ACT-Wazalendo na CHADEMA wamefanya pakubwa ila sisi Wananchi ndiyo tumewaangusha. Tusiwaingilie katika maamuzi yoyote wanayochukua baada ya Uchaguzi

ACT-Wazalendo na CHADEMA wamefanya pakubwa ila sisi Wananchi ndiyo tumewaangusha. Tusiwaingilie katika maamuzi yoyote wanayochukua baada ya Uchaguzi

Msiwalaumu Wananchi na wapiga kura. Walaumuni viongozi wenu upinzani ambao hawako serious ktk kuleta mabadiliko mbadala wa siasa. Hebu jiulizeni 2015 walituletea mtu anaye "vibrate" na kutaka kutulazimisha awe Rais kwa GIA ya ANGANI. 2020 wanatuletea "mental retarded", "a man of two faces", Shoga mropokaji, Mtume wa mabeberu awe Rais. Hivi huwa wanathani Wananchi ni MABOYA? Kwa nini hawa viongozi wenu hawanaga mipango ya kuandaa na kumnadi mgombea ajaye?
 
Mimi mwenyewe ni chadema, lakini chadema ile ya Dr.Slaa yenye kushindana kwa hoja sio chadema hii ya kudandia kauli za rais kuwa ndio hoja zao za msingi.
Fulani kaguswa na police tu , tayari ni agenda ya chama mihemko mingi kuliko...

Upinzani wa hovyo kabisa
 
Chadema ishajifia kitambo, hawajui hata wanasimamia nini! Hili la kukosa hoja zao, kimewafanya kila siku kudandia nakucheza ngoma ya ccm! Nanukuu "mwaka huu tunashindana na vyama dhaifu haijawahi kutokea" bashiru.
Kabisa
 
Hata huyo Dr. Slaa angekwambia uingie barabarani usingeingia.

Watanzania ni wanafki.
Siyo watanzania wanafiki bali hawana sababu ya msingi na yenye mashiko ya kuandamana , kama mnavyo lazimisha

Alafu kwa nini mnapo zungumzia watanzania ninyi mnaji- exclude[emoji1787][emoji1787] nyie wa wapi?
 
Kimsingi Tu wananchi hawapo aware kabisa na maandamano , ukitaka ukosane na mtanzania mwambie issue za fujo, mtanzania ni mtu wa bata na Amani zaidi ya hapo humpati.

Kuhusu kuibiwa kura mi nakataa, kuna wabunge kweli kura zao zimechakachuliwa ila kwenye uraisi Lissu kapigwa peupeee, na maraia wanajua ndo mana wanaona issue ya maandamano ni ngoma isiyochezeka, wanajua walichomfanyia Lissu kwenye sanduku, in short Tu wananchi ni wajumbe waliochangamka.

Na hii ya kuannounce maandamano ilikuwa ndo the greatest test Kwa Lissu kama kwel anakubalika mioyoni mwa watu na issue imeburst na kuonyesha kuwa most Tanzanian adult people hawamuelewi.
Haswaaa
 
Unatetea lichama ambalo tayari lishakufa. Acha kumsemasema mfu
Inaweza kupita siku kweli hujaitaja CDM?
Kama mnadhani mmeua upinzani basi akili zenu haziko sawa!Tutaendelea kuwanyoosha hapa JF na mtaani kama kawaida!
 
Tz bado kabisa kujitambua itachukua miaka 100. Hutakiwi ku risk maisha yako kwa sababu sabubu yao. Akili za kikoloni bado zipo kwa wengi. Imagine msomi anakwambia anatamani Magufuli aongezewe muda. Kwa hiyo kati ya watanzania wote anaaminika mwenye uwezo ni mmoja tu.
Kama ambavyo inaaminika kuwa katika vyama vyote vya upinzani chadema ndio chama pekee cha upinzani na vyengine vyote vinatumika na serikali,na pia hakuna kiongozi bora hapo chadema kama Mbowe.
 
Watu ambao hata kwenda kupiga kura hawakwenda kama walivyokuwa wakienda kwenye mikutano ya kampeni,mpaka hapo ilipaswa ujiulize kwanini imekuwa hivyo? Na sasa mtu ambaye hata hakuona umuhimu kushiriki zoezi la kupiga kura ndio huyo utegemee aache shughuli zake na kwenda kuandamana?
 
Tusiogope wala kukata tamaa, kila jambo na wakati wake. Kwa mwelekeo huu wa ccm na maamuzi yao kupora will ya Watanzania, upinzani utashamiri zaidi.

Mbinyo wahisani na jumuia za kimataifa,

Waliohidi wananchi hawatomudu hata 40% mfano kujenga majengo sector afya sio issue, vifaa tiba ,madawa vitenganishi ni garama maradufu.

