ACT Wazalendo: Abdul Nondo amekutwa na kiwango kikubwa cha sumu mwilini

ACT Wazalendo: Abdul Nondo amekutwa na kiwango kikubwa cha sumu mwilini

Hii mada ilifaa ikae kwenye jukwaa la siasa.

Tukirudi kwenye mada, madaktari wa Bongo wanaweza kutishwa wasiseme ukweli.

Pia, huenda ndio maana hawakumjeruhi sana kwasababu walijua wameshampa sumu itayomdhuru polepole.

Inawezeka watekaji sasa wamebadili style ya kuua/kudhuru wanaowateka kwa kuwadhuru kimyakimya kama hivyo kupunguza kelele za watu.
 
Umeokotwa usiku unasema niliwaambia wanipeleke ofisi ya chama usiku saa 5 sababu watanisaidia sasa kweli saa 5 usiku nani yupo ofisini? kama aliweza kuwapigia simu kwanini asingewapigia pale pale alipopatikana. Huyo aliyemuokota mbona haonekani? kweli hakuna hata mashahidi.
Umeona eeh.

Inawezekana alijiteka, akajipiga hadi kujivimbisha mikono mgongo na nyayo, akajiwekea sumu, kisha kwenda kujitupa coco beach, na baadae kuita watu wampeleke ofisini kwao.

Au unaonaje?
 
Tlaatlaah Lucas Mwashambwa na Shangazi yenu The Sunk Cost Fallacy 2 njaa za mabosi wenu zinamalizia kuligawa Taifa vipande vipande.
gentleman,
aliegawanyika ni wewe pekeyako na viongozi waandamizi wa chama chako amabo hawewezi tena kutizamana macho kwa macho. Ni suala la muda tu pambano lianze rasmi...

Tanzania ni moja,
na itabaki kua moja chini ya jemedari mkuu wa nchi moja, na kipenzi cha waTanzania Dr.Samia Suluhu Hassan na si vinginevyo :pulpTRAVOLTA:
 
Umeokotwa usiku unasema niliwaambia wanipeleke ofisi ya chama usiku saa 5 sababu watanisaidia sasa kweli saa 5 usiku nani yupo ofisini? kama aliweza kuwapigia simu kwanini asingewapigia pale pale alipopatikana. Huyo aliyemuokota mbona haonekani? kweli hakuna hata mashahidi.
Aonekane kivipi Ndugu yangu?
Unataka ushuhuda UPI apa mkuu
 
Atujafikia uko
😏
1000016796.jpg
 
Umeokotwa usiku unasema niliwaambia wanipeleke ofisi ya chama usiku saa 5 sababu watanisaidia sasa kweli saa 5 usiku nani yupo ofisini? kama aliweza kuwapigia simu kwanini asingewapigia pale pale alipopatikana. Huyo aliyemuokota mbona haonekani? kweli hakuna hata mashahidi.
Weye mjinga sana walipokelewa na walinzi wa chama khanisi Waheed weye
 
Abdul Nondo akutwa na kiwango kikubwa cha sumu mwilini

Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT-Wazalendo Taifa Ndg. Abdul Nondo jana tarehe 03 Disemba 2024, alifanyiwa upasuaji mdogo kwenye unyayo baada ya madakatri wanaomuuguza katika hospitali ya Aga Khan kubaini uwepo wa mivunjiko midogomodogo iliyotokana na kuumizwa vibaya wakati alipotekwa na baadae kutelekezwa katika ufukwe wa Bahari wa Coco Beach jijini Dar eSalaam.

Aidha Madaktari wamedai mwili wa Abdul Nondo unaonyesha kuwa na kiwango kikubwa cha Sumu ambayo mpaka sasa hawajajua kama zimetokana na athari za kupigwa na kuteswa au kama alipewa kitu chenye sumu na watekaji wake.

Kutokana na hali hiyo Uongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa, umewaomba madaktari kumfanyia Uchunguzi zaidi kwa ajili ya kubaini aina ya Sumu iliyo mwilini mwake na kama zimetokana na kupewa Sumu
Kwa sasa hali ya Mwenyekiti Abdul Nondo bado si nzuri, mikono yake imevimba na ana maumivu makali mwilini japo madaktari wanaendelea kupambana kuhakikisha afya yake inaimarika na kurudi kwenye hali yake ya kawaida.

Tunawashukuru watanzania wote kwa maombi yenu kwa Mwenyekiti wetu, tunaomba tuendelee kumwombea wakati madaktari nao wakiendelea kupambana kurejesha afya yake katika hali ya kawaida.
Wampeleke India kabla haujawa too late.
 
Back
Top Bottom