Ahlan Mohamed. Mbona unazidi kufuka muungwana? Hakuna mahali nilipoandika kukufunza adabu na wala sitajaribu. Kwetu tumefunzwa kuongea katika hadhra.
Nitakuvunjia heshima kwa kuanzia wapi wewe mzee wa Mjini! Nikija Dar nyakati hizo nilikuwa na kaptura , Nyerere peke yake aliweza, seuse ngulumbili mimi. Turudi katika mjadala wala usiwe na wahaka heshima ya mtu haivunjwi
Mzee Said, swali langu ni moja ambalo huenda limetibua nyongo lakini sikulipata kwingine ni katika maandiko yako
Hivi si kweli Mzee Kiyate alimpa Nyerere sh 200 za Mboga wakati akienda sokoni?
Hili la mboga lisikutie simanzi, mboga yaweza kuwa msemo ikimaanisha pishi za mchele, kipande cha Ng'onda au fungu la matembele. Sh 200 nyakati hizo nyingi, je, si kweli kwa mujibu wa maandiko yako Kiyate alimpa Mwalimu?
Pili, Mohamed si uliwahi kutueleza hata fundi cherahani wa nguo za Mwalimu? Au tuvute uzi
Picha ya Mwalimu akiwa na kaptura si ilitoka katika nyaraka zako zilizopo katika kavazi la Mwalimu?
Tatu, Mohamed hujawahi kusema Dosa alifilisika kwasababu ya shughuli za Chama?
Nne, Mohamed, hujawahi kuandika mahali ukasema Kiyate aligawa kadi Rufiji?
Mbona ukiulizwa wawa mbogo, maneno useme mwanazuoni, tukifanya reference inakuwa muhali, tukiuliza inakuwa tafrani.
Tujadiliane taratibu tukirudisha nyoyo zetu na kuzungumza kwa mila na desturi zetu sisi wa Pwani na Magila
Nguruvi3,
Sijui kipi kimekufanya uje na staili hii ya kujifanya mpole kwangu na kujitahidi
kuaminisha wasomaji kuwa mimi nimegadhibika.
Sidhani kama kwa mtindo huu utafika mbali na mimi.
Mimi siwezi kuandika kuhusu ''kaptula,'' na maandishi yangu yangekuwa katika
mtindo huo nisingekuwa hapa nilipo katika kuandika historia ya Tanganyika.
Ningedharaulika miaka mingi.
Labda nikufahamishe kitu.
Market Master
Abdul Sykes sare yake ya kazi pale Kariakoo ilikuwa kaptula
na shati jeupe.
Baba yangu akifanya kazi siku hizo ikiitwa ''Exchange,'' Idara ya Simu Posta ya
kikoloni nikimuona akivaa kaptula na ''stockings.''
Wazee wengi hapa Dar es Salaam katika 1950 sisi wadogo tukiwaona na kivazi
hicho na kwa hakika kilikuwa kivazi cha wasomi.
Hivi vijembe vyako vya, ''kaptula,'' mtupie mtu mwingine mimi sihusiki navyo.
Ikiwa umekuta uandishi wa ''kaptula,'' katika yale niliyoandika basi lete hapa
tusome tumalize ubishi huu.
Uhusiano wa
Mshume Kiyate na
Mwalimu Nyerere nimeueleza kwa kirefu
katika kitabu cha
Abdul Sykes yeyote atakae anaweza akasoma.
Wala simlazimishi mtu kuamini, si hayo ya
Kiyate Mshume hata kuwa
Abdul
kadi yake ya TANU ni no. 3 na mdogo wake
Ally ni na. 2 na
Nyerere na. 1 si
lazima iaminike.
Huna haja ya kuamini.
Dossa nimesema amefilisika katika siasa.
Katika
Kavazi la Mwalimu Nyerere hakuna nyaraka zangu hizo kama umeziona
ni nyaraka ambazo mimi nimepata katika
Nyaraka za Sykes hakuna chochote
katika hizo nyaraka zinazohusu ''kaptula.''
Sijapata kusema kuwa
Kiyate Mshumi aligawa kadi za TANU Rufiji.
Rufiji
Abdul Sykes alimkabidhi
Said Chamwenyewe hii iilikuwa Julai 1954
wakati wa kuisajili TANU na ndiyo walitoa wanachama wa mwanzo wa TANU
na uamuzi huu ulifanywa nyumbani kwa
Ally Sykes Mtaa wa Kipata na hapo
aikuwapo walikuwa
Abdul, Ally na
Nyerere na Bi.
Zainab mkewe
Ally Sykes.
Abdul Sykes mwenyewe yeye aliuza kadi za TANU pale kazini kwake Kariakoo
Market.
Kisa hiki nimekieleza katika kitabu cha
Abdul Sykes atakae anaweza kusoma.
Nahitimisha kwa kufahamisha kuwa sina ''muhali,'' wala ''tafrani,'' lugha yangu
ndiyo hii ikiwa hii unaona ni shari kwako basi hakika una lako jambo.