine, vitu vinatengenezwa kulingana na hela yako sasa kwa nini mtu alalamike kutomiliki kitu kizuri? Akubali tu kuwa uwezo umeishia hapo na ajikubali
 
Samsung ni simu, na Infinix ni simu!

Kama ni gharama, zote ni za gharama. Hakuna inayotolewa bure.

Isitoshe, Infinix inatunza sana chaji!

Wanaowakejeli wanomiliki simu za INFINIX, TECNO na ITEL waache hiyo tabia mara moja. Hawajui jinsi wahusika walivyohenyeka kuzipata.
Watuache kabisa team itel🤣
 
Samsung ni simu, na Infinix ni simu!

Kama ni gharama, zote ni za gharama. Hakuna inayotolewa bure.

Isitoshe, Infinix inatunza sana chaji!

Wanaowakejeli wanomiliki simu za INFINIX, TECNO na ITEL waache hiyo tabia mara moja. Hawajui jinsi wahusika walivyohenyeka kuzipata.
Uko sahihi ndugu. Waache dharau. Wa Infinix kainunia kulingana na kipato chake. Huyo mwenye kipato kikubwa amekipata kwa rehma za Mungu sawa na sisi wenye kidogo. Mtoaji ni mmoja na akiamua kumnyang'anya mtu hashindwi!!
 
Watuache kabisa team itel🤣
Mimi isingelikuwa masuala ya mawasiliano kwa mtandao (internet) na kutunza documents, hata simu janja nisingezimiliki. Simu yangu ya kwanza kuimiliki ilikuwa ni PHILIPS, watu wakanitania sana kuwa ni mche wa sabuni lakini sikujali. Kisha nikaenda SIEMENS, halafu NOKIA ya tochi.

Nilipogundua faida za SMART, nikaaanza na TECNO, ikaja ITEL, kisha INFINIX, ikifuatiwa na ...

Na zote hizo zilikuwa ni simu nzuri kwangu kwa sababu zilitimiza ipasavyo majukumu niliyoziagiza.
 
Ifinix,,, Tecno na itel simu za wapiga picha vijijini huko haswaa kwenye Sherehe za jando,,NDOA na makongamano ya Kwaya wakati wa mavuno yako poa haswa Dodoma na ukanda wa majirani zake wa karibu
 
Hivi kumbe kipimo cha kuwa una HeLa ni kumiliki simu ya samsung Leo ndo ni mejua
Siyo kweli mkuu. Ni utaishi tu wa mtu! Huwezi kununua kitu usichokihitaji kwa vile tu una hela! Mbona inasemekana Putin hana simu janja?
 
Back
Top Bottom