ACT: Tunapinga mpango wa DC Temeke kufuta Kata 10 ili kupisha Bandari Kavu, wamenogewa na biashara

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876

ACT Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam imepokea kwa mshangao na kupinga vikali kauli za Mkuu wa Wilaya ya Temeke Ndg. Sixtus Mapunda kuhusu mpango wa kuhamisha wakazi na kuathiri uwepo wa kata zipatazo 10 katika Wilaya ya Temeke kwa madai ya kupisha ujenzi au shughuli za Bandari Kavu (ICDs). Kauli hiyo ilitolewa tarehe 27 Agosti 2026 akiwa katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ndg. Albert Chalamila, kwenye eneo la Kirimanjaro ICD, Kurasini.

Katika kauli hiyo, Ndg. Mapunda alisema kuwa Manispaa ya Temeke imeandaa kata 10 nyingine kufuata mfano wa Kurasini kwa ajili ya matumizi yanayohusiana na Bandari, huku akieleza kuwa wananchi wanapaswa kuelewa kuwa ‘Bandari haihami, ila sisi wanadamu tunaweza kuhama.

Inasitikisha sana, ingawa haishangazi kusikia hivyo kutoka Viongozi wa CCM kutoa kauli hizo katika hali ambayo Dar es Salaam imeshuhudia ongezeko kubwa la bandari kavu, vituo vya makasha na maghala ya mizigo. Utitiri huu umechangia msongamano mkubwa wa malori, foleni kubwa barabani, uharibifu wa barabara, ucheleweshaji wa mizigo, kuongezeka kwa gharama za biashara na kuvurugika kwa maisha ya wananchi.

Kauli ya awali ~ DC Mapunda: Baada ya Kurasini, Temeke tumetenga Kata 10 nyingine kwa matumizi ya Bandari

ACT Wazalendo Mkoa hatutakubali wananchi wa Temeke kuwa wahanga wa uzembe wa Serikali katika mipango miji na usimamizi wa sekta ya usafirishaji. Hatutakubali kata za wananchi kufutwa, wakazi kuhamishwa na maisha yao kuvurugwa wakati Serikali yenyewe imeshindwa kutumia maeneo ambayo tayari iliyatenga na kuyawekea miundombinu kwa ajili ya shughuli za bandari kavu.

Serikali tayari ilitenga na kuendeleza eneo la Kwala, Mkoa wa Pwani, kwa madhumuni ya kuhudumia shughuli za bandari kavu. Eneo hilo limeunganishwa na miundombinu muhimu ya usafirishaji na lilikusudiwa kupunguza msongamano wa mizigo katika Jiji la Dar es Salaam.

Kwa hiyo, ni kinyume cha mantiki kwa Serikali kushindwa kutumia kikamilifu Kwala halafu leo ije na mpango wa kufuta kata na kuwahamisha wananchi wa Temeke ili kupisha shughuli ambazo zinaweza na zinapaswa kupelekwa nje ya Jiji la Dar es Salaam.

ACT Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam tunaendelea kuunga mkono tamko la Waziri Kivuli wa Miundombinu, Ujenzi na Uchukuzi wa ACT Wazalendo Ndg. Abdallah Mtutura la kutaka bandari kavu ziondolewe katikati ya Jiji la Dar es Salaam, kusitisha utolewaji wa vibali vipya na shughuli hizo kuelekezwa Kwala.

Aidhai, tunamtaka Mkuu wa Wilaya wa Temeke kusitisha mara moja mpango wowote wa kuwahamisha wakazi au kufuta kata za Temeke kwa kisingizio cha kupisha Bandari Kavu;

Iwapo Serikali itaendelea kupuuza sauti za wananchi na kusukuma mbele mpango huu wa kuwaondoa wakazi wa Temeke katika maeneo yao, ACT Wazalendo itahamasisha wananchi wa Temeke na Dar es Salaam kwa ujumla kutumia haki yao ya kikatiba ya kuandamana kwa amani na kupaza sauti dhidi ya mpango huu.

Tunawaambia wananchi wa Temeke kuwa hatutawaacha peke yao katika mapambano haya. Tutatumia njia zote halali kupinga mpango wowote unaolenga kuwanyang'anya wananchi makazi yao na kufuta maeneo yao kwa sababu ya kushindwa kwa Serikali kupanga mji na kusimamia shughuli za bandari.