Wawekezaji wakubwa wataendelea kupungua.

Sector utalii bado tete

Miradi mikubwa SGR,Bwawa Nyerere, madaraja nk bado yanahitaji fedha nyingi kilichofanyika hata 25% bado.

Hakika Watanzania tutajuta pamoja.
 
Msiwalaumu Wananchi na wapiga kura. Walaumuni viongozi wenu upinzani ambao hawako serious ktk kuleta mabadiliko mbadala wa siasa. Hebu jiulizeni 1995 walituletea mtu anaye "vibrate" na kutaka kutulazimisha awe Rais kwa GIA ya ANGANI. 2020 wanatuletea "mental retarded", "a man of two faces", Shoga mropokaji, Mtume wa mabeberu awe Rais. Hivi huwa wanathani Wananchi ni MABOYA? Kwa nini hawa viongozi wenu hawanaga mipango ya kuandaa na kumnadi mgombea ajaye?
Kama wapinzani hawafai kama usemavyo kwa nini basi mlifanya ujambazi kwenye uchaguzi? Si mngewaacha wananchi wawakatae wenyewe?
 
Unasema Tundu lissu alishinda kwa Kura halali? Kura zipi ? Au Kura za Twitter na JF! Hivi nyie mbona mnaota Sana CHADEMA! Tena ashukuru Sana hata kupata Kura hizo M1, hivi mlitegemea TL atafikisha Kura 6M kama alizopata lowassa 2015?

Kubalini Uchaguzi mmeshashi dwa ! Kelele hizi tulizitegemea Sana! Na Tatizo lenu hamkubali kuambiwa ukweli.
Na tuliwaonya kuwa watashindwa vibaya sana. Ccm kwa sasa amebadili mbinu za siasa anatumia base yake kule machinations kitu ambacho chadema haina hata shina moja.Halafu utegemee kushinda, kwa taarifa yako sasa hivi ccm inakwenda kuwaingiza mabalozi kwenye payroll ya chama watafanya kazi on daily basis kuhakikisha wanachama wanakuwa wafia chama tayari kwa mapambano ya 2025 kwa ushindi mwingine mnono. Siasa za kuchafuana haxina afya tena
 
Kama wapinzani hawafai kama usemavyo kwa nini basi mlifanya ujambazi kwenye uchaguzi? Si mngewaacha wananchi wawakatae wenyewe?
Kwani hawa waliowakataa kwenye sanduku la kura, na waliokataa kupokea maagizo yao ya kuandamana ulidhani ni ng'ombe? Ni WANANCHI wewe ukiwamo.
 
Wanaonifuatilia humu wanajua mimi ni CCM. Lakini ni ile iliyokuwa CCM ya Mwalimu (RIP mzee wetu), siyo hii CCM ya sasa iliyojaa ulaghai mtupu.

Kutokana na CCM kukengeuka, nimejikuta (siko peke yangu, tupo wengi sana) sina namna bali kuunga mkono jitihada na harakati zote zinazofanywa na vyama mbadala makini, hususani kwa sasa hivi ni ACT na Chadema.

Sote tunakumbuka wakati wa kampeni kuelekea uchaguzi wa October 28, mikutano ya Maalim Seif kule visiwani ilikuwa inajaza nyomi ya kufa mtu. Halkadhalika huku bara, Tundu Lissu nyomi zake zilikuwa kwa mamilioni.

Watanzania wengi tunaamini, na dunia nzima pia inaamini uchaguzi wa mwaka huu Tundu Lissu alishinda kwa kura halali na Maalim Seif naye vivyo hivyo.

Baada ya uchaguzi kuporwa na CCM, wito kutoka kwa Tundu Lissu na Maalim Seif ulikuwa watu wote tuingie barabarani. Ni wito ambao ulikuwa pia ukisisitiziwa sana na viongozi hawa wakati wa kampeni.

Cha ajabu sasa... zile nyomi zilizokuwa zinakuja kwenye mikutano ya kampeni haijulikani zimepotelea wapi, hata ambapo viongozi wakuu wa vyama walipoanza kuwa persecuted na dola, sisi wananchi KIMYAA!

Wenzetu Kenya wana moja ya mifumo mizuri sana ya demokrasia nchini mwao, ni ya kupigiwa mfano si barani Africa pekee bali dunia nzima. Hii imetokana na kuwepo kwa katiba mpya ambayo ililazimika kupatikana baada ya kambi ya upinzani kudhulumiwa uchaguzi. Sote tunajua kilichotokea baada ya hapo.

Pointi yangu ni kwamba hakuna mahali popote chini ya jua mtu anapewa haki yake kwenye kishaza cha dhahabu. Hakuna, hakuna na hakuna!

