Acheni wakulima wauze mahindi kwa wateja kwa bei ya soko

Huihui2

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
7,021
Reaction score
11,475
Waziri Hussein Bashe alikuwa na msimamo mzuri kuanzia alipoteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo kuhusu kufungua mipaka kwa wageni kuja kununua mazao ya kilimo nchini.

Hii ilikuwa ni furaha kwa wakulima wetu, lakini miezi kama 6 tu iliyopita kwa kelele za Watanzania wavivu wakaiyumbisha Serikali mpaka ikaamua kudhibiti biashara ya mahindi.

Angalia kinachoendelea leo kwenye kichwa cha habari cha gazeti la Mwananchi.

20231016_073156.jpg
 
Waziri Hussein Bashe alikuwa na msimamo mzuri kuanzia alipoteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo kuhusu kufungua mipaka kwa wageni kuja kununua mazao ya kilimo nchini. Hii ilikuwa ni furaha kwa wakulima wetu. LAKINI miezi kama 6 tu iliyopita kwa kelele za Watanzania WAVIVU wakaiyumbisha Serikali mpaka ikaamua kudhibiti biashara ya mahindi. Angalia kinachoendelea leo kwenye kichwa cha habari cha gazeti la MwananchiView attachment 2783448
We nae ni punguani,wakati Serikali inanunua ndio bei ilikuwa kubwa.

Sasa mwaka huu uzalishaji ni mkubwa, Serikali ilinunua Tani 350,000 lakini Bado Kuna Tani iddle kama 400,000 ambazo sio mfanyabiashara Wala nani ananunua.

Mbaya zaidi Kenya wameivisha na wakazuia kuingiza mahindi kwao wakulima hawana pa Kupeleka hiyo ziada na msimu wa Kilimo umefika hivyo Serikali imesema mwisho wa mwezi huu itaanza kununua tena.

Bei Bado ni kubwa ila mahindi hayatoki bei Iko kwenye 70,000-80,000 lakini hakuna wanunuzi ,Sasa hii sio bei ya soko? Mahindi hata yakiuzwa 55,000 kama yanatoka inamlipa mkulima.

Hakuna awamu ambapo wakulima wamepata faida ya Kilimo kama awamu ya mama na wanamshukuru Kwa Hilo na Serikali haijazuia popote.

Mwisho kama kweli kutakuwa na El nino lazima Serikali itanunua maana mwaka utakoafuata utakuwa na uzalishaji mdogo hivyo chakula Cha njaa kitatakiwa.
 
Option ni waache soko liamue, na mipaka isifungwe, anaetaka kuuza china auze, anaetaka kuuza kenya auze tu
Wapi mpaka umefungwa? Kwani hata Sasa soko haliamui bei? Saizi hakuna wanunuzi maana hata majirani Wana mahindi na wamezuia mahindi kuingia.

Na.kwa.taarufa Yako Serikali imenunua gunia Kwa 80,000-90,000 baada ya kuacha kununua ndio beinzimepungua Hadi 70,000 Hadi 60,000 huko Ruvuma na mazao hapo Bado.
 
Njaa kuu inakuja ULIMWENGUNI, Serikali iongeze uwezo wake wa kupanua maghala na kutunza chakula.

Pia ni vizuri mahindi yakageuzwa kuwa unga na kuwa packed Ile kukaa muda mrefu.

Tunakoelekea, biashara kubwa itakuwa chakula.

Upanga tauni na majanga vinaenda kuipiga Dunia.

Serikali chini ya Bashe ni sikivu katika suala Zima la kununua chakula na kutunza.

Wabarikiwe.

Amen
 
Bashe mwenyewe amegeuka mnunuzi wa mahindi
Hili ndiyo kosa kubwa sana serikali ya Samia imetufanyia sisi wakulima. Bashe tulikuwa tunamwelewa sana. Wakulima tulikuwa na vicheko, tuliobahatika tuliuza kidogo mahindi huko huko shambani wakenya walitufuata tukawapa Kwa bei mzuri.
Lakini Serikali imeingilia biashara ya mahindi eti wanatataka kununua wao Kisha wake ya waende kununua kwao, sijui wawe na TIN namba, wasiende Moja Kwa Moja mashambani! Huko ni kumkomoa mshirika. Mahindi yametudodea ndani hatuna mahali pa kuuza. Kuna Ndugu yangu ana gunia 3000 Hana mahali pa kuuza. Mimi Nina gunia 100 Sina mahali pa kuuza. Mahindi yamo ndani yanaliwa na panya huku wakenya wanakufa na njaa.

