Pre GE2025 ACT waongea baada ya Nondo kupatikana, wasema alipigwa sana na alikuwa kwenye kitisho cha kifo

Pre GE2025 ACT waongea baada ya Nondo kupatikana, wasema alipigwa sana na alikuwa kwenye kitisho cha kifo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Jeshi la polisi lipo siku litapigwa na kitu kizito hawataamini macho yao.
 
D

Uh! Umeshangaza sana. Yaani mtu akiwa kwenye hali mbaya sana, watu hawawezi kumsaidia!! Wakati kwa watu wenye akili timamu, unachokisema ni kinyume chake. Kwa mwenye akili timamu, mtu aliyepo kwenye hali mbaya sana ndiye watu humsaidia kwa haraka.

Mara 3 nimewahi kuwachukua watu waliogongwa na magari, na kuwakimbiza haraka hospitali, wakiwa hawajitambhi, na sijui kama walipona au la, ila mimi nilitekeleza wajibu wangu wa kiutu.

Polisi walinishukuru sana na kusema kuna watu wa ajabu, wakiona mtu amegongwa na gari, wanamkimbia huyo majeruhi, huku wakieneza maneno ya uwongo, kuwa eti ukimsaidia aliyegongwa na gari, unageuziwa kesi kuwa ni wewe uliyemgonga. Labda hao ndiyo wenye mawazo kama hayo ya kwako.

Mimi katika hizo mara zote 3, polisi walinishukuru, na hakuna hata mmoja aliyewahi kunisumbua kwa lolote, zaidi ya kuombwa tu details zangu.
Unapajua coco beach saa nne Usiki panakuwaje
 
Zanz hatujawahi kusikia utekaji na namna hii
Zanzibar ndio walianzisha hizi drama za kutekwa, bara wakaiga. Kumbuka mashehe wa uamsho walitekwana baadaye wakakutwa porini, Sasa kutekwa imekuwa dili bara. ACT wameona CDM wanafaidi sana na hizi drama za utekaji nao wameingia sasa
 
Ondoa uchama mkuu hii isseu ukute hata wasio na chama wanatekwa
 
Amejiuliza maswali ya ufahamu kama ambavyo mtu mwenye akili timamu anapaswa kufanya.
Act wazalendo walienda kituoni gogoni wakakuta gari lililombeba nondo linabadilishwa plate number.unataka kusema Nini?
Ifike hatua TUACHE MZAHA NA MASIKHARA KWENYE MAISHA YA WATU.
 
Mhhhh.....
Mbona tena maelezo ya mwenyekiti hayaeleweki..🤔

Wakati anapigwa alikua anaambiwa nini??

Alipo tupwa coco, aliomba msaada kwa nani??

Kidogo inafikirisha usiku wa saa nne/tano unapo omba msaada eneo kama koko nani atakuamini na kubeba msala huku akiona muhusika anahali mbaya??
Au ndio tuhitimishe kama wahenga walivyosema mganga karudisha kuku...😜
Acha mambo hayo unajifanya huelewi au kwa sababu hajatekwa ndugu yako
 
Wakuu,

Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Isihaka Mchinjita amesema kuwa Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa chama hicho Abdul Nondo amepigwa sana na kuumizwa sana pia kwa hali aliyonayo hawezi kuzungumza vizuri.

Mchinjita ameyasema hayo usiku huu (2:15 Disemba 02, 2024) baada ya kufika katika hospitali ya Aga Khan alipolazwa Nondo na kueleza kuwa baada ya kutekwa kwa Nondo alifungwa kitambaa cheusi na kupigwa sana huku akitishiwa kifo.

Pia soma: Dar: Abdul Nondo amechukuliwa na Watu wasiojulikana katika mazingira ya utatanishi Kituo cha Mabasi cha Magufuli

“maelezo yake ni kwamba alipotolewa pale stendi ya Magufuli alifungwa kitambaa kwa hiyo hakuwa anaona baada ya hapo amekuwa akipigwa muda mrefu baadae walisitisha kwenye eneo ambalo halifahamu baadae alitupwa pale Coco Beach ambapo walimfungua kitambaa na pingu na alibaini kwamba yupo Coco Beach na akaomba msaada”.