Imetolewa na:
Ndg. Felix Kamugisha
Katibu wa Mkoa, Dar es Salaam
3 Septemba, 2026
 
ACT wanajifanya kuongea kinyume na WASHIRIKA wao ...!!? OMO au Jusa wakisia watamtia adabu huyo DOGO kwa kumhujumu DADA. Haoni hata akina Zitto wa meshaufyata kabisa....!!
 
haya mashehe wako wapi? kwa maana wanaonewa hapa na muslims, tmk ni predominatly muslim.

muslims wa hii nchi siku zote wako better off kama nchi ikiwa Christian klk kinyume chake, na huo ndiyo ukweli wenyewe hata kama ni ngumu kumeza, sasa nani atawatetea? shehe mwaipopo yuko wapi? bakwata je? muslim on muslim, walipowafukuza na kuwamisha wamasai kwao baadhi yenu muslims wa tanzagiza mliitetea hii regime sasa wameingia mjini na they will not stop mpaka kila mtu atafikiwa.

hii vita ni good vs evil wote tuungane against evil ...
 
Wawajengee maghorofa yenye apartments kabla kuwahamishia wakazi hao wa kata 10 ambao kwa sasa wanaoishi katika mitaa iliyopangika toka enzi ya mkoloni.

Bila kufanya utaratibu huo hapo juu ni kuzidi kutanua mitaa isiyo na mpangilio na jiji kuzidi kuwa mitaa ya makaazi ya mabanda
 
kwala nini hatima yake, maana sgr link tayari
 
1788443327527.png

TOKA MAKTABA :
09 August 2026

Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, kupitia Baraza la Madiwani na viongozi wake linaloongozwa na CCM , imeidhinisha mpango wa kutenga na kuongeza kata 10 maalum

View: https://m.youtube.com/watch?v=KC45PqeUAHk

Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, kupitia Baraza la Madiwani na viongozi wake, imeidhinisha mpango wa kutenga na kuongeza kata 10 maalum kwa ajili ya ujenzi na upanuzi wa bandari kavu (Inland Container Depots - ICDs) mitaani. Hatua hii inakuja kufuatia ongezeko kubwa la shehena na makontena yanayopakuliwa katika bandari ya Dar es Salaam

Sababu Kuu za Kutenga Maeneo Hayo kwa mujibu wa madiwani hao wa chama kimoja CCM ni :

Kuhifadhi shehena kubwa: Ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam umesababisha kupakuliwa kwa zaidi ya makontena 160,000 kwa mwezi (kiwango kilichotarajiwa kufikiwa mwaka 2030). Maeneo mapya yanasaidia kupunguza mrundikano bandarini.

Ukaribu wa soko na viwanda: Takwimu zinaonesha asilimia 67 ya mizigo inayobaki Dar es Salaam huishia wilayani Temeke kutokana na uwepo wa viwanda vingi na ukaribu wake na soko kuu la Kariakoo.

Kupunguza foleni za malori: Mpango huu unalenga kuondoa changamoto ya msongamano mkubwa wa malori yanayopaki kando ya barabara kuu za jiji

Mikakati na Maagizo ya Serikali ya CCM
Wakati wa ziara ya ukaguzi wa uwekezaji kwenye bandari kavu ya Kilimanjaro (KICD) iliyopo Kurasini, Temeke mnamo Agosti 27, 2026, viongozi wa serikali walisisitiza mambo yafuatayo:

Ushirikiano wa Wananchi: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda, wamewataka wananchi kutoa ushirikiano katika maeneo yaliyotengwa ili kupisha uwekezaji huo muhimu wa kiuchumi.

Miundombinu ya Reli na Barabara: Serikali imepanga kuunganisha bandari kavu zote na miundombinu ya reli. Pia, mashirika ya TANROADS na TARURA yameagizwa kujenga barabara za mzunguko (bypass roads) ili kurahisisha mzunguko wa malori.

Maegesho Ndani ya ICD: Waendeshaji wa bandari kavu wametakiwa kuhakikisha wana maeneo makubwa na ya kutosha ya maegesho ya ndani ili malori yasubiri mzigo yakiwa ndani ya vituo na sio barabarani.
 
01 September 2026

DG TASAC: BANDARI KAVU ZAONGEZA UFANISI WA BANDARI YA DAR ES SALAAM​

Imewekwa: 01 September, 2026

View: https://m.youtube.com/watch?v=vcRc6gKWXgY
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Bw. Mohamed Mallick Salum, amesema uanzishwaji na uendeshaji wa bandari kavu umechangia kupunguza msongamano wa shehena na kuongeza ufanisi zaidi wa Bandari ya Dar es Salaam.

