Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
ACT Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam imepokea kwa mshangao na kupinga vikali kauli za Mkuu wa Wilaya ya Temeke Ndg. Sixtus Mapunda kuhusu mpango wa kuhamisha wakazi na kuathiri uwepo wa kata zipatazo 10 katika Wilaya ya Temeke kwa madai ya kupisha ujenzi au shughuli za Bandari Kavu (ICDs). Kauli hiyo ilitolewa tarehe 27 Agosti 2026 akiwa katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ndg. Albert Chalamila, kwenye eneo la Kirimanjaro ICD, Kurasini.
Katika kauli hiyo, Ndg. Mapunda alisema kuwa Manispaa ya Temeke imeandaa kata 10 nyingine kufuata mfano wa Kurasini kwa ajili ya matumizi yanayohusiana na Bandari, huku akieleza kuwa wananchi wanapaswa kuelewa kuwa ‘Bandari haihami, ila sisi wanadamu tunaweza kuhama.
Inasitikisha sana, ingawa haishangazi kusikia hivyo kutoka Viongozi wa CCM kutoa kauli hizo katika hali ambayo Dar es Salaam imeshuhudia ongezeko kubwa la bandari kavu, vituo vya makasha na maghala ya mizigo. Utitiri huu umechangia msongamano mkubwa wa malori, foleni kubwa barabani, uharibifu wa barabara, ucheleweshaji wa mizigo, kuongezeka kwa gharama za biashara na kuvurugika kwa maisha ya wananchi.
Kauli ya awali ~ DC Mapunda: Baada ya Kurasini, Temeke tumetenga Kata 10 nyingine kwa matumizi ya Bandari
ACT Wazalendo Mkoa hatutakubali wananchi wa Temeke kuwa wahanga wa uzembe wa Serikali katika mipango miji na usimamizi wa sekta ya usafirishaji. Hatutakubali kata za wananchi kufutwa, wakazi kuhamishwa na maisha yao kuvurugwa wakati Serikali yenyewe imeshindwa kutumia maeneo ambayo tayari iliyatenga na kuyawekea miundombinu kwa ajili ya shughuli za bandari kavu.
Serikali tayari ilitenga na kuendeleza eneo la Kwala, Mkoa wa Pwani, kwa madhumuni ya kuhudumia shughuli za bandari kavu. Eneo hilo limeunganishwa na miundombinu muhimu ya usafirishaji na lilikusudiwa kupunguza msongamano wa mizigo katika Jiji la Dar es Salaam.
Kwa hiyo, ni kinyume cha mantiki kwa Serikali kushindwa kutumia kikamilifu Kwala halafu leo ije na mpango wa kufuta kata na kuwahamisha wananchi wa Temeke ili kupisha shughuli ambazo zinaweza na zinapaswa kupelekwa nje ya Jiji la Dar es Salaam.
ACT Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam tunaendelea kuunga mkono tamko la Waziri Kivuli wa Miundombinu, Ujenzi na Uchukuzi wa ACT Wazalendo Ndg. Abdallah Mtutura la kutaka bandari kavu ziondolewe katikati ya Jiji la Dar es Salaam, kusitisha utolewaji wa vibali vipya na shughuli hizo kuelekezwa Kwala.
Aidhai, tunamtaka Mkuu wa Wilaya wa Temeke kusitisha mara moja mpango wowote wa kuwahamisha wakazi au kufuta kata za Temeke kwa kisingizio cha kupisha Bandari Kavu;
Iwapo Serikali itaendelea kupuuza sauti za wananchi na kusukuma mbele mpango huu wa kuwaondoa wakazi wa Temeke katika maeneo yao, ACT Wazalendo itahamasisha wananchi wa Temeke na Dar es Salaam kwa ujumla kutumia haki yao ya kikatiba ya kuandamana kwa amani na kupaza sauti dhidi ya mpango huu.
