D
Uh! Umeshangaza sana. Yaani mtu akiwa kwenye hali mbaya sana, watu hawawezi kumsaidia!! Wakati kwa watu wenye akili timamu, unachokisema ni kinyume chake. Kwa mwenye akili timamu, mtu aliyepo kwenye hali mbaya sana ndiye watu humsaidia kwa haraka.
Mara 3 nimewahi kuwachukua watu waliogongwa na magari, na kuwakimbiza haraka hospitali, wakiwa hawajitambhi, na sijui kama walipona au la, ila mimi nilitekeleza wajibu wangu wa kiutu.
Polisi walinishukuru sana na kusema kuna watu wa ajabu, wakiona mtu amegongwa na gari, wanamkimbia huyo majeruhi, huku wakieneza maneno ya uwongo, kuwa eti ukimsaidia aliyegongwa na gari, unageuziwa kesi kuwa ni wewe uliyemgonga. Labda hao ndiyo wenye mawazo kama hayo ya kwako.
Mimi katika hizo mara zote 3, polisi walinishukuru, na hakuna hata mmoja aliyewahi kunisumbua kwa lolote, zaidi ya kuombwa tu details zangu.