Kibaya zaidi nasikia Urusi wanataka kuweka ghala ya kuuza nafaka Kenya, maana yake tutakuwa tumepoteza soko la Kenya mazima.
Kazi ya kilimo kwa Tanzania ni kazi ya hovyo hovyo. Tuwashauri vijana wasidanganyike watakuwa masikini.
 
Kwamba wewe ni MKULIMA uliyetunza gunia 3000 ndani?

Acha uongo wewe Si MKULIMA ni Dalali .

Huku masokoni kilo ya unga 1300 , iweje utunze ndani Badala ya kupeleka masokoni.

Serikali ishikilie hapo hapo, soko la ndani Bado hatujitoshelezi.
 
Hili ndiyo kosa kubwa sana serikali ya Samia imetufanyia sisi wakulima. Bashe tulikuwa tunamwelewa sana. Wakulima tulikuwa na vicheko, tuliobahatika tuliuza kidogo mahindi huko huko shambani wakenya walitufuata tukawapa Kwa bei mzuri.
Lakini Serikali imeingilia biashara ya mahindi eti wanatataka kununua wao Kisha wake ya waende kununua kwao, sijui wawe na TIN namba, wasiende Moja Kwa Moja mashambani! Huko ni kumkomoa mshirika. Mahindi yametudodea ndani hatuna mahali pa kuuza. Kuna Ndugu yangu ana gunia 3000 Hana mahali pa kuuza. Mimi Nina gunia 100 Sina mahali pa kuuza. Mahindi yamo ndani yanaliwa na panya huku wakenya wanakufa na njaa.

Kibaya zaidi nasikia Urusi wanataka kuweka ghala ya kuuza nafaka Kenya, maana yake tutakuwa tumepoteza soko la Kenya mazima.
Kazi ya kilimo kwa Tanzania ni kazi ya hovyo hovyo. Tuwashauri vijana wasidanganyike watakuwa masikini.
ChoiceVariable njoo usome hapa maana wewe umetoa taarifa ya uwongo
 
Serikali itanunua mahindi yote,huyo Jamaa kaandika upuuzi tuu usio na msingi na hafuatilii Hali ya mambo. Serikali kununua mahindi inahusikaje na soko kudoda?

Pili hakuna mfanyabiashara ataruhusiwa kwenda farm directly Kununua mahindi ya mkulima bila Kufuata vigezo.

Mwisho Ruto wa Kenya kazuia importation ya mahindi Kwa sababu wamezalisha ziada Kwa ruzuku kama Tanznaia na hivyo wanataka kununua mahindi Yao kwanza na sio ku import mahindi ya Tanzania ambayo ni bei rahisi harafu wauzie Serikali ya Kenya itakuwa hawajamsaidia mkulima wao ndio maana wamezuia.
 
Hili ndiyo kosa kubwa sana serikali ya Samia imetufanyia sisi wakulima. Bashe tulikuwa tunamwelewa sana. Wakulima tulikuwa na vicheko, tuliobahatika tuliuza kidogo mahindi huko huko shambani wakenya walitufuata tukawapa Kwa bei mzuri.
Lakini Serikali imeingilia biashara ya mahindi eti wanatataka kununua wao Kisha wake ya waende kununua kwao, sijui wawe na TIN namba, wasiende Moja Kwa Moja mashambani! Huko ni kumkomoa mshirika. Mahindi yametudodea ndani hatuna mahali pa kuuza. Kuna Ndugu yangu ana gunia 3000 Hana mahali pa kuuza. Mimi Nina gunia 100 Sina mahali pa kuuza. Mahindi yamo ndani yanaliwa na panya huku wakenya wanakufa na njaa.