Tunawaambia wananchi wa Temeke kuwa hatutawaacha peke yao katika mapambano haya. Tutatumia njia zote halali kupinga mpango wowote unaolenga kuwanyang'anya wananchi makazi yao na kufuta maeneo yao kwa sababu ya kushindwa kwa Serikali kupanga mji na kusimamia shughuli za bandari.
Imetolewa na:
Ndg. Felix Kamugisha
Katibu wa Mkoa, Dar es Salaam
3 Septemba, 2026
Kwala hakuendeki huko !kwala nini hatima yake, maana sgr link tayari
TOKA MAKTABA :
09 August 2026
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, kupitia Baraza la Madiwani na viongozi wake linaloongozwa na CCM , imeidhinisha mpango wa kutenga na kuongeza kata 10 maalum
View: https://m.youtube.com/watch?v=KC45PqeUAHk
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, kupitia Baraza la Madiwani na viongozi wake, imeidhinisha mpango wa kutenga na kuongeza kata 10 maalum kwa ajili ya ujenzi na upanuzi wa bandari kavu (Inland Container Depots - ICDs) mitaani. Hatua hii inakuja kufuatia ongezeko kubwa la shehena na makontena yanayopakuliwa katika bandari ya Dar es Salaam
Sababu Kuu za Kutenga Maeneo Hayo kwa mujibu wa madiwani hao wa chama kimoja CCM ni :
Kuhifadhi shehena kubwa: Ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam umesababisha kupakuliwa kwa zaidi ya makontena 160,000 kwa mwezi (kiwango kilichotarajiwa kufikiwa mwaka 2030). Maeneo mapya yanasaidia kupunguza mrundikano bandarini.
Ukaribu wa soko na viwanda: Takwimu zinaonesha asilimia 67 ya mizigo inayobaki Dar es Salaam huishia wilayani Temeke kutokana na uwepo wa viwanda vingi na ukaribu wake na soko kuu la Kariakoo.
Kupunguza foleni za malori: Mpango huu unalenga kuondoa changamoto ya msongamano mkubwa wa malori yanayopaki kando ya barabara kuu za jiji
Mikakati na Maagizo ya Serikali ya CCM
Wakati wa ziara ya ukaguzi wa uwekezaji kwenye bandari kavu ya Kilimanjaro (KICD) iliyopo Kurasini, Temeke mnamo Agosti 27, 2026, viongozi wa serikali walisisitiza mambo yafuatayo:
Ushirikiano wa Wananchi: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda, wamewataka wananchi kutoa ushirikiano katika maeneo yaliyotengwa ili kupisha uwekezaji huo muhimu wa kiuchumi.
Miundombinu ya Reli na Barabara: Serikali imepanga kuunganisha bandari kavu zote na miundombinu ya reli. Pia, mashirika ya TANROADS na TARURA yameagizwa kujenga barabara za mzunguko (bypass roads) ili kurahisisha mzunguko wa malori.
Maegesho Ndani ya ICD: Waendeshaji wa bandari kavu wametakiwa kuhakikisha wana maeneo makubwa na ya kutosha ya maegesho ya ndani ili malori yasubiri mzigo yakiwa ndani ya vituo na sio barabarani.
mwaka sasa toka uzinduzi , ila bado haieleweki nani mwenye mamlaka hata ya kutueleza nini kinasuasuaKwala hakuendeki huko !
Labda itoke aje kiongozi imara,no kujuwana
Kwala kutaendeka
Ova
ACT Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam imepokea kwa mshangao na kupinga vikali kauli za Mkuu wa Wilaya ya Temeke Ndg. Sixtus Mapunda kuhusu mpango wa kuhamisha wakazi na kuathiri uwepo wa kata zipatazo 10 katika Wilaya ya Temeke kwa madai ya kupisha ujenzi au shughuli za Bandari Kavu (ICDs). Kauli hiyo ilitolewa tarehe 27 Agosti 2026 akiwa katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ndg. Albert Chalamila, kwenye eneo la Kirimanjaro ICD, Kurasini.