Akizungumza Agosti 31, 2026, katika Ukumbi wa PSSSF Dar es Salaam, Bw. Salum amesema ongezeko la shehena limeongeza mahitaji ya maeneo mbadala ya kuhifadhi na kuhudumia makasha.

Amesema kati ya mwaka 2021 na 2025, shehena iliyohudumiwa bandarini iliongezeka kwa asilimia 88, kutoka tani milioni 16.9 hadi milioni 31.8, huku shehena ya makasha ikiongezeka kwa asilimia 58, kutoka makasha 749,850 hadi 1,185,153.

“Bandari kavu husaidia kupunguza msongamano bandarini na kuiwezesha Bandari ya Dar es Salaam kutoa huduma kwa ufanisi zaidi. Bandari hii ni kitovu cha uchumi wa Taifa na biashara ya kikanda,” amesema Bw. Salum.

Amesema Bandari ya Dar es Salaam ina uwezo wa kuhifadhi makasha 27,900. Julai 2026, eneo la bandari linaloendeshwa na TEAGTL lilihudumia makasha 91,625, hali inayoonesha ongezeko la mizigo.

Bw. Salum amesema Serikali imeendelea kuongeza uwezo wa kuhudumia mizigo kwa kuanzisha bandari kavu Kwala, Morogoro na Isaka, pamoja na kuhamasisha uwekezaji wa sekta binafsi katika miundombinu ya usafirishaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Bw. Abed Galius, amesema TPA inaendelea kuboresha uwezo wa kuhifadhi na kuhamisha makontena ili kukabiliana na ongezeko la mizigo na kuimarisha nafasi ya Tanzania kama kitovu cha biashara kikanda.

Aidha, Mwenyekiti wa Wamiliki wa Bandari Kavu, Bw. Meleck Shange, amesema sekta binafsi ina wajibu wa kuwekeza katika bandari kavu, vifaa, mifumo na nguvu kazi, huku Serikali ikisimamia usalama wa huduma.

TASAC inaendelea kuimarisha usimamizi wa bandari kavu kwa kuhakikisha zina maeneo na maegesho ya kutosha, barabara zenye uwezo unaothibitishwa na TARURA au TANROADS, na ujazo wa mizigo usiozidi asilimia 60. Na kwa sasa TASAC pia imesitisha kwa muda utoaji wa leseni mpya za bandari kavu Dar es Salaam

View: https://m.youtube.com/watch?v=8IYA42yR7aU
 
Kwala hakuendeki huko !

Labda itoke aje kiongozi imara,no kujuwana
Kwala kutaendeka

Ova
mwaka sasa toka uzinduzi , ila bado haieleweki nani mwenye mamlaka hata ya kutueleza nini kinasuasua
 
ACT Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam imepokea kwa mshangao na kupinga vikali kauli za Mkuu wa Wilaya ya Temeke Ndg. Sixtus Mapunda kuhusu mpango wa kuhamisha wakazi na kuathiri uwepo wa kata zipatazo 10 katika Wilaya ya Temeke kwa madai ya kupisha ujenzi au shughuli za Bandari Kavu (ICDs). Kauli hiyo ilitolewa tarehe 27 Agosti 2026 akiwa katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ndg. Albert Chalamila, kwenye eneo la Kirimanjaro ICD, Kurasini.

Katika kauli hiyo, Ndg. Mapunda alisema kuwa Manispaa ya Temeke imeandaa kata 10 nyingine kufuata mfano wa Kurasini kwa ajili ya matumizi yanayohusiana na Bandari, huku akieleza kuwa wananchi wanapaswa kuelewa kuwa ‘Bandari haihami, ila sisi wanadamu tunaweza kuhama.

Inasitikisha sana, ingawa haishangazi kusikia hivyo kutoka Viongozi wa CCM kutoa kauli hizo katika hali ambayo Dar es Salaam imeshuhudia ongezeko kubwa la bandari kavu, vituo vya makasha na maghala ya mizigo. Utitiri huu umechangia msongamano mkubwa wa malori, foleni kubwa barabani, uharibifu wa barabara, ucheleweshaji wa mizigo, kuongezeka kwa gharama za biashara na kuvurugika kwa maisha ya wananchi.