Kibaya zaidi nasikia Urusi wanataka kuweka ghala ya kuuza nafaka Kenya, maana yake tutakuwa tumepoteza soko la Kenya mazima.
Kazi ya kilimo kwa Tanzania ni kazi ya hovyo hovyo. Tuwashauri vijana wasidanganyike watakuwa masikini.
Mkuu tatitizo la sasa halijasababishwa na bashe wala samia bali kenya ndo imepiga marufuku uingizaji wa mahindi kutoka nje ili kulinda wakulima wake kwa sababu wamehivisha mahindi mengi , na soko kubwa la mahindi ya tz liko kenya.

Kiufupi ukitaka wakulima hasa wa mahindi wafaidike hapa nchini la kwanza ni kuwaombea njaa wakenya.
 
Option ni waache soko liamue, na mipaka isifungwe, anaetaka kuuza China auze, anaetaka kuuza Kenya auze tu
Mipaka haijafungwa mkuu bali kenya ndo imezuia uingizwaji wa mahindi kutoka nje ili kulinda wakulima wake wa mahindi.
 
Waziri Hussein Bashe alikuwa na msimamo mzuri kuanzia alipoteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo kuhusu kufungua mipaka kwa wageni kuja kununua mazao ya kilimo nchini.

Hii ilikuwa ni furaha kwa wakulima wetu, lakini miezi kama 6 tu iliyopita kwa kelele za Watanzania wavivu wakaiyumbisha Serikali mpaka ikaamua kudhibiti biashara ya mahindi.

Angalia kinachoendelea leo kwenye kichwa cha habari cha gazeti la Mwananchi.

View attachment 2783448
Mnataka kusiwe na udhibiti ili fisadi na walanguzi wadhibiti kila kitu. Sasa hamkuona mahindi yote yakiishia kenya na wao kuyauza nje na kupata hela za kigeni wao badala yetu? Wakenya wakaja bila udhibiti na kwenda hdii vijijini kununua kwa shilingi ya kitanzania kwa kubadilishiwa hela zao na walanguzi. Hatukulia njaa kama watanzania? Sera za bashe ni kukuza ufisadi tu aende nazo somalia huko ndio ubabe na nguvu zinatawala.
 
Hili ndiyo kosa kubwa sana serikali ya Samia imetufanyia sisi wakulima. Bashe tulikuwa tunamwelewa sana. Wakulima tulikuwa na vicheko, tuliobahatika tuliuza kidogo mahindi huko huko shambani wakenya walitufuata tukawapa Kwa bei mzuri.
Lakini Serikali imeingilia biashara ya mahindi eti wanatataka kununua wao Kisha wake ya waende kununua kwao, sijui wawe na TIN namba, wasiende Moja Kwa Moja mashambani! Huko ni kumkomoa mshirika. Mahindi yametudodea ndani hatuna mahali pa kuuza. Kuna Ndugu yangu ana gunia 3000 Hana mahali pa kuuza. Mimi Nina gunia 100 Sina mahali pa kuuza. Mahindi yamo ndani yanaliwa na panya huku wakenya wanakufa na njaa.

Kibaya zaidi nasikia Urusi wanataka kuweka ghala ya kuuza nafaka Kenya, maana yake tutakuwa tumepoteza soko la Kenya mazima.
Kazi ya kilimo kwa Tanzania ni kazi ya hovyo hovyo. Tuwashauri vijana wasidanganyike watakuwa masikini.
Unayosema ni kweli , baada ya serikali kuingilia kati wakenya walifunga mpaka kuingiza mahindi .
Nikichukua hyo TIN number na added bureacracy nikienda kenya kuuza nakuta mahindi ya Uganda na malawi ni cheaper kuliko ye2 , Shida serikali hudhani kuwa tukiwa na kitu wengine hawana hawajui supply chains huku chini ni intertwined sana .
Nliacha kununua mahindi kwa wakulima , Rostam na genghi wamewekeza kwa ghala kubwa Nairobi ICD wanaingiza mahindi toka urusi ,serikali isiposhtuka soko lile litaenda
 
Back
Top Bottom