Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 593
- 1,376
Wakuu,
Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Isihaka Mchinjita amesema kuwa Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa chama hicho Abdul Nondo amepigwa sana na kuumizwa sana pia kwa hali aliyonayo hawezi kuzungumza vizuri.
Mchinjita ameyasema hayo usiku huu (2:15 Disemba 02, 2024) baada ya kufika katika hospitali ya Aga Khan alipolazwa Nondo na kueleza kuwa baada ya kutekwa kwa Nondo alifungwa kitambaa cheusi na kupigwa sana huku akitishiwa kifo.
Pia soma: Dar: Abdul Nondo amechukuliwa na Watu wasiojulikana katika mazingira ya utatanishi Kituo cha Mabasi cha Magufuli
“maelezo yake ni kwamba alipotolewa pale stendi ya Magufuli alifungwa kitambaa kwa hiyo hakuwa anaona baada ya hapo amekuwa akipigwa muda mrefu baadae walisitisha kwenye eneo ambalo halifahamu baadae alitupwa pale Coco Beach ambapo walimfungua kitambaa na pingu na alibaini kwamba yupo Coco Beach na akaomba msaada”.
Soma pia: Taarifa ya Polisi kuhusu kutekwa kwa Abdul Nondo sijaielewa
Kuhusu kitu ambacho Nondo alikuwa anaambiwa na watekaji Mchinjita amesema “maelezo anaytoa (Abdul Nondo) ni kwamba alipigwa na alikuwa kwenye kitisho cha kifo na yeye alipopelekwa pale Coco Beach na pale baharini alijua ni hatma yake kwa sababu alikuwa amefungwa na wakamuacha kwenye lile eneo lakini baadae akatishwa tu kwamba akikamatwa tena basi hawatomuachia”.