Kauli ya awali ~ DC Mapunda: Baada ya Kurasini, Temeke tumetenga Kata 10 nyingine kwa matumizi ya Bandari

ACT Wazalendo Mkoa hatutakubali wananchi wa Temeke kuwa wahanga wa uzembe wa Serikali katika mipango miji na usimamizi wa sekta ya usafirishaji. Hatutakubali kata za wananchi kufutwa, wakazi kuhamishwa na maisha yao kuvurugwa wakati Serikali yenyewe imeshindwa kutumia maeneo ambayo tayari iliyatenga na kuyawekea miundombinu kwa ajili ya shughuli za bandari kavu.

Serikali tayari ilitenga na kuendeleza eneo la Kwala, Mkoa wa Pwani, kwa madhumuni ya kuhudumia shughuli za bandari kavu. Eneo hilo limeunganishwa na miundombinu muhimu ya usafirishaji na lilikusudiwa kupunguza msongamano wa mizigo katika Jiji la Dar es Salaam.

Kwa hiyo, ni kinyume cha mantiki kwa Serikali kushindwa kutumia kikamilifu Kwala halafu leo ije na mpango wa kufuta kata na kuwahamisha wananchi wa Temeke ili kupisha shughuli ambazo zinaweza na zinapaswa kupelekwa nje ya Jiji la Dar es Salaam.

ACT Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam tunaendelea kuunga mkono tamko la Waziri Kivuli wa Miundombinu, Ujenzi na Uchukuzi wa ACT Wazalendo Ndg. Abdallah Mtutura la kutaka bandari kavu ziondolewe katikati ya Jiji la Dar es Salaam, kusitisha utolewaji wa vibali vipya na shughuli hizo kuelekezwa Kwala.

Aidhai, tunamtaka Mkuu wa Wilaya wa Temeke kusitisha mara moja mpango wowote wa kuwahamisha wakazi au kufuta kata za Temeke kwa kisingizio cha kupisha Bandari Kavu;

Iwapo Serikali itaendelea kupuuza sauti za wananchi na kusukuma mbele mpango huu wa kuwaondoa wakazi wa Temeke katika maeneo yao, ACT Wazalendo itahamasisha wananchi wa Temeke na Dar es Salaam kwa ujumla kutumia haki yao ya kikatiba ya kuandamana kwa amani na kupaza sauti dhidi ya mpango huu.

Tunawaambia wananchi wa Temeke kuwa hatutawaacha peke yao katika mapambano haya. Tutatumia njia zote halali kupinga mpango wowote unaolenga kuwanyang'anya wananchi makazi yao na kufuta maeneo yao kwa sababu ya kushindwa kwa Serikali kupanga mji na kusimamia shughuli za bandari.

Imetolewa na:
Ndg. Felix Kamugisha
Katibu wa Mkoa, Dar es Salaam
3 Septemba, 2026

21 October 2026
Mtaa wa Mji Mpya
Kata ya Azimio
Postikodi: 15106
Wilaya ya Temeke
Dar es Salaam, Tanzania

WANAFUNZI NA WANANCHI WAPINGA ENEO LA SHULE YA AZIMIO KUNYAKULIWA NA KAMPUNI YA BANDARI KAVU 21 OCTOBER 2026

View: https://m.youtube.com/watch?v=zB9qpCrNRrs

Eneo la Square meter 12,000 ya shule ya Azimio iliyopo halmashauri ya Temeke jijiji Dar es Salaam lanyakuliwa na mwekezaji wa bandari kavu

Wanafunzi waongea na diwani wao kupinga zoezi hilo katika shule hiyo huku wazazi pia wajiuliza maamuzi haya ya kutaka kugeuza eneo la shule kuwa bandari kavu

Naye DC mkuu wa wilaya : Mipango ya Eneo: Eneo la Mtaa wa Mji Mpya na Kata ya Azimio linahusika na mijadala ya mipango ya maendeleo na matumizi ya ardhi ya Wilaya ya Temeke chini ya Mkuu wa Wilaya, Sixtus Mapunda

4 September 2026
DC SIXTUS MAPUNDA, MADIWANI HALMASHAURI YA TEMEKE NA MIPANGO YAO
WAKAZI WA KATA 10 KUHAMISHWA KUPISHA BANDARI?, ACT KUITISHA MAANDAMANO, DC TEMEKE ATEMA CHECHE

View: https://m.youtube.com/watch?v=G96kNHM0JFc
 
Bandari kavu ziwekwe kariakoo na posta ndio karibu na bandari
 
ACT Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam imepokea kwa mshangao na kupinga vikali kauli za Mkuu wa Wilaya ya Temeke Ndg. Sixtus Mapunda kuhusu mpango wa kuhamisha wakazi na kuathiri uwepo wa kata zipatazo 10 katika Wilaya ya Temeke kwa madai ya kupisha ujenzi au shughuli za Bandari Kavu (ICDs). Kauli hiyo ilitolewa tarehe 27 Agosti 2026 akiwa katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ndg. Albert Chalamila, kwenye eneo la Kirimanjaro ICD, Kurasini.