Soma pia: Taarifa ya Polisi kuhusu kutekwa kwa Abdul Nondo sijaielewa

Kuhusu kitu ambacho Nondo alikuwa anaambiwa na watekaji Mchinjita amesema “maelezo anaytoa (Abdul Nondo) ni kwamba alipigwa na alikuwa kwenye kitisho cha kifo na yeye alipopelekwa pale Coco Beach na pale baharini alijua ni hatma yake kwa sababu alikuwa amefungwa na wakamuacha kwenye lile eneo lakini baadae akatishwa tu kwamba akikamatwa tena basi hawatomuachia”.
Mimi nampa pole sana Nondo ila chama cha ACT sikiamini sana hasa kiongozi wake mstaafu hiki chama kimekaa kimaadeal deal tu na asilimia kubwa ya waanzilishi wa chama hiki hawakutoka vizuri kwenye vyama walivyotoka. Ngoja tuine jinsi hili sakata linavyoklwenda kwa mawazo yangu na mimi hisia zangu zinavyonoutuma naona kama sarakasi fulani zakufifisha mjadala wa uchaguzi wa serikaali za mitaa Aidha ACT walihusishwa au haswakuhussishwa moja kwa moja ,mimi niendelee kuwadhauri watu pamoja na sakata hilli lakinii mijadala ya nini kilicho jiri ktk uchaguzi wa serkali za mitaa na mambo yaliyojiri wakati wa huo utekaji uchagguzi yaendelee ujhadiliwa. Mimi nauamini kwa asilimia 100% uongozi wa sasa wa wananchi ACT lakini wajue kabisa wenye hocho chama wasnaweza kuwauza wakati wowote wskilleta jeuri. ACT kkinaendelea kujijjenga na kuimarika ila msingii uikiwa mbovu jengo kuimarika ni kazi sana.
 
Je, na wewe uimejiuliza Sativa alinusurikaje?
Je, wanaosema ni Kudra ya mwenyezi Mungu huwa chanzo ni nini hadi watamke hivyo?
Mimi yote najiuliza na nimeshajiuliza.

All in all kwa upande wangu naamini alitekwa.
 
Wakuu,

Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Isihaka Mchinjita amesema kuwa Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa chama hicho Abdul Nondo amepigwa sana na kuumizwa sana pia kwa hali aliyonayo hawezi kuzungumza vizuri.

Mchinjita ameyasema hayo usiku huu (2:15 Disemba 02, 2024) baada ya kufika katika hospitali ya Aga Khan alipolazwa Nondo na kueleza kuwa baada ya kutekwa kwa Nondo alifungwa kitambaa cheusi na kupigwa sana huku akitishiwa kifo.

Pia soma: Dar: Abdul Nondo amechukuliwa na Watu wasiojulikana katika mazingira ya utatanishi Kituo cha Mabasi cha Magufuli

“maelezo yake ni kwamba alipotolewa pale stendi ya Magufuli alifungwa kitambaa kwa hiyo hakuwa anaona baada ya hapo amekuwa akipigwa muda mrefu baadae walisitisha kwenye eneo ambalo halifahamu baadae alitupwa pale Coco Beach ambapo walimfungua kitambaa na pingu na alibaini kwamba yupo Coco Beach na akaomba msaada”.

Soma pia: Taarifa ya Polisi kuhusu kutekwa kwa Abdul Nondo sijaielewa

Kuhusu kitu ambacho Nondo alikuwa anaambiwa na watekaji Mchinjita amesema “maelezo anaytoa (Abdul Nondo) ni kwamba alipigwa na alikuwa kwenye kitisho cha kifo na yeye alipopelekwa pale Coco Beach na pale baharini alijua ni hatma yake kwa sababu alikuwa amefungwa na wakamuacha kwenye lile eneo lakini baadae akatishwa tu kwamba akikamatwa tena basi hawatomuachia”.
Hawa act si ni watoto penwa wa imekuwaje?
 
Pia soma:

Kiongozi wa Ngome ya vijana wa upinzani Tanzania atupwa ufukweni baada ya kutekwa nyara​

2 Desemba 2024

Tzouthl.b

Image: ACT Wazalendo

Kiongozi wa ngome ya vijana wa upinzani Tanzania ACT Wazalendo, Abdul Nondo amepatikana baada ya kutupwa ufukweni, chini ya siku moja baada ya kuripotiwa kutekwa nyara katika jiji kuu la Dar es Salaam.

Chama chake, ACT Wazalendo, kinasema Nondo alipigwa na kujeruhiwa vibaya na amelazwa hospitalini.

