Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
ACT Wazalendo imefuatilia kwa karibu kukithiri kwa tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo mbalimbali nchini, hususan ongezeko la mgao wa maji unaowaacha mamilioni ya wananchi bila hakika ya huduma hiyo kwa siku kadhaa mfululizo. Katika maeneo tuliyofuatilia maji hutoka mara moja kwa wiki, usiku wa manane au hayatoki kabisa, hali inayowalazimu wananchi kutumia fedha nyingi kununua maji, kupoteza muda wa uzalishaji na kuwaathiri wanafunzi, vituo vya afya na shughuli nyingine za kijamii na kiuchumi.
Katika miezi ya hivi karibuni tumepokea malalamiko mengi kutoka maeneo yanayohudumiwa na DAWASA, ikiwemo Ubungo, Kimara, Mbezi, Kinyerezi, Tabata, Kurasini, Tegeta, Bunju, Manzese, Gongo la Mboto, Kigamboni na Makumbusho. Hali kama hiyo pia ipo katika mikoa ya Njombe, Mwanza, Dodoma, Pwani, Mara (Butiama, Rorya na Bunda) pamoja na Iringa-Mufindi Kaskazini ambako wananchi wameendelea kusubiri kwa zaidi ya miaka mitatu utekelezaji wa Mradi wa Maji wa RDO bila mafanikio.
ACT Wazalendo inafahamu kuwa kukithiri kwa tatizo la mgao, upatikanaji duni wa huduma za maji kunatokana na uzembe, usimamizi dhaifu wa miradi, ubadhirifu wa fedha za umma na kushindwa kuwawajibisha wanaosababisha hasara katika sekta hii muhimu. Aidha, tunajua kuna hila ya Wizara ya Maji kupitia waziri Jumaa Aweso na taasisi zake ili kuhalalisha kuuza miundombinu ya maji ya umma kwa jina la Ubia na Ubinafsishaji kwa kuwanuifaisha watu wachache kwa gharama ya maumivu ya wananchi walio wengi.
Kwa miaka kadhaa, ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali zimeendelea kubainisha uchakavu wa miundombinu, upotevu mkubwa wa maji, uzalishaji usiokidhi mahitaji na usimamizi usioridhisha wa miradi. Mfano ni Mradi wa Same–Mwanga–Korogwe wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 400 ambao tayari unapoteza takribani asilimia 70 ya maji yanayozalishwa. Hali hii inaonesha kuwa tatizo si ukosefu wa fedha wala maji, bali ni kushindwa kwa Serikali kutekeleza wajibu wake.
Kwa msingi huo, ACT Wazalendo inaitaka Serikali:
Kukomesha mara moja mgao wa maji na kuhakikisha huduma ya maji inapatikana saa ishirini na nne kwa siku, siku saba kwa wiki.
Kukagua na kukamilisha miradi yote ya maji, huku wote waliohusika na ubadhirifu wakichukuliwa hatua za kisheria.
Kuchukua hatua dhidi ya menejimenti na bodi za mamlaka za maji zilizoshindwa kutekeleza wajibu wake, hususan DAWASA.
Kusitisha mipango yoyote ya kubinafsisha sekta ya maji na kuongeza uwekezaji wa Serikali katika huduma hiyo.
Kuelekeza fedha zote za Mfuko wa Maji, ikiwemo shilingi bilioni 207.01 za mwaka 2024/2025 pamoja na makusanyo ya mwaka 2025/2026, katika upanuzi wa miundombinu ya maji.
Wananchi hawahitaji ahadi mpya; wanahitaji maji ya uhakika. Serikali inapaswa kuwajibika kwa kuhakikisha kila Mtanzania anapata haki yake ya msingi ya maji safi na salama.
Imetolewa na;
Ndg. Yasinta Cornely Awiti Waziri Kivuli wa Maji
ACT Wazalendo Julai 4, 2026