M-mbabe
JF-Expert Member
- Oct 29, 2009
- 13,203
- 23,027
Wanaonifuatilia humu wanajua mimi ni CCM. Lakini ni ile iliyokuwa CCM ya Mwalimu (RIP mzee wetu), siyo hii CCM ya sasa iliyojaa ulaghai mtupu.
Kutokana na CCM kukengeuka, nimejikuta (siko peke yangu, tupo wengi sana) sina namna bali kuunga mkono jitihada na harakati zote zinazofanywa na vyama mbadala makini, hususani kwa sasa hivi ni ACT-Wazalendo na CHADEMA.
Sote tunakumbuka wakati wa kampeni kuelekea uchaguzi wa October 28, mikutano ya Maalim Seif kule visiwani ilikuwa inajaza nyomi ya kufa mtu. Halkadhalika huku bara, Tundu Lissu nyomi zake zilikuwa kwa mamilioni.
Watanzania wengi tunaamini, na dunia nzima pia inaamini uchaguzi wa mwaka huu Tundu Lissu alishinda kwa kura halali na Maalim Seif naye vivyo hivyo.
Baada ya uchaguzi kuporwa na CCM, wito kutoka kwa Tundu Lissu na Maalim Seif ulikuwa watu wote tuingie barabarani. Ni wito ambao ulikuwa pia ukisisitiziwa sana na viongozi hawa wakati wa kampeni.
Cha ajabu sasa, zile nyomi zilizokuwa zinakuja kwenye mikutano ya kampeni haijulikani zimepotelea wapi, hata ambapo viongozi wakuu wa vyama walipoanza kuwa persecuted na dola, sisi wananchi KIMYAA!
Wenzetu Kenya wana moja ya mifumo mizuri sana ya demokrasia nchini mwao, ni ya kupigiwa mfano si barani Africa pekee bali dunia nzima. Hii imetokana na kuwepo kwa katiba mpya ambayo ililazimika kupatikana baada ya kambi ya upinzani kudhulumiwa uchaguzi. Sote tunajua kilichotokea baada ya hapo.
Pointi yangu ni kwamba hakuna mahali popote chini ya jua mtu anapewa haki yake kwenye kishaza cha dhahabu. Hakuna, hakuna na hakuna!
Viongozi wa ACT-Wazelendo na CHADEMA wamejitahidi sana kwa kadri ya uwezo wao kufanya mass mobilization ili ku replicate zile jitihada za Kenya, lakini matokeo yake ni uthibitisho wa kauli chungu ya mzee Jomo Kenyatta aliyomtamkia Mwalimu Nyerere kuwa "wewe huko Tanzania unaongoza makondoo" (not the exact quote but no mistake about the content).
Sasa, sasa.... kwa vile sisi Watanzania tumeshindwa kuwa wafuasi wazuri wa hawa viongozi wa hivi vyama viwili mbadala, basi tusiviingilie hata kidogo katika maamuzi yoyote watakayoona yanafaa now and going forward kwa ajili ya mustakabali wa vyama vyao.
Kuna mijadala inaendelea kwenye media kutoka kwa wafuasi na wasio wafuasi wa ACT/CHADEMA kuhusu eti wafanye au wasifanye nini baada ya kuporwa uchaguzi na dola, ilihali wananchi hao wameshindwa kufanya kile vyama hivi kiliwaomba kufanya (yaani mass revolt) in the first place. Huu ni unafiki mkubwa wa Watanzania (makondoo a la mzee Jomo) na tabia zetu za kupenda vya kutelezea!
Annoyed,
Mwalimu M-mbabe.