Katika kauli hiyo, Ndg. Mapunda alisema kuwa Manispaa ya Temeke imeandaa kata 10 nyingine kufuata mfano wa Kurasini kwa ajili ya matumizi yanayohusiana na Bandari, huku akieleza kuwa wananchi wanapaswa kuelewa kuwa ‘Bandari haihami, ila sisi wanadamu tunaweza kuhama.

Inasitikisha sana, ingawa haishangazi kusikia hivyo kutoka Viongozi wa CCM kutoa kauli hizo katika hali ambayo Dar es Salaam imeshuhudia ongezeko kubwa la bandari kavu, vituo vya makasha na maghala ya mizigo. Utitiri huu umechangia msongamano mkubwa wa malori, foleni kubwa barabani, uharibifu wa barabara, ucheleweshaji wa mizigo, kuongezeka kwa gharama za biashara na kuvurugika kwa maisha ya wananchi.

Kauli ya awali ~ DC Mapunda: Baada ya Kurasini, Temeke tumetenga Kata 10 nyingine kwa matumizi ya Bandari

ACT Wazalendo Mkoa hatutakubali wananchi wa Temeke kuwa wahanga wa uzembe wa Serikali katika mipango miji na usimamizi wa sekta ya usafirishaji. Hatutakubali kata za wananchi kufutwa, wakazi kuhamishwa na maisha yao kuvurugwa wakati Serikali yenyewe imeshindwa kutumia maeneo ambayo tayari iliyatenga na kuyawekea miundombinu kwa ajili ya shughuli za bandari kavu.

Serikali tayari ilitenga na kuendeleza eneo la Kwala, Mkoa wa Pwani, kwa madhumuni ya kuhudumia shughuli za bandari kavu. Eneo hilo limeunganishwa na miundombinu muhimu ya usafirishaji na lilikusudiwa kupunguza msongamano wa mizigo katika Jiji la Dar es Salaam.

Kwa hiyo, ni kinyume cha mantiki kwa Serikali kushindwa kutumia kikamilifu Kwala halafu leo ije na mpango wa kufuta kata na kuwahamisha wananchi wa Temeke ili kupisha shughuli ambazo zinaweza na zinapaswa kupelekwa nje ya Jiji la Dar es Salaam.

ACT Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam tunaendelea kuunga mkono tamko la Waziri Kivuli wa Miundombinu, Ujenzi na Uchukuzi wa ACT Wazalendo Ndg. Abdallah Mtutura la kutaka bandari kavu ziondolewe katikati ya Jiji la Dar es Salaam, kusitisha utolewaji wa vibali vipya na shughuli hizo kuelekezwa Kwala.

Aidhai, tunamtaka Mkuu wa Wilaya wa Temeke kusitisha mara moja mpango wowote wa kuwahamisha wakazi au kufuta kata za Temeke kwa kisingizio cha kupisha Bandari Kavu;

Iwapo Serikali itaendelea kupuuza sauti za wananchi na kusukuma mbele mpango huu wa kuwaondoa wakazi wa Temeke katika maeneo yao, ACT Wazalendo itahamasisha wananchi wa Temeke na Dar es Salaam kwa ujumla kutumia haki yao ya kikatiba ya kuandamana kwa amani na kupaza sauti dhidi ya mpango huu.

Tunawaambia wananchi wa Temeke kuwa hatutawaacha peke yao katika mapambano haya. Tutatumia njia zote halali kupinga mpango wowote unaolenga kuwanyang'anya wananchi makazi yao na kufuta maeneo yao kwa sababu ya kushindwa kwa Serikali kupanga mji na kusimamia shughuli za bandari.

Imetolewa na:
Ndg. Felix Kamugisha
Katibu wa Mkoa, Dar es Salaam
3 Septemba, 2026

Maendeleo na siasa havijawahi kukaa room moja

Haya maujinga Magu aliyapiga mapema sana
 
Sawa kama wanafanya kwa muktadha wa mipango miji ya kisasa.
 
Back
Top Bottom