Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
ok.🐒ACT Wazalendo tunalaani kwa nguvu zote uamuzi wa Serikali kusitisha kwa miezi sita leseni ya uchapishaji na usambazaji wa Gazeti la MwanaHALISI, kuanzia tarehe 19 Agosti 2026. Serikali imesema hatua hiyo imetokana na madai ya kukiuka viwango vya usahihi, mizania na uthibitishaji wa taarifa.
Tunatambua wajibu wa vyombo vya habari kuzingatia weledi. Hata hivyo, makosa ya kitaaluma yanapaswa kushughulikiwa kwa njia inayolinda uhuru wa habari, haki ya kusikilizwa na maslahi ya umma. Serikali imejipa mamlaka ya kumchunguza, kumsikiliza na kumuadhibu mtoa huduma wa habari. Hii inakinzana na kanuni za haki na utawala bora.
Uhuru wa habari na haki ya kupata, kutoa na kupokea taarifa ni nguzo za Katiba, demokrasia na uwajibikaji wa Serikali. Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 na sheria nyingine zinazoweka mamlaka makubwa Mkurugenzi wa Habari juu ya vyombo vya habari zinapaswa kufutwa na kuondoa vifungu vinavyokandamiza uhuru wa habari.
ACT Wazalendo tunaitaka Serikali isimamishe mara moja adhabu dhidi ya MwanaHALISI na kurejesha leseni yake.
Aidha, tunatoa rai kwa wanahabari, vyama vya Siasa, Azaki na wapenda demokrasia wote nchini kuunganisha nguvu kupigania kuundwa kwa chombo huru cha kitaaluma cha wanahabari kushughulia malalamiko yao; kupigania kufutwa kwa sheria zote kandamizi na kuetetea uhuru wa vyombo vya Habari nchini. Udhalimu dhidi ya mmoja ni udhalimu kwa wote. TUUNGANE SASA dhidi ya dola dhalimu na tishio kwa demokrasia yetu.
Kufungia gazeti ni hatua inayogusa haki ya jamii kupata taarifa na kufuatilia uwajibikaji wa wenye mamlaka. Serikali inayoheshimu demokrasia inapaswa kuvumilia ukosoaji, si kutumia sheria kandamizi kuinyamazisha jamii.
Ndg. Shangwe Ayo
Waziri Kivuli wa Mawasiliano, Habari na Teknolojia ya Habari 19 Agosti, 2026
Bure kabisa nyinyi na ccm ni damu damu acheni utapeliACT Wazalendo tunalaani kwa nguvu zote uamuzi wa Serikali kusitisha kwa miezi sita leseni ya uchapishaji na usambazaji wa Gazeti la MwanaHALISI, kuanzia tarehe 19 Agosti 2026. Serikali imesema hatua hiyo imetokana na madai ya kukiuka viwango vya usahihi, mizania na uthibitishaji wa taarifa.
Tunatambua wajibu wa vyombo vya habari kuzingatia weledi. Hata hivyo, makosa ya kitaaluma yanapaswa kushughulikiwa kwa njia inayolinda uhuru wa habari, haki ya kusikilizwa na maslahi ya umma. Serikali imejipa mamlaka ya kumchunguza, kumsikiliza na kumuadhibu mtoa huduma wa habari. Hii inakinzana na kanuni za haki na utawala bora.
Uhuru wa habari na haki ya kupata, kutoa na kupokea taarifa ni nguzo za Katiba, demokrasia na uwajibikaji wa Serikali. Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 na sheria nyingine zinazoweka mamlaka makubwa Mkurugenzi wa Habari juu ya vyombo vya habari zinapaswa kufutwa na kuondoa vifungu vinavyokandamiza uhuru wa habari.
ACT Wazalendo tunaitaka Serikali isimamishe mara moja adhabu dhidi ya MwanaHALISI na kurejesha leseni yake.
Aidha, tunatoa rai kwa wanahabari, vyama vya Siasa, Azaki na wapenda demokrasia wote nchini kuunganisha nguvu kupigania kuundwa kwa chombo huru cha kitaaluma cha wanahabari kushughulia malalamiko yao; kupigania kufutwa kwa sheria zote kandamizi na kuetetea uhuru wa vyombo vya Habari nchini. Udhalimu dhidi ya mmoja ni udhalimu kwa wote. TUUNGANE SASA dhidi ya dola dhalimu na tishio kwa demokrasia yetu.
Kufungia gazeti ni hatua inayogusa haki ya jamii kupata taarifa na kufuatilia uwajibikaji wa wenye mamlaka. Serikali inayoheshimu demokrasia inapaswa kuvumilia ukosoaji, si kutumia sheria kandamizi kuinyamazisha jamii.
Ndg. Shangwe Ayo
Waziri Kivuli wa Mawasiliano, Habari na Teknolojia ya Habari 19 Agosti, 2026
ACT Wazalendo tunalaani kwa nguvu zote uamuzi wa Serikali kusitisha kwa miezi sita leseni ya uchapishaji na usambazaji wa Gazeti la MwanaHALISI, kuanzia tarehe 19 Agosti 2026. Serikali imesema hatua hiyo imetokana na madai ya kukiuka viwango vya usahihi, mizania na uthibitishaji wa taarifa.