Pre GE2025 ACT waongea baada ya Nondo kupatikana, wasema alipigwa sana na alikuwa kwenye kitisho cha kifo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hii nchi kupaza sauti tu hakutoshi bali ni kuchukua hatua. Haiwezekani watu tukaaminishwa kuwa tuko huru na wakati tunanyimwa hata tu uhuru wa kuongea. Ifike wakati tuseme sasa basi. Ila kama tutaendelea kulialia hivi hata wao wahusika wa matukio hayo watajiona wameweza. Matukio haya yanaumiza sana ila kama hayajakugusa moja kwa moja yawezekana usinielewe.
 
Huu ndio utu kuna watu hawana utu kabisa!! Eti msalaba! Jamani!!
 
Ushrikiano uliokuwepo kwenye hii kadhia kati ya viongozi ACT na polisi ni kama ule wa yule mwandishi aliotekeshwa na wanaosemekana ni wafanyabiashara wenzake. Nasubiri pongezi kwa jeshi la polisi kutuka ACT
 
Isipokuwa tuwe wakweli ACT wamepambana sana kwa uharaka mkubwa na kufanikisha kumpatia. CDM wao hawako makini kwa mfano akina Soka na wengineo
 
Isipokuwa tuwe wakweli ACT wamepambana sana kwa uharaka mkubwa na kufanikisha kumpatia. CDM wao hawako makini kwa mfano akina Soka na wengineo
Hawakua na nia ya kummaliza, Mzee Kibao mbona taarifa zilitoka mapema sana na CDM walipiga kelele sana, Akina Soka CDM pia walipambana na walipaza sana Sauti mpaka mwenyekiti akaitisha waandishi wa habari akaweka wazi mchoro wa tukio la akina Soka, Ulitaka wapambaneje?

Vipi Kuhusu Kombo Wa Tanga CDM walipaza Sauti kwa Mwezi Mzima ndo Polisi wakaja kusema wanae, Unataka CDM wapambaneje waunde jeshi?

Huu mkumbo wa kusifia eti ACT wamepambana naona ndo Ajenda yenyewe, Huu utekwaji wa Nondo unaanza kutia Mashaka kwa hizi sifa yawezakua hii ilikua drama
 
Je, na wewe uimejiuliza Sativa alinusurikaje?
Je, wanaosema ni Kudra ya mwenyezi Mungu huwa chanzo ni nini hadi watamke hivyo?
 
Point ya msingi na weledi haijaguswa, Je Nondo alipewa maelekezo gani hata kupelekea kutishiwa kifo endapo angekamatwa mara ya pili? Na maelekezo hayo alipewa kwa masilahi ya nani?
 
Tumuombe Yesu, aondoe viongozi wasio Linda wananchi wake.
Hii 👆 👆 inafikirisha sana. Kumbuka kwamba Viongozi waliopo madarakani tumewaweka uongozini ss wenyewe (mimi na wewe)tena kwa Hiari ya Utashi wetu(Free Will) na hatukumshirikisha huyo Yesu. Sasa iweje leo unataka umsumbue Yesu?? Mbona unataka kumwonea Yesu?
 
waliokuwa wanampiga walitaka nini kwake? au walikuwa wakimuulia nini? hawezi kupigwa bila sababu hata kama ni ya kijinga
 
waliokuwa wanampiga walitaka nini kwake? au walikuwa wakimuulia nini? hawezi kupigwa bila sababu hata kama ni ya kijinga
Tumwombe Mungu amjalie wepesi wa kupona halafu atakuja kusema yy mwenyewe kwa kinywa chake. Kwa sasa ni mgonjwa amelazwa Hospitali.
 
Nawaonea huruma vijana wanasiasa wa Tanzania, mnapoteza muda bure tu kuwapigania hao mnaowapigania, wenzenu hawana time na nyie na wanawadhiaki,


Achaneni na siasa za upinzani Vijana kina Nondo na wengine,pambanieni maisha yenu na familia yenu, Mnaona wenzenu kina Kafulila, Kina joshua Nasary,petrobas Katambi,na wengineo wapo serikalini wanakula maisha,

Mna hatarisha uhai wenu kutetea vibwengo.
Tanzania itaendelea kuwepo hata ikiliwa vipi,

Unganeni na wengine mle mema ya nchi.
 
Umeeleza vizuri uliwakimbiza Hospital sasa kweli unamuokota mtu usiku kaumia sana unampeleka kwenye ofisi ya chama??? mhhh hebu tunyoshe maelezo hapa.
 
anza mkuu toka tu barabarani sisi nyuma yako
 
Una shida gani Kwani!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…