Viongozi wa ACT na Chadema wamejitahidi sana kwa kadri ya uwezo wao kufanya mass mobilization ili ku replicate zile jitihada za Kenya, lakini matokeo yake ni uthibitisho wa kauli chungu ya mzee Jomo Kenyatta aliyomtamkia Mwalimu Nyerere kuwa "wewe huko Tanzania unaongoza makondoo" (not the exact quote but no mistake about the content).

Sasa, sasa.... kwa vile sisi Watanzania tumeshindwa kuwa wafuasi wazuri wa hawa viongozi wa hivi vyama viwili mbadala, basi tusiviingilie hata kidogo katika maamuzi yoyote watakayoona yanafaa now and going forward kwa ajili ya mustakabali wa vyama vyao.

Kuna mijadala inaendelea kwenye media kutoka kwa wafuasi na wasio wafuasi wa ACT/Chadema kuhusu eti wafanye au wasifanye nini baada ya kuporwa uchaguzi na dola, ilihali wananchi hao wameshindwa kufanya kile vyama hivi kiliwaomba kufanya (yaani mass revolt) in the first place. Huu ni unafiki mkubwa wa Watanzania (makondoo a la mzee Jomo) na tabia zetu za kupenda vya kutelezea!

Annoyed,
Mwalimu M-mbabe.
Very well said , that's the absolute truth. Tukiwa kwenye social media behind the keyboard tunkuwa majabari sana, lakini when push come to shove sote tunaingia mitini never to bee seen again. You have every right to be annoyed.
 
Inaweza kupita siku kweli hujaitaja CDM?
Kama mnadhani mmeua upinzani basi akili zenu haziko sawa!Tutaendelea kuwanyoosha hapa JF na mtaani kama kawaida!
Upinzani haupo siku zote. Leo mkipewa mtihani mdogo tu wa kuwasilisha members Register mtapoteana.Hamjawa tayari kutafuta dola tangu mlipozaliwa 1995 leo miaka 25
 
Kwani hawa waliowakataa kwenye sanduku la kura, na waliokataa kupokea maagizo yao ya kuandamana ulidhani ni ng'ombe? Ni WANANCHI wewe ukiwamo.
You're right!

20201107_150129.jpg
 
Mleta mada, Jeshi la polisi la Tanzania halina uoga kupiga wananchi risasi ili kulinda maslahi ya genge la watu wachache walioko madarakani.

Nchi za wenzetu za Ulaya wanaandamana wakiwa na uhakika hawatopigwa risasi, huku TZ ukiangalia yaliyotokea Zanzibar unaona wazi wako tayari kuua!

Sasa hata ingekuwa wewe, kushiriki maandamano ambayo unaweza kupigwa risasi ukafa, ni vigumu kushiriki.

Kana unataka unazungumzia Arab spring ya waarabu, basi jiulize kabla hawajaingia barabarani walivumilia ujinga kwa miaka mingapi bila kuingia barabarani? - Kisha jiulize kule Misri jeshi lilipoanza kuchapa watu risasi bila wasiwasi hayo maandamano yaliendelea?

Katika nchi ambayo Jeshi liko Tayari kutandika watu risasi kwa sababu tu ya maandamano raia hawako tayari kuuawa. Labda yatangazwe Maandamano ya kuung'oa utawala madarakani na wananchi wawe tayari kwa hilo na wawe tayari kulipa gharama za mabadiriko hayo kwa damu zao ndo utayaona hayo maandamano, lakini na kufanikiwa kwake itategemea mtawala yuko tayari kuua wangapi ili kubaki madarakani. Watawala wengine wako tayari kuua watu hata10000 ili alinde madaraka yake!
 
Pole sana Mwalimu Mbabe

Waliovipa kura hivyo vyama sio wanachama wao pekee bali ni wananchi!.

Hivyo wananchi wana right ya kuvishauri vyama vyao baada ya kushindwa, lazima vifanye the right thing.

Viongozi wa baadhi vyama hawako kwenye the right thinking capacity, they don't think right, kuchanganyikiwa kushindwa kumewafanya kuwa na hali inayotwa preudo insanity, hivyo wanaweza kufanya rational decisions za ajabu.
Ku
Wale viongozi na wanachama wenye muwasaidie viongozi wa vyama vyenu kufanya maamuzi sahihi yenye public interest.

P
Tuanze na madai dhidi ya CCM na serekali.
 
Upinzani haupo siku zote. Leo mkipewa mtihani mdogo tu wa kuwasilisha members Register mtapoteana.Hamjawa tayari kutafuta dola tangu mlipozaliwa 1995 leo miaka 25
Upinzani ni mawazo ya mabadiliko!Na hapo ndipo mnapokwama!Nakuhakikishia hawa wote waliopo akina Mbowe wakijiunga na CCM,mtashangaa bado mitandaoni tunaendelea kuwanyoosha!
 
Back
Top Bottom