Naibu Mwenyekiti wa chama hicho, Isihaka Mchinjita, alisema Nondo amezibwa macho na kushambuliwa mara kwa mara huku akitishiwa kuuawa.

Polisi wametoa taarifa kuthibitisha kisa hicho katika ufukwe wa Coco beach Oysterbay jijini Dar es Salaam siku ya Jumapili usiku, wakisema wanachunguza kisa hicho.

Walisema alikuwa ametelekezwa ufukweni na watekaji wake na aliomba msaada kwa mwendesha teksi ya pikipiki bodaboda , ambaye alimpeleka katika ofisi za chama.

“Kutoka hapo viongozi wa chama walimkimbiza hospitalini kwa matibabu. Tunachunguza na tutachukua hatua za kisheria,” msemaji wa polisi David Misime alisema Jumatatu asubuhi.

Baada ya kumtembelea hospitalini, Mchinjita alisema katika taarifa yake ya awali saa 7 usiku , kwamba Nondo alipigwa "muda mrefu" kabla ya kutupwa ufukweni ambako watekaji "walimvua kitambaa machoni na kumpiga. pingu”.

"Nondo alisema waliomteka nyara walimtisha na kumuonya kwamba wakimkamata tena, hawatamuokoa maisha yake," aliongeza. Sababu ya kutekwa nyara kwake haijabainika.

Siku ya Jumapili, ACT Wazalendo kilisema Abdul Nondo alinyakuliwa dakika chache baada ya kuwasili kutoka eneo la Magharibi mwa nchi la Kigoma ambako alikuwa akiwapigia kampeni wagombea wa chama hicho katika uchaguzi wa mitaa uliofanyika wiki iliyopita uliogubikwa na utata kiasi kuitwa uchafuzi wa uchaguzi wa TAMISEMI 2024

.
Alikuwa amechukuliwa kutoka kituo cha basi jijini Dar es Salaam alfajiri ya Jumapili na watu wawili waliokuwa wakisafiri kwa gari jeupe la magurudumu manne.

Polisi sasa wanasema uchunguzi unaendelea ili kubaini washukiwa na kubaini nia yao.
Tukio hili linafuatia kutekwa nyara na kuuawa kwa kiongozi mwandamizi kutoka chama kikuu cha upinzani CHADEMA mwezi Septemba 2024.

Katika utekaji wa kiongozi mwandamizi, Ali Mohamed Kibao wa CHADEMA alitolewa kwenye basi na kupigwa kisha kumwagiwa tindikali. Rais Samia Suluhu Hassan alikemea tukio hilo na kutaka uchunguzi wa mauaji hayo ufanyike.
Chanzo: BBC
 
Mhhhh.....
Mbona tena maelezo ya mwenyekiti hayaeleweki..🤔

Wakati anapigwa alikua anaambiwa nini??

Alipo tupwa coco, aliomba msaada kwa nani??

Kidogo inafikirisha usiku wa saa nne/tano unapo omba msaada eneo kama koko nani atakuamini na kubeba msala huku akiona muhusika anahali mbaya??
Au ndio tuhitimishe kama wahenga walivyosema mganga karudisha kuku...😜
Aliomba msaada kwa bibi yako.
 
Ushrikiano uliokuwepo kwenye hii kadhia kati ya viongozi ACT na polisi ni kama ule wa yule mwandishi aliotekeshwa na wanaosemekana ni wafanyabiashara wenzake. Nasubiri pongezi kwa jeshi la polisi kutuka ACT
Acha roho mbaya. Nd mana mmeenguliwa kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa!! Mavi kabisa ww
 
Inaonekana Kuna ukweli unaujua.ebu tuambie tusije kuwapa lawama polisi bure
Wewe ume elewaje, kwani?
Si hayo kauliza maswali. Umejaribu kujibu hata moja kati ya hayo maswali, badala ya wewe kujazia tu tafsiri yako, ambayo nayo hukutaka kuieleza hapa?
 
Wewe ume elewaje, kwani?
Si hayo kauliza maswali. Umejaribu kujibu hata moja kati ya hayo maswali, badala ya wewe kujazia tu tafsiri yako, ambayo nayo hukutaka kuieleza hapa?
Umekielewa ulichoandika?au na wewe mwili mkubwa akili KISODA?
 
Back
Top Bottom