Mkuu 'Bams', nadhani hukuelewa alicho lenga aliye uliza maswali (Ushman).D
Uh! Umeshangaza sana. Yaani mtu akiwa kwenye hali mbaya sana, watu hawawezi kumsaidia!! Wakati kwa watu wenye akili timamu, unachokisema ni kinyume chake. Kwa mwenye akili timamu, mtu aliyepo kwenye hali mbaya sana ndiye watu humsaidia kwa haraka.
Mara 3 nimewahi kuwachukua watu waliogongwa na magari, na kuwakimbiza haraka hospitali, wakiwa hawajitambhi, na sijui kama walipona au la, ila mimi nilitekeleza wajibu wangu wa kiutu.
Polisi walinishukuru sana na kusema kuna watu wa ajabu, wakiona mtu amegongwa na gari, wanamkimbia huyo majeruhi, huku wakieneza maneno ya uwongo, kuwa eti ukimsaidia aliyegongwa na gari, unageuziwa kesi kuwa ni wewe uliyemgonga. Labda hao ndiyo wenye mawazo kama hayo ya kwako.
Mimi katika hizo mara zote 3, polisi walinishukuru, na hakuna hata mmoja aliyewahi kunisumbua kwa lolote, zaidi ya kuombwa tu details zangu.
Huo utu wema kama ulio uonyesha wewe ndiyo inayo takiwa hiyo. Hukuwa na hofu yoyote na usalama wako ulipo kuwa unafanya wema huo. Maeneo ya hapo ulipo toa msaada hukuwa na mashaka nayo; na pengine ilikuwa ni mchana.
Hapo 'Coco beach' pana sifa yake; na wakati wenyewe ni usiku!
Huyo/hao wasamaria wema pengine walikuwa ni watu zaidi ya mmoja. Siyo rahisi kwa mtu mmoja kusimama maeneo hayo usiku
Sasa, huyu /hawa wasamaria wema walombwa na majeruhi awahishwe kwenye ofisi za chama; au hospitalini, au hata katika mikono ya polisi kwa usalama? Ni nani hawa/huyu msamaria mwema?
Wewe polisi wali kushukuru; kwa sababu ulifuata taratibu za kujitambulisha kwao, au siyo?