Katika kauli hiyo, Ndg. Mapunda alisema kuwa Manispaa ya Temeke imeandaa kata 10 nyingine kufuata mfano wa Kurasini kwa ajili ya matumizi yanayohusiana na Bandari, huku akieleza kuwa wananchi wanapaswa kuelewa kuwa ‘Bandari haihami, ila sisi wanadamu tunaweza kuhama.
Inasitikisha sana, ingawa haishangazi kusikia hivyo kutoka Viongozi wa CCM kutoa kauli hizo katika hali ambayo Dar es Salaam imeshuhudia ongezeko kubwa la bandari kavu, vituo vya makasha na maghala ya mizigo. Utitiri huu umechangia msongamano mkubwa wa malori, foleni kubwa barabani, uharibifu wa barabara, ucheleweshaji wa mizigo, kuongezeka kwa gharama za biashara na kuvurugika kwa maisha ya wananchi.
Kauli ya awali ~ DC Mapunda: Baada ya Kurasini, Temeke tumetenga Kata 10 nyingine kwa matumizi ya Bandari
ACT Wazalendo Mkoa hatutakubali wananchi wa Temeke kuwa wahanga wa uzembe wa Serikali katika mipango miji na usimamizi wa sekta ya usafirishaji. Hatutakubali kata za wananchi kufutwa, wakazi kuhamishwa na maisha yao kuvurugwa wakati Serikali yenyewe imeshindwa kutumia maeneo ambayo tayari iliyatenga na kuyawekea miundombinu kwa ajili ya shughuli za bandari kavu.
Serikali tayari ilitenga na kuendeleza eneo la Kwala, Mkoa wa Pwani, kwa madhumuni ya kuhudumia shughuli za bandari kavu. Eneo hilo limeunganishwa na miundombinu muhimu ya usafirishaji na lilikusudiwa kupunguza msongamano wa mizigo katika Jiji la Dar es Salaam.
Kwa hiyo, ni kinyume cha mantiki kwa Serikali kushindwa kutumia kikamilifu Kwala halafu leo ije na mpango wa kufuta kata na kuwahamisha wananchi wa Temeke ili kupisha shughuli ambazo zinaweza na zinapaswa kupelekwa nje ya Jiji la Dar es Salaam.
ACT Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam tunaendelea kuunga mkono tamko la Waziri Kivuli wa Miundombinu, Ujenzi na Uchukuzi wa ACT Wazalendo Ndg. Abdallah Mtutura la kutaka bandari kavu ziondolewe katikati ya Jiji la Dar es Salaam, kusitisha utolewaji wa vibali vipya na shughuli hizo kuelekezwa Kwala.
Aidhai, tunamtaka Mkuu wa Wilaya wa Temeke kusitisha mara moja mpango wowote wa kuwahamisha wakazi au kufuta kata za Temeke kwa kisingizio cha kupisha Bandari Kavu;
Iwapo Serikali itaendelea kupuuza sauti za wananchi na kusukuma mbele mpango huu wa kuwaondoa wakazi wa Temeke katika maeneo yao, ACT Wazalendo itahamasisha wananchi wa Temeke na Dar es Salaam kwa ujumla kutumia haki yao ya kikatiba ya kuandamana kwa amani na kupaza sauti dhidi ya mpango huu.
Tunawaambia wananchi wa Temeke kuwa hatutawaacha peke yao katika mapambano haya. Tutatumia njia zote halali kupinga mpango wowote unaolenga kuwanyang'anya wananchi makazi yao na kufuta maeneo yao kwa sababu ya kushindwa kwa Serikali kupanga mji na kusimamia shughuli za bandari.
Imetolewa na:
Ndg. Felix Kamugisha
Katibu wa Mkoa, Dar es Salaam
3 Septemba, 2026
Maendeleo na siasa havijawahi kukaa room moja

Wanamtandao wamenunua Wilaya