LGE2024 ACT Wazalendo: Khamis Mbeto Khamis hana haki ya kutupangia njia ya kutumia kupinga Sheria mbovu

LGE2024 ACT Wazalendo: Khamis Mbeto Khamis hana haki ya kutupangia njia ya kutumia kupinga Sheria mbovu

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
KURA YA MAPEMA._page-0001.jpg

KURA YA MAPEMA._page-0002.jpg
MBETO HANA HAKI YA KUTUPANGIA, NJIA YA KUTUMIA KUPINGA SHERIA MBOVU.

Ndugu Wanahabari, awali ya yote nichukue fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kutujaalia uhai na uzima, na ukimya katika nchi hii, pia kuwashukuru nyinyi wanahabari, kwa kuitikia wito wetu, kila pale ambapo tumewaita kuja kwa ajili ya kutusikiliza na kuuhabarisha umma, bila ya kuchoka.

Kwa hakika munafanya kazi kubwa sana

Ndugu Wanahabari, leo tumeamua kuwaita makusudi, kwa lengo la kuuhabarisha umma kutokana na kauli za kihuni zilizotolewa hivi karibuni na Katibu wa Idara Maalum ya Itikadi na Uenezi Zanzibar wa Chama cha Mapinduzi, Ndugu Khamis Mbeto Khamis, kwa Mwenyekiti wetu wa Chama Taifa Mh. Othman Masoud Othman, kuhusiana na kauli yake dhidi ya kura ya Mapema aliyoitoa, Siku ya Jumamosi ya tarehe 16/11/2024, akiwa katika Kongamano la Vijana wa Mkoa wa Kusini Unguja.

Ndugu Wanahabari, sisi Chama Cha ACT Wazalendo, tunaona kauli za ndugu Khamis Mbeto ambazo bila shaka amepata baraka kutoka kwa viongozi wake, ni kauli za kihuni zinazoashiria, mipango na dhamira yao ya mauwaji mengine makubwa waliyoyapanga kuelekea uchaguzi wa 2025, kama walivyotekeleza katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.

Ndugu waandishi wa habari, jambo la kwanza nataka kuliweka wazi hapa kuwa kauli ya Mwenyekiti wetu wa Chama kuhusu kupinga kwetu kura ya Mapema na kumalizana nayo kwa njia yoyote ile kabla ya uchaguzi sio kauli binafsi ya Othman Masoud Othman.

Ni kauli ya viongozi wote wa ACT Wazalendo na inaungwa mkono na wafuasi na wanachama wetu, Umma wanaotuunga mkono upo pamoja na Mwenyekiti wetu.

Pili, ipo hoja ngumbaru inayotolewa naa viongozi wa CCM kuwa kura ya Mapema ipo kisheria na hatuna haja ya kuipinga. Huu ni ulaghai wa kisiasa wa CCM. Napenda nimkumbushe Ndugu Mbeto na viongozi wa CCM, labda kwa umri wake anaweza asilijue hili.

Hata ubaguzi wa Rangi kule Afrika Kusini (Apartheid) ulikuwepo kwa mujibu wa Sheria lakin Dunia nzima ilisimama kuwapinga Makaburu na kwa Tanzania mapambano ya kupinga ubaguzi wa rangi yaliongozwa na Mwalim Nyerere aliekuwa Mwenyekiti wa CCM.

Sasa Kura ya Mapema haina tofauti na sheria ya Ubaguzi wa Rangi. Sisi Chama cha ACT Wazalendo tutawahamasisha wananchi kupinga Sheria mbovu kwa njia yoyote ile kama CCM walivyotuhamasisha kupinga sheria ya Ubaguzi wa Rangi ya Makaburu wa Afrika Kusini. Ni kazi yetu na ni wajibu wote kama chama cha siasa. Mbeto hana haki ya kutupangia njia ya kutumia kupinga sheria mbovu.

Ndugu Wanahabari, ACT Wazalendo hatujawahi kusema tusichikiamini na ambacho hatuwezi kukitekeleza, ikiwa Ndugu Mbeto na Viongozi wake wa Chama Cha Mapinduzi, Wamepanga kuwashughulikia viongozi wetu, jambo hili sio jipya wala geni kwetu, tumeshazoea kupigwa, kuuliwa na tukaachiwa walemavu, mayatima na wajane kutokana na mipango na maelekezo ya Chama Cha Mapinduzi.

Ngugu Wanahabari, ni wazi kwamba CCM hawawezi kushindani, Uchaguzi ulio huru na haki bila ya kuvitumia vyombo vya dola kutekeleza mauwaji na mateso kwa Wazanzibari, kila kinapokaribia kipindi cha uchaguzi, kauli kama hizi za Ndugu Khamis Mbeto sio ngeni wala mpya, ni kauli tulizozizoea kila siku kutoka katika midomo ya Viongozi wa Chama cha Mapinduzi, kila pale wanapoona tayari wamekosa muelekea na kushindwa uchaguzi uliopo mbele yao.

Ndugu Wanahabari, kwetu sisi ACT Wazalendo, suala la Kura ya Mapema, wala hatutafuni Maneno kwamba haitokuwepo wala hatutokubali na kuruhusu kilichotokea katika Uchaguzi wa 2020, tutahakikisha jambo hili tunamalizana nalo mapema, tena mchana kweupi kwa njia yoyote ile.

Sasa ikiwa Ndugu Mbeto amejipanga na vyombo vya Dola kuhakikisha wanawadhibiti na kuwashughulikia Viongozi wetu, hili kwetu sio geni wala jipya, na wala wasisiburi, kipindi hicho cha kuwadhibiti waanze sasa, kwani tunarejea tena kama alivyosema Mwenyekiti wetu Taifa kwamba Uchaguzi wa 2025 hatutafanya kosa, kama ambavyo tumelifanya 2020.

Hatutasubiri kutaangazwa kura ya mapema eti ndio tuje tupinge, hapana hatutafanya kosa hili, Uchaguzi wa 2025 tutamalizana mapema kabla ya kufika Kwenye Uchaguzi.

Ahsante sana kwa kunisikiliza
 
Back
Top Bottom