Acheni kutumia vitunguu saumu kama dawa ya kukata harufu mdomoni pigeni mswaki

Acheni kutumia vitunguu saumu kama dawa ya kukata harufu mdomoni pigeni mswaki

kwakutumia mswaki laini ulopakwa dawa ya meno ya kutosha, pangusa au sugua ulimi wako taratibu mara kadhaa, sugua meno ya mbele kwa ndani na nje, zamisha mswaki taratibu kwenye magego yaani meno makubwa ya ndani sugua taratibu juu na chini. Fanya hivyo mara mbili ikiwa mdomo wako unatoa harufu kali zaidi kwa muda wa chini ya masaa6 tangu uswaki.

Usiogope kutokwa damu kwa mara ya kwanza, hiyo damu inayotoka ilikua ni hifadhi ya uchafu wa kinywa na meno yako. Baadae haitatoka tena.

Rudia kuswaki hata mara 3 ikiwa mdomo wako unazalisha harufu kali chini ya masaa6 baada ya kuswaki.

Safisha pua kila asubuh, huna haja kuweka sabuni, tumia tu maji safi, ziba pua moja fanya kama unapenga kamasi kuondoa harufu na uvundo ulozalishwa na mipua yako usiku ulipokua unakoroma.
Ukiacha kufanya hivyo ukipiga chafya kwenye kundi la watu utatoa harufu kali sana kutoka puani mwako itakayokera watakao kua karibu yako.

Tumia pamba au kifaa chochote kitakachokuwezesha kuondoa uchafu maskioni, kama utagundua, unapopeana hug na mtu mume au mtu mke unaweza kukutana na harufu kali ambayo mara nyingi hutokea maskioni kwa mtu mwenye maskio machafu. Hasa wanasuka nywele ambao hunawa uso tu kwa muda mrefu. Hawa hutoa harufu kali na mbaya sana ya nywele zilizovunda na maskio machafu.

Hitimisho,
Hakikisha unaswaki vizur zaidi ya mara moja walau kila asubuh, unasafisha pua vizuri kila asubuh na unasafisha maskio yako vizuri kuepuka kuwa kero kwa watakao kua karibu nawe au utakao wasogelea.
Umesema vyema
 
Mchana huu nimetafuna vitunguu maji, kisha nikatafuna vitunguu saumu, ni vichungu balaa huo muwasho pilipili ikasome. Ishu ikawa mdomo kunuka vibaya, ikabidi nikanunue pipi ili kutoa harufu mbaya mdomoni.
 
Kuna siku tulikunywa muarobaini kikombe cha chai, mwili mzima ukawa unatoa jasho linanuka muarobaini
 
Mchana huu nimetafuna vitunguu maji, kisha nikatafuna vitunguu saumu, ni vichungu balaa huo muwasho pilipili ikasome. Ishu ikawa mdomo kunuka vibaya, ikabidi nikanunue pipi ili kutoa harufu mbaya mdomoni.
Ahahahaha izo mambo waachie waziefu mzee😂😂😂
Moisemusajiografii wewe ujajaribu?
 
Ase kutafuna kitungu ni ngumu sana
Ni kazi rahisi.Chagua muda mzuri uliotulia na una uhakika hautotoka nyumbani si chini ya masaa zaidi ya manne.Au,ukishindwa kuvitumia vyenyewe pekee,pendelea vilivyofanywa viungo tu katika vyakula tu.Hivyo huwa vimepunguzwa ukali wa harufu.Ni kama kwenye kachumbari,pilau,nyama nk.
 
Mh bado ujanishaur
 
Tumia vitunguu Swaumu na mtindi..
Na isitoshe vitunguu Swaumu ni km Antibiotic pia,lakini pia inatibu nguvu za kiume pia..
 
Back
Top Bottom