Muungano kwa sasa ni sentimental, muda utafika wazanzibari wasipo badilika utakufa natural death.
Na Wazanzibar wanahusika zaidi, iwe kwa manufaa au la , uharibifu umeshanyika.
Mimi na wewe haya majibizano hatujaanza leo, huko nyuma tulikuwa wide apart kwenye hoja (toka zama rasimu ya katiba). Mimi nikiwa pro muungano.
Sina tatizo na Muungano, lakini muungano wowote lazima uwe 'win-win situation''. Kwasasa Muungano umekuwa burden kwa Tanganyika. Fikiria, Mchango wa Zanzibar haupo lakini kuna investment kubwa inafanywa kuwa please. Hakuna Mkoa wa Tanganyika unaopokea resource nyingi kuliko Zanzibar.
Tazama population na eneo la Zanzibar plus autonomy ya kuwa na serikali halafu ujiulize, kwanini Zbar !
Leo bado nipo upande wa muungano, ila naona wazanzibari wanahitaji kubadilika. Ipo siku viongozi wa kesho ambao hawalishiwi propaganda za muungano kama nilizokua nazo mimi wakati nipo shule (maana sio kizazi cha TANU) bali wa kulishwa propaganda zao muungano wao.
Kizazi cha sasa ni tofauti na kile cha Mwalimu.Muungano unaangaliwa kwa jicho la uchumi si undugu wa kufanana. Waliosaidia ku sentisitize kizazi cha Watanganyika ni Wazanzibar kama akina OMO. Tuwashukuru sana
Ukimuuliza OMO, mchango wa Zanzibar katika muungano ni upi, hana jibu na wala hajawahi kujibu
Ukimuuliza wapi wanaonewa, hana jibu lakini akitoka hapo anarudia upuuzi ule ule.
Ukimwambia kwanini ACT hawapeleki mswada Baraza la Wawakilishi kuvunja muungano, hana jibu
Kwa hivyo nina kijisentimenti ka muungano, japo mtu kama OMO anachosha balaa; sasa ipo siku kutakuwa na watu serikalini ambao hawana sentiments za TANU na Afro Shiraz kwa upande wa bara kabisa. Hoja zao na msingi wao wa maamuzi itakuwa what’s in it for us; hapo ndio tutakapo gawana mbao.
Maalimu Seif alikuwa reasonable ukimlinganisha na OMO. Huyu OMO hana hoja za msingi na hata anazotoa ni hafifu sana. Kuhusu watu Serikali Wapo tayari ni 'suala la muda tu'' na kila mahali watu wanauliza swali lako ''what's in it for us''. Na kwanini Wazanzibar wana 'special status'' katika muungano! na wao kwa u special wao wana mchango gani kwa maendeleo ya Tanganyika.
Kwanini Tanganyika haina autonomy ya mambo ambayo Zanzibar hawataki yawe ya Muungano!
Kwa mfano Elimu ya Juu, Afya, Kilimo, Utalii, Madini, Viwanda na Biashara, Maliasili n.k. kwanini ziwe za JMT ambazo Zanzibar ni beneficiary kwa kupitia jina Tanzania lakini Zanzibar hao hao hawataki kuwa sehemu ya mchango wa hayo mambo tena wanasema ni mambo yameongezwa kinyemala
Kasheshe wanazaliana hao balaa, sijui wataenda wapi.
Hilo ni tatizo lao! Hawatazami jinsi Zbar inavyouzwa, visiwa vyote mnada! ni tatizo lao