ACT Wazalendo: Abdul Nondo amekutwa na kiwango kikubwa cha sumu mwilini

ACT Wazalendo: Abdul Nondo amekutwa na kiwango kikubwa cha sumu mwilini

Umeokotwa usiku unasema niliwaambia wanipeleke ofisi ya chama usiku saa 5 sababu watanisaidia sasa kweli saa 5 usiku nani yupo ofisini? kama aliweza kuwapigia simu kwanini asingewapigia pale pale alipopatikana. Huyo aliyemuokota mbona haonekani? kweli hakuna hata mashahidi.
Hivi unaonaje kama ungekuwa unachukua miaka au umri wa watu wengine unajiongezea ili uishi miaka mingi na uriowapola ukiwaacha wakijifia,je ungeuwa wangapi?una roho mbaya sana
 
Hivi unaonaje kama ungekuwa unachukua miaka au umri wa watu wengine unajiongezea ili uishi miaka mingi na uriowapola ukiwaacha wakijifia,je ungeuwa wangapi?una roho mbaya sana
Sasa roho mbaya kuuliza ni nani huyo alimuokota na kumpeleka ofisini?
 
Sasa roho mbaya kuuliza ni nani huyo alimuokota na kumpeleka ofisini?
zamu yenu inakuja kama hutalipiya wewe watalipia wanao, Mozambique wameshaanza kunyolewa wananchi wanachoma ofisi za Frelimo na kuvamia vituo vya polisi na kufungua magereza kuwaachia wafungwa
 
zamu yenu inakuja kama hutalipiya wewe watalipia wanao, Mozambique wameshaanza kunyolewa wananchi wanachoma ofisi za Frelimo na kuvamia vituo vya polisi na kufungua magereza kuwaachia wafungwa
Anza wewe kama kidume kweli
 
Abdul Nondo akutwa na kiwango kikubwa cha sumu mwilini

Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT-Wazalendo Taifa Ndg. Abdul Nondo jana tarehe 03 Disemba 2024, alifanyiwa upasuaji mdogo kwenye unyayo baada ya madakatri wanaomuuguza katika hospitali ya Aga Khan kubaini uwepo wa mivunjiko midogomodogo iliyotokana na kuumizwa vibaya wakati alipotekwa na baadae kutelekezwa katika ufukwe wa Bahari wa Coco Beach jijini Dar eSalaam.

Aidha Madaktari wamedai mwili wa Abdul Nondo unaonyesha kuwa na kiwango kikubwa cha Sumu ambayo mpaka sasa hawajajua kama zimetokana na athari za kupigwa na kuteswa au kama alipewa kitu chenye sumu na watekaji wake.

Kutokana na hali hiyo Uongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa, umewaomba madaktari kumfanyia Uchunguzi zaidi kwa ajili ya kubaini aina ya Sumu iliyo mwilini mwake na kama zimetokana na kupewa Sumu
Kwa sasa hali ya Mwenyekiti Abdul Nondo bado si nzuri, mikono yake imevimba na ana maumivu makali mwilini japo madaktari wanaendelea kupambana kuhakikisha afya yake inaimarika na kurudi kwenye hali yake ya kawaida.

Tunawashukuru watanzania wote kwa maombi yenu kwa Mwenyekiti wetu, tunaomba tuendelee kumwombea wakati madaktari nao wakiendelea kupambana kurejesha afya yake katika hali ya kawaida.
Lipo la kujifunza, kwamba, yeyote yanaweza kumkuta. Kila mtu apinge ukatiri juu ya mtu yeyote.
 
Back
